Ndugu zangu wana jukwaa,ni matumaini yangu kuwa ni wazima na mnaendelea vyema na mapumziko ya mwishoni mwa wiki.
Ndugu zangu mimi ni mwalimu katika moja ya wilaya katika mkoa wa Rukwa.
Siku ya Mei mosi 2016, tulisikiliza hotuba ya Mheshimiwa Rais Magufuli hasa aliposema vyama vya wafanyakazi visilazimishe wafanyakazi kuwa wanachama wake viwaache wafanyakazi wachague vyama wanavyovitaka.
Kweli kabisa hotuba hii ilituelimisha sana, tukakiangalia chama chetu cha CWT na kuona mapungufu ambayo sitaki kuyazungumzia leo. Ndipo tukaanza mchakato wa kujiondoa CWT. Mungu bariki tukasikia kuwa Kigoma kuna chama kipya cha walimu kimeanzishwa na kimepata usajili tarehe 24/06/2015 na kupewa namba ya makato.
Tukafuatikilia na kukuta ni kweli kuna chama hicho kinaitwa Chama cha Kulinda na Ketetea Haki za Walimu Tanzania (CHAKUHAWATA). Hawa ndugu walitutembelea na tukajiunga.
Sasa tunaambiwa tutakatwa na vyama vyote viwili. Tusaidieni sheria inasemaje, sababu CWT ni wakala.