Nisaidieni GPS kwenye simu ya samsung S5830i

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Mar 28, 2011
1,002
274
Wakuu habarini za weekend natumai mu wazima.Niko hapa kuomba msaada wa jinsi ya kutumia gps kwenye hii simu yangu.
 
Wakuu habarini za weekend natumai mu wazima.Niko hapa kuomba msaada wa jinsi ya kutumia gps kwenye hii simu yangu.

Gps ni technology inayowezesha watu kukulocate sehemu ulipo

Gps unayo italocate sehemu ulipo then what?

Kwakweli gps ambazo tunazo kwenye simu ni kama function less au for funny ila kama utalipia ni kitu kimoja muhimu sana.

Kwa nokia kuna gps ya kulipia kuanzia dola 6 hadi 19 kwa mwaka ambayo itakulocate popote ulipo na kuku integrate na ovi maps.

Hii itafanya kazi hivi mimi nina huduma ya gps na wewe unayo nakuad katika gps yangu na wewe unani add katika gps yako kupitia map tutaweza kuonana

Mfano unatoka posta unaenda magomeni kwenye map yangu ntaona kidoti kinamove from posta to magomeni

Hii itakusaidia hata simu ikiibiwa kuweza kumuona mwizi kila akienda.

Kwa black berry niliona map zao zina gps na ni bure, kwa nokia tunalipia sjajua kwa samsung ila kwa sababu android ina google map na wana maslahi i hope itakuepo cheap au free

Labda kama yupo mwengine ana ujuz zaidi atakusaidia
 
Hiyo simu ni android, kuwasha GPS nenda settings, location and security, tick Use GPS satellites, hapo utakuwa umewasha GPS, pia unaweza kutick Use Wireless Networks, hii inatafuta location kwa kutumia minara na Wifi zilizokuzunguka.

Sasa GPS yako iko on unaweza kutumia Google Maps/places/latitude au program zozote zinazohitaji location, kama unataka raw gps values nenda Google Play (market) search GPS utakuwa maprogram kibao.
 
Wakuu habarini za weekend natumai mu wazima.Niko hapa kuomba msaada wa jinsi ya kutumia gps kwenye hii simu yangu.

Mkuu simu hiyo inatumia OS ya Android na kama ni hivyo basi inabidi ukiwa kwenye internet ukitumia Google kama search engine uende kwenye Market portal na uingize (download) application iitwayo Navigation.

Kwa kuwa Application ya Maps tayari ipo na ikiwa inategemea google search engine basi unapohitaji kutumia GPS inabidi kwanza kwenda kwenye internet na baada ya hapo google maps za hapo ulipo zita-integraten na Navigation na huenda ukafanikwa kupata mahali unapokusudia.

Utaratibu ni kama ufuatavyo.

Nenda kwenye settings:

Tiki kwenye Wifi ili iwe available

Pia tiki kwenye internet ya mtandao unaotumia (mobile internet) na awe operator wako.

Ukimaliza funga hiyo page na pale juu kwenye main page yako utaona lama ya H kwamba upo kwenye internet.

Then:

Kama unayo Application ya Navigation au GPS au Maps basi click na utaona inaanza kutafuta location.

Jaza anuani au jina la mahala unapokusudia kwenda na iweke simu yako kwenye kikalio mbele ya dirisha au kwenye hook yake uliyoigandamiza kwenye kioo kwa ndani ya dirisha la mbele.

Kaa tayari kuelekezwa.

Samahani kama kuna mahala ntakuwa nimesahau maana naingia kupiga kinywaji kidogo.
 
Back
Top Bottom