Nisaidieni jamani nifanyeje?

Mkuu, pole sana! Ndo maisha hayo . . . kua uvikute . . . walituambia wahenga wetu. Ndo hayo ya ukubwa. Hakika mama mtoto kakukosea sana. Kaa, utulie uone namna nzuri ya kumsaidia awe mtu mwenye utu, awe mke na si mpita njia, atambue kwamba vyote vilivyoko nyumbani ni vyake na si vya mwingine kiasi cha kutamani kuviiba. Anamwibia nani sasa? Msaidie atambue kwamba wewe ni wake tu hana mpinzani mwingine mtaani kiasi cha kumfanya akulishe madude ya madawa. Huyo mama hajatulia. Anahitaji tuisheni ndefu na iliyojaa upendo. Akikuelewa umempata mkeo asipokuelewa basi mzee beba huo msalaba, utafanyaje!!

Nakushauri usimwache ndoa. Unahitaji kumsaidia abadilike, akue na kukomaa katika maisha hayo. Akuamini!! Poles sana mkuu. Hiyo nayo ni shule ya aina yake. Liwe ni somo tosha kwako na kwetu wengine.
 
kwanza pole sana, pili mshukuru Mungu kwa kuyajua madhaifu ya mwenzako, tatu, ni PM then tutapeana nyenzo nzuri sana kwa faida ya mtoto kisaikolojia
 
Pole sana kaka, ila kila kitu kiko kwenye himaya yako, Unajua! mtu akipenda chongo huona kengeza,
Jaribu kuwa mvumilivu kidogo, na pia jaribu kumshauri mkeo kwenda kusali huenda akimrudia mungu ataona kuwa ni makosa makubwa kwa anayoyafanya. Pia wewe muombe Mungu kwani hakuna mjanja hasa kwenye eneo hilo.
 
kwanza pole sana, pili mshukuru Mungu kwa kuyajua madhaifu ya mwenzako, tatu, ni PM then tutapeana nyenzo nzuri sana kwa faida ya mtoto kisaikolojia


Anyisile! Malafyale! huna haja ya kwenda nyuma ya pazia!

Hapa tunamsaidia Ndugu yetu Eaka lakini pia tunajifunza! Tafadhali tushirikishe hiyo nyenzo!
 
Anyisile! Malafyale! huna haja ya kwenda nyuma ya pazia!

Hapa tunamsaidia Ndugu yetu Eaka lakini pia tunajifunza! Tafadhali tushirikishe hiyo nyenzo!

Asante Maskini,,,
hata mimi nahisi wana JF wana haki ya kujua. Though nitam PM kama alivyotaka ila kwa sasa japo wajuzwe wana JF wote
 
Kwanza pole sana kwa yaliyo kupata .ila shukuru mungu maana amesha kufunulia yote wazi ,kwanza mkeo ni mshrikina ,pili hakupendi kwa dhati ,alikupendea mali zako ,sasa nakushauri , moja ondoa dhana ya kusema nimependa sana jhilo halipo kupenda unaamua kua sasa napenda ,jaribu kusahau ,ila fanyahivyo kama wewe sio muombaji (mtu wa sala) lakini kama ni mtu wa sala inawezekana maombi yako yame jibiwa sasa endelea kuomba maana inawezekana hata huko aliko enda ameenda kwa kwa mganga kukupumbaza ,omba sana ili namganga ashindwe ,tena muombee ili abadilike kabisa aache uchawi akuambie ukweli maana umesha jua nyenzo zake vizuri .alafu akirudi muonyeshe mapenzi ya dhati hadi ajione mkosaji nina uhakika atalia sana ataomba msamaha na atakueleza yote aliyo ya fanya .la mwisho huyo mtoto inavyo onesha una uwezo mkubwa mimi ningeona kumpeleka shule ya bweni ingekua vizuri zaidi .maana anaathirika ki saikolojia .japo najua huyo ndio faraja yako kwa sasa .tena angalia sana huyo mtoto ana weza akawa sio wa kwako .
 
Pole mkuu. Kama imefika mahali akawa hana woga wa kumleta nyumbani jua ushaibiwa sana si chini ya miaka mi-4.na kama kaondoka mwenyewe jua kashafanya mengi kiasi kwamba hata ujasiri wa kutafuta suluhu hana. Funga maduka kama waweza uza gari,tafuta jingine,anza upya jua hapo huna mtu
 
Mimi huwa sifurahii talaka ila kwa hili I am speechless!!! Nendeni kwa wachungaji na maaskofu ili waone wafanyeje kuhusu ndoa ya mwanamke wa waganga wa kienyeji, mzinzi na mwizi wa pesa za familia, a selfish woman ever.

I hope hajawahi msituni kujitundika, to hell with her!!
 
Mkuu this is very sad and depressing!!

Jaribu kufikiria kama ukimkosa utakuwa na hali gani na ni kiasi gani moyo wako umeuizamisha kwa huyo dada; kumbuka
hirizi
accounts za siri
sim cards kibao
uongo
ex-boyfriend nk

Nakushauri upime sana na ujaribu kufanya maamuzi ya kukusaidia wewe, na mtoto na familia yako!!! pima gharama za kuishi na mtu wa namna hiyo na gharama za kumkosa

Kumbuka duniani everyone is replaceable
 
Eeka Mangi. Pole sana bro. Kah! Jamaani! Wanawake wengine bwana sijui wanataka wapawe kitu gani ili waridhike? Sasa kwa style hii sie ambao tunapanga kuoa tutashindwa sasa! Nikioa ntakuwa nashinda home ili wife wasije nichukulia, nikishinda home wife atanikimbia kwasababu ntafulia. Sasa tufanyeje au tuendelee na useja wetu ni mwendo wa kugonga kisha tunatambaa!
Any way! Me ushauri wangu bro, kuwa mpole washirikishe wazee wa pande zote mbili ili muafaka upatikane baina yenu nikiwa na maana ya mkeo akiri makosa yake na kuomba msamaha mbele ya wazee. Kama atakiri na kuomba msamaha, msamehe ndugu yangu (Japo inauma Jikaze).
 
Du! pole kaka. haya ndo yanaitwa masahibu! Hilo ndo tatizo la wanawake wengi. Samahani kusema hivyo kwani si wote lakini wengi. ukitaka kuwaridhisha wanawake kwa kila wanachotaka lazima uishie na dissapointment lkn hilo linawatokea wengi. piga moyo konde. fungua ukurasa mpya
 
Da pole kaka, i hope all is well by now. Wanawake sometimes we can be so stupid
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…