Nisaidieni jamani nifanyeje?

Ni afadhali angekuwa na wazazi. Wote walishafariki na nilishiriki kikamilifu kumsaidia kwa wakati huo. Wacha ndugu zake ambao nimewasaidi kwenye matatizo makubwa hayasemeki. Nasomesha hata watoto wa ndugu zake, mmoja amemaliza form 4 na mwingine yupo class 4 english medium. Mimi ndo baba yake ndo mama yake.

Yaani sina hata la kusema.
 
Kwa sababu kaamua kuondoka na hujui alipo kwa sasa huna la kufanya zaidi ya kumwomba Mungu akuepushe na balaa zote. Ila akirudi na kutaka kuendelea kukaa nawe mpeleke kwa viongozi wa Dini yako mkaliongee hilo swala. nadhani wao watakushauri vizuri baada ya kuwasikiliza wote wawili. wewe ndo mwamuzi wa mwisho, kama bado unampenda unaweza ukamsamehe na mkayaanza maisha mapya ingawa kwa kweli ni ngumu sana hasa kwa hayo yote aliyoyafanya
 
Pole Mangi, ni ngumu kupata maneno ya faraja kwa ajili yako kutokana na mkasa huu. Lakini naomba umshukuru Mungu kuwa una uzima na kuwa amekulinda mpaka sasa hata kama mke wako alikuwa na haya mambo machafu aliyokuwa nayo.

Cha msingi tulia, usiamue jambo lolote kwa haraka na then muombe Mungu akusaidie kukuepusha na jambo hili na akupe hekima ya unaamua nini kwa ajili ya faida yako na ya mtoto wako.

Inawezekana Mungu aliyefanya haya yakaeleweka kwako ana jinsi atakovyokusaidia kuondokana na tatizo hili. Ila kwa ujumla huu ni mtihani mgumu katika familia ukizingatia tayari mlikuwa na ndoa ya muda mrefu.
 
Yaani sina hata la kusema.

we ka mimi bubu. Hapa naandika tu. Uzoefu unaniweka hapa. Nimemaliza creti moja ya ndovu na bado nataka kunywa. Hazipandi kichwani hata japo leo nipate kausingizi. Mwenzenu mie naangamia hivihivi. Tangu nimuoe huyu mama sina hata kapembeni, Ama kweli MIE MUME *****
 
Miaka 20 ya ndoa kaka inaniuma! Mtoto wa kwanza yuko chuo kikuu mtu anafanya haya. Ningekuwa wapi kama wote tungekuwa waaminifu. Duka la nguo tangu jana limefungwa. Hili la supermarket ni vigumu maana vitu vitaharibika. Hivi niko hai watu wanachezea mali zangu je ningekuwa nimekufa?

Poleni sana Mkuu kwa hili lililokupata ambalo linasikitisha sana. Nakusifu sana kwa kutochukua hatua mikononi mwako ambapo baadhi ya Wanaume hupenda kufanya hivyo na labda kuishia kumpiga mwanamke kitu ambacho mimi sikiafiki maana ukiwa na hasira kiasi hiki unaweza kumpiga mtu ukaua tayari kukawa na kesi tofauti. Hilo la kwenda polisi ni muhimu sana maana huwezi kujua huyu Mwanamke amefanya uamuzi upi. Kila la heri.
 
Pole sana Mangi, hayo ni majaribu...kuna jambo kuu Mungu anataka ujifunze kutokana na tukio hili. Kama walivyoshauri wengine, tulia na umshirikishe Mungu akuongoze katika kipindi hiki.


Annina
 
Umeenda kwanza Angaza kabla hujaanza hayo mambo mengine,ushauri wa bwelele nenda kwanza Angaza ukitoka hapo nenda bank,then nenda kwa shehe kama muislam,kama mkiristo kwa mchungaji
 
Miaka 20 ya ndoa kaka inaniuma! Mtoto wa kwanza yuko chuo kikuu mtu anafanya haya. Ningekuwa wapi kama wote tungekuwa waaminifu. Duka la nguo tangu jana limefungwa. Hili la supermarket ni vigumu maana vitu vitaharibika. Hivi niko hai watu wanachezea mali zangu je ningekuwa nimekufa?

....... Kumbe ni mama mtu mzima tu huyu,miaka 20 ya ndoa si haba.
Lakini anafanya vitu utafikiri mtoto, jamani wanawake wengine sijui hata wanaakili za aina gani khaaa!!
Huyu mama mshirikina tena sana tu, maana umekuta hadi hirizi kwenye hand bag yake mie naona hafai huyu, atakuja kukumaliza kabisa, usikute hata limbwata alikulisha........ wewe zidi kumuomba Mungu akuepushe na hila za giza.

Zaidi angalia moyo wako unasemaje kuhusu huyo mwanamke, maana wewe ndio unajua zaidi maumivu ya kusalitiwa.
Kama wewe ndio kaka yangu na huyo angekuwa wifi yangu, ningemfanyia kitu mbaya maana anaweza kuhatarisha maisha ya kaka yangu na watoto. Hakuna mtu anayenibore kama mtu mshirikina.
Pole sana Eeka Mangi, Mungu akutie nguvu uweze kupambana na hili jaribu.
 
pole sana.
wakati mwingine kuna watu humu
huwa wanashauri tusioe na tunawaona machizi....
they could be right.....
ulaya katika kila vichaa wanne wanaume,mmoja source ni mapenzi....

ushauri wangu mpe talaka yake haraka sana.........
jizuie hasira,kubali kushindwa
na sometime kushindwa sio ubwege,
u can be a winner in everything in life.
 
Eaka
Habari za siku nyingi
Pole sana kaka yangu nimesoma kisa chako hadi nimetokwa na machozi, ama kweli penye miti hakuna wajenzi yaani huyo mkeo amepata mume anayemjali na bado anamchezea? Sijui niseme nini kaka lakini kwa kuwa ni mke wa ndoa na kwa kuwa hutamkamata live kuwa anatembea na huyo 'uncle' wake huwezikumcharge kwa uasherati (unless una evidence zaidi). Suala la Bank za siri, simcards ni suala la uwazi na uaminifu- akueleze alivyozipata hizo pesa na kwa nini halulueleza; aeleze simcards zote ni za nini ikiwezekana kaka ziwashe uone kama kutakuwa na simu au sms zozote zitakazokusaidia kupata habari zaidi.

Suala la hirizi ni gumu but akueleze (ikiwezekana akupeleke) alikozitoa na ni za nini. Ukishapata hizi information zote then UAMUZI UNAO WEWE MWENYEWE.
 
Kaka Eaka!

wakati naendelea kutafakari habari hii ya kusikitisha naomba nikupe POLE na kumshukuru Mungu kuwa hakukuacha kiumbe wake angamie!

Nikusaidie kukuambia kuwa USIOGOPE wala hili lisikuumize zaidi tena! Mungu unayemwamini AMEKUSHINDIA na ndio maana upo hapa kutushuhudia; Sifa utukufu tunamrudishia yeye!

Mtoto ndio ananiuma sana kwa kuwa hili linaonyesha dhahili kumchanganya na kwa kweli hapo ndio wote mlipokosea; kwa yeye kumshirikisha na wewew kumwuliza; mmefanya achoose royalty! Hii ni mbaya! Tena ni mbaya sana!

Tafuta haraka sana sehemu mtoto akake huko mbali nayi kwa muda si chini ya miezi sita! na ikiwezeka akakae na mtu ambaye atakuwa rafiki yake na kuanzia sasa zaidi ya kumsalimia usimwulize tena wala kumsimulia habari za mama yake! Huwezi jua ni kiasi gani ameumia na kwakuwa hajui acope vipi inaweza kumpa kilema cha akili kabisa; hapa ndio pa kuangalia weye umeshaumia inatosha haipaswi kumuumiza mwanenu!

Nitakuja baadae na ushari zaidi!

Endelea kumshukuru mungu kwa yote
 
Pole sana , Kwakweli inaumiza moyo. Bwana akutie nguvu.Katika hali kama hii usifanye mambo kwa pupa. Tulia , tuliza akili halafu tafakari zaidi, angalia pande zote za shilingi. Kama unaweza kuishi bila yeye? na watoto je? Na kama unaweza kuendelea kuishi naye nini hatima yako? Maana katika hali kama hii huyo mwanamke anaweza akakutoa roho ili aendelee kufaidi maisha. Lakini pia jaribu kuangalia kitu kimoja , je watoto wote ni wenu? Wako? maana hata huyo mtoto mdogo anaweza kuwa wa huyo jamaa ndio maana anaona sawa kumleta nyumbani. Tafakari na omba mungu akuonyeshe njia iliyo sahihi na salama Kwako.
 
mchumba wake wa zamani.....,? mkuu, run DNA test kwa watoto wako. ulifanya haraka sana kumwanzishia biashara. Sielewi ni kabila gani but be careful, if possible confiscate business and car
 
Pole sana mkuu. Mkeo sio mwaminifu jaribu kujisahaulisha utazoea. Mwanamke anapofikia hatua hiyo inauma sana.
 
pole sana.
wakati mwingine kuna watu humu
huwa wanashauri tusioe na tunawaona machizi....
they could be right.....
ulaya katika kila vichaa wanne wanaume,mmoja source ni mapenzi....

ushauri wangu mpe talaka yake haraka sana.........
jizuie hasira,kubali kushindwa
na sometime kushindwa sio ubwege,
u can be a winner in everything in life.

The Boss, kuacha kuoa sio solution. Imagine kila mwanaume aache kuoa itakuwaje? we need each other katika haya maisha, ndo maana Mungu akaona ni muhimu kuoana. Cha msingi tu ni Kumwomba Mungu wakati unafanya maamuzi ya kutafuta mwenza, na kuendelea kumwomba siku zote katika maisha yenu. Siwezi kusema unahitaji kuwa mwangalifu maana unaweza kuwa mwangalifu wakati wa kuchagua halafu mtu akabadilika akiwa ndani ya nyumba.
Usiogope kuoa The Boss (kama bado hujaoa), angalia mifano ya ndoa unazozizimikia ndo zikupe motivation. Ndoa ni nzuri sana kama ukipata mwenza ambaye mnaelewana.
 
Pole sana Mangi,unapaswa kumshukuru mungu kwa kukulinda muda wote huo,pia napenda kuwapongeza wana jf wote kwani wote waliochangia wameonesha wazi hisia zao jinsi walivyoguswa na yaliyokufika na wamejaribu kukusaidia kimawazo.Hapa mimi kweli nimefarijika na nieona kuwa hii ni sehemu ya uhakika ya kuwasaidia watu walio katika matatizo.IDUMU JF.Mungu ibariki JF.
 
Ndugu yangu pole sana kwa yaliyokukuta zaidi zidisha maombi kwani kama ni MUNGU ndiye aliyekupa atakuonyesha njia sahihi ya kukabiliana nahilo tatizo. Ushauri wa mwanadamu unaweza kuangalia upande mmoja lakini ukiomba kwa Mungu atakupa ulio bora na wa busara.
 
Ndugu wana JF, Wapendwa wangu
Najisikia faraja kwa ushauri, nasaha na pole zenu. Nilikimbilia hapa nikiwa najua kuwa nitapata faraja ya moyo.
Hadi sasa sijaamua lolote ingawa baadhi ya rafiki na wasaidizi wangu walinishauri niondoke kwenye makazi yangu ya kawaida na nitafute mahali nipumzike kwa kipindi. Niliona ni ushauri wa maana kwa kiasi. Nimeondoka mimi na mwanangu na kwa sasa nipo mbali kidogo na nyumbani kwangu Moshi. Ninakuhakikishieni ushauri, na nasaha zote mlizonipa nitazifanyia kazi kwa uangalifu mkubwa bila papara yoyote na mwisho wa siku nina hakika kuwa nitapata suluhu. Ndugu zangu siku hiyo ikifika nitawajulisha nini na ni kwa nini nimefikia uamuzi huo nitakaofikia. Si rahisi sana kutaja wote kwa majina ila nasema asanteni sana na Mungu awabariki sana.
Kwa kusema hivi sio kwamba ninfunga hii mada la hasha bali tuendelee kushirikishana yote yanayotuhusu pamoja.
Mungu awe nasi sote.
 
Just have peace of mind, kuwa tayari kwa lolote, amini kuwa Mungu anakupenda. Kwa mawazo yangu huyo sio wa kurudi na kuishi naye, hafai kabisa. Toa taarifa polisi na kwa wandugu zake. Imarisha ulinzi wako na watoto wako. Mali zote ulizovuna jaribu kuziteketeza kwa faida ya watoto wako, mtenge kabisa. Hiyo ndio kambi ya kunyea mazima. Subiri, utampata tu anayekufaa. Mkaribishe Mungu afanye kazi kwako, atakunusuru zaidi na atakulinda.
 
Eeka Mangi,
I am trully sorry for your awful situation. As some said hapo juu God loves you and that is why HE revealed all this to you.
What I can say Brother is that nenda kaombewe, all those hirizis and what not are not good. If you are christian tafuta pastor to pray over you so that the shackles of darkness maybe broken. They are a sign of the times, though. People do not want to work hard, they want easy, example ni kama huyo "uncle", collecting money from your wife and driving her car. Some one once said that it is the new Job description, a kept man. As for your wife, I feel sorry for her...She got greedy too!! she wanted to have a cake and eat it. So far in life no one has managed to do this, have the cake and eat it. They are always found out.
Usife moyo, let God direct your footsteps.
 
Back
Top Bottom