Nisaidieni jamani nifanyeje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nisaidieni jamani nifanyeje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eeka Mangi, Mar 14, 2010.

 1. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sijui naanzia wapi ila yalonikuta sitokaa kusahau maishani mwangu.
  Mke kanitenda. Jamani kanitenda! Lol. Mimi ni mdau katika sekta ya utalii. Nimejibana saana mpaka nikamfungulia mke wang maduka mawili. Moja la nguo na lingine mini superket. Nikampa na gari ndogo ya kutembelea. Siku moja hivi majuzi mtoto akanambia kuna baba mmoja anaendeshaga gari ya mama pindi ninaposafiri. Nikaanza kufanya uchunguzi. Nikaja kugundua huyu jamaa alikuwa mchumbake kabla sijamuoa. Ikabidi siku moja niage naenda nje ya mji. Nilipoondoka tu jamaa naye akaja wakachkua gari yangu huyo wakaondoka! Mbaya sana alikuwa na mtoto wangu wa miaka sita. Akaenda na jamaa mpaka home. Jamaa akamsubiri wife wangu akabadilishe nguo akamwambia mtoto kuwa asjekuniambia kuwa alikuja na uncle...... Mtoto akajakunambia. Hakika iliniuma sana ukizingatia ni mtu ambaye nimejitahidi sana kuwasaidia yeye na familia yake (yaani wakwe zangu). Niliteseka sana rohoni. Juzi usiku kama saa nane hivi ilibidi nimuulize. Alichonambia kuwa huyo uncle ni kama kaka yake na wamekuwa pamoja mtaa mmoja. Nilipomuuliza iweje gari n iliyonunua mimi ampe mtu aendeshe bila idhini yangu? Akajibu aliwhi kumpa gari mara moja tu. Kuhusu kwenda nyumbani akajibu alimkuta njiani na mama yake akampa lifti. lakini yeye haishi mtaa ninaoishi. Nilipowauliza wafanyakazi wa pale dukani wakanambia aliondoka naye toka hapo dukani. Je kama ilikuwa kwa nia njema kwa nini aseme hakutoka naye? Kwa nini amwambie mtoto asinambie?
  The next day alienda kazini kama kawida lakini aliaga kuwa anawahi nyumbani kufanya usafi. Lakini niligundua hali isiyo ya kawaida. Nilipomuuliza maelezo kamili kuhusu tuhuma zake alitoka chumbani na kukimbilia sebuleni. Nilipoamaka jana aliingia chumbani na kuchukua mkoba wake akauficha. Ilibidi tuanze kikao asubuhi baada ya watoto kuondoka. Niliyoyakuata ni mengi. Mi najua kuwa ana bank account 1 tu lakini ana akaunt nyingine 2 bank tofauti na zote zina hela. Slip zinaonyesha kuwa huwa anaweka pesa wakati mimi sipo. Wacha hirizi nilizozikuta ambazo zina jina langu na la mama yangu. Ana simcard zaidi ya 5 na zote zina fedha. Alilia sana, akaomboleza sana, akamwomba mtoto yule mdogo amwoombee radhi mtoto akamkataa.
  Alipoona mambo yamezidi aliondoka kimya kimya tangu jana na sijui yuko wapi.
  Mkiwa kama familia mnanishauri vipi?
   
 2. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  I thought its a right place to run into. But no one have seen importance.
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  mkuu upo mikononi salama mwa wana jf, usijali.

  kwanza pole.
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  una bahati Mungu kakufunulia mapema, kama unampenda hakuna ushauri utakao kufaa, lakini kama una shaka na pendo lenu basi kama alivyotoka hapaswi kurudi hata akilia kwa machozi ya damu

  maana ni fedhea, hivi huyo mtoto wa miaka sita anajifunza nini, mnamtorture mtoto kisaikolojia angali mdogo kabisa, alafu ndio mnaemshirikisha kama shahidi na ndio huyohuyo wa kuwaombea wakosaji msamaha

  YOTE TISA, KUMI HILO LA HIRIZI NI BALAA, SIPATI PICHA UMESHAKULA MATAKATAKA YA AINA GANI? ( maji ya maiti, uchafu wa uk.ni nk),

  POLE MKUU
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Pole sana aisee!! Inasikitisha. Sikuwahi kujua ni kipi kinachomfaa na kumtosha mwanamke. Haupo peke yako bro, wengi wamelizwa na hawa binadamu. Nawafahamu kadhaa walioingia gharama kubwa kuwasomesha wake zao na hata kuwafungulia biashara kama ulivyofanya wewe, mwisho wa siku wakatelekezewa watoto.
  Inaweza kuwa vigumu kwetu kukushauri ufanye nini, lakini sikiliza moyo wako unasema nini. Kwa sababu sisi wengine tutasema umuache au umvumilie wakati moyo wako una jambo lingine la ziada. Ila tu jitahidi uzizuie hasira zako, ili usimdhuru wala usijidhuru. Kuna mabinti wengi tu wazuri huko nje. Ukimkosa huyo unaweza kumpata mwingine aliye bora kumshinda huyo au mbovu zaidi ya huyo. Yote yanawezekana.
  Mshukuru Mungu kwamba Mahirizi yake hayajakudhuru na pia mwombe Mungu akupe ujasiri katika kufanya maamuzi yenye hekima zaidi.
   
 6. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2010
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Pole sana ndio ukubwa huo, mie nakushauri naomba sana umtoe mtoto kwenye hili sakata maana nikumjengea picha mbaya pindi atakapo kua, ni hayo tu hayo, mengine muyamalize tu ki utu uzima.
   
 7. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #7
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu pole sana kwa yaliyo kupata, hii ishu yako ni ngumu kidogo,kwa maelezo yako ya juu juu ina onekana mkeo ana mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa!,swala la kuwa na A/C zaidi ya moja ina maanisha hataki ujue kiasi cha pesa alicho nacho au ana deal nyingine nje ya hiyo miradi uliyo mfungulia (mambo ya ujasiriamali hayo)...Cha muhimu wewe ndiye unamjua mkeo viruzi jaribu kufutilia njendo zake vizuri uweza kujua mengi zaidi.
   
 8. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #8
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hapa ndipo kwenye kasheshe ukijaribu kumuacha tu anarudi kwa mganga wake kwenda kuongeza vikorombwezo! Ndugu kama wewe ni muumini mzuri wa imani yako usitie shaka hata kidogo Mungu anakupenda sana na ndio maana amekuonyesha haya yote mapema kabla hali haijawa mbaya hivyo shukuru sana kwa hilo.
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mkuu pole sana. funga novena hasa kipindi hiki cha kwaresma km ni mkristu otherwise kuwa mwangalifu sana na jaribu kujiwekea mipaka, mtaniwia radhi mama zangu lkn kuna baadhi ya wanawake hawaolewi kwa mapenzi ya dhati huwa wanaangalia una nini, kazi gani utamfanyie kila kitu lkn utaishia kufedheheka tu. kitu kimoja nimejifunza ktk mahusiano, ukimtimizia au kutaka kumridhisha mwanamke kwa kila anachotaka lazima uishie na dissapointment lkn wale wanaowatwanga na kuwapelekesha wake zao ndo mashujaa
   
 10. M

  MaMkwe JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2010
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Usimtushe mwenzio hakuna lolote. Vinginevyo asingeweza kuziona hizo hirizi. Mungu yu pamoja nawe. Omba akupe mke mwema. Mkuu ni heri kuachwa kuliko kuacha. Kwa kuwa kakimbia usimtafute. Toa taarifa polisi na kwa ndugu zake. Wewe ni dume bwana simamia haki yako ya kuwa kichwa cha familia. Jipange upya, utafanikia.
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  Mar 14, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Pole sana Mkuu
   
 12. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mtoto ana hasira kuliko mimi. Hataki hata kumwona. Sasa hivi kaniuliza mbona mama haji kuchukua nguo zake? Nimemwambia kasafiri atakuja tu
   
 13. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Asante mkuu kwa ushauri ila nimefuatilia kwa karibu sana. Hata amejaribu kuniunganisha na jamaa kibiashara na hata kutaka mimi niwe msimamizi wa harusi yake lakini nikanusa harufu fulani hivi. Jamaa akashtuka kuwa nimehisi jambo akakimbia todate sijamwona. Kimsingi sidhani kama naweza kulala naye kitanda kimoja tena. Nafikiri naye anajua hilo ndo maana kajiondokea maana sikumfukuza.
  tatizo kubwa ni hali yangu kwa sasa. Sijui nifanye nini maana kama nimepigwa na mawe mwili mzima. Sijalala kwa siku kadhaa sasa. Na bado sijui nasikia kulala ama ni nini ila mwili wote unaniuma. Ndugu zangu nifanyeje?
   
 14. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Pole sana mkuu! Nimesoma nimesikitika sana ukizingatia mimi na Mwanaume laweza kunikuta vile vile!

  Kwanza tuliza akili mkuu! Katika kipindi kama hiki ni vizuri sana kutochukua mmamuzi makubwa kwa maana yaweza kuwa yanatokana na Hasira na Maumivu ya Moyo!

  Ushauri wangu ni Jaribu kujifunza kuishi bila huyo Mwanamke, siyo Mtu mzuru, ni mshirikina na zaidi anaonekana kutokuwa Mwaminifu!

  Pole sana mkuu Mungu akutie Nguvu na Busara katika Kipindi hiki kigumu but this is the time to evaluate how Mature you are! Handle the matter careful maana destruction haitokuwa kwako pekee hata kwa Mtoto wenu
   
 15. C

  Chief JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2010
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Mangi. Kweli nakuonea huruma sana. Sijui kama una rafiki wa kiume ambaye yupo close na wewe sana na kumweleza ili uweze kushusha mzigo huu kwani usipopata ushauri wa karibu na kuyaweka moyoni tu unaweza kuishia kufanya kitendo kibaya na/au kuathirika kiafya pamoja na kushindwa kutekeleza majukumu yako ya kazi. Hatua moja ya muhimu ni kuwafahamisha wazazi wake na polisi kuhusu kutoroka kwa mkeo. POLE SANA Eeka Mangi. POLE. Mungu akupe uvumilivu mkuu usio kifani uweze kuendelea na shughuli zako kama kawaida. Machozi yamenilengalenga. Mtoto wako awe consolation kwako.
   
 16. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  CarthbetL huwezi amini ila nilimwonya kuwa MIMI KULOGWA ASAHAU TANGU TUKIWA BADO WACHUMBA. Sasa naona kaamini yangu maneno. Atawaloga hao hao waume za watu wenye imani haba sio mimi. Na wanasema mchawi mpe mwanao kaka.
   
 17. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #17
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ni afadhali angekuwa na wazazi. Wote walishafariki na nilishiriki kikamilifu kumsaidia kwa wakati huo. Wacha ndugu zake ambao nimewasaidi kwenye matatizo makubwa hayasemeki. Nasomesha hata watoto wa ndugu zake, mmoja amemaliza form 4 na mwingine yupo class 4 english medium. Mimi ndo baba yake ndo mama yake. Hili la polisi hata mimi nakubaliana na wewe maana huwezi jua. Nimepiga simu kwa ndugu zake wanadai hawajamuona. Mkuu umenipa ushauri bomba sana, naenda polisi sasa hivi
   
 18. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #18
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  baada ya kusoma nimegundua haya

  mkeo: mshirikina
  mwizi
  malaya

  ushauri:

  hakufai huyu kakumulika mchana tayari kaka je usiku inakuwaje, Mungu yu upande wako umelijua hili mapema.

  funga maduka hayo kwa mda,
  mwanamke hana adabu, anatumia jina lako na mma yako kwa ushirikina. pole maana nahisi kuwa umekula vyakula vya ajabu sana na kunywa maji wanayooshea maiti.

  ahana nae kwa kuwa kakimbia wewe kaa kimya, wala usimtafute.

  halua haina kipolo kaka hakufai huyu muuaji na asiyeridhika
   
 19. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #19
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Miaka 20 ya ndoa kaka inaniuma! Mtoto wa kwanza yuko chuo kikuu mtu anafanya haya. Ningekuwa wapi kama wote tungekuwa waaminifu. Duka la nguo tangu jana limefungwa. Hili la supermarket ni vigumu maana vitu vitaharibika. Hivi niko hai watu wanachezea mali zangu je ningekuwa nimekufa?
   
 20. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #20
  Mar 14, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  pole sana mkuu;
  lakini ndo hivyo kuna jamaa yangu huku niliko yeye mkewe nae alimfanyia madudu kama haya,
  sasa kuna siku mgeni alikuja pale kwake ikabidi jamaa amtume mtoto soda dukani, kabla ya kwenda mtoto ikabidi atafute chupa tupu ya soda pale home, mtoto akaingia chumbani kwa wazaz wake aliwahi kuiona chupa huko. ile anaichukua chupa na kuifikisha sebulen sura yule baba ikawa inatokea ndani ya chupa inakuja nje, na yule baba na mgeni walikuwepo pale, wakati sura ya baba inatoka ndani ya chupa, kule dukani kwa mama paka wengi walijaaa ndani ya duka hadi wakawa wanatapakaa nje. palikuwa hapatoshi

  wanaposema kua uyaone sio magorofa!!! haya mambo yapo.

  NB: miaka 20 ya ndoa umekuwa ukiishi katika kifungo, haidhuru mkuu umelijua hili Mungu kaamua kukutoa kifungoni
   
Loading...