Nisaidieni akili za huyu jirani

Nisaidieni akili za huyu jirani

mamkuu5

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2014
Posts
1,139
Reaction score
721
Wadau heshima zenu,

Mwenzenu naishi kwenye nyumba za kota za watumishi wa uma some where hapaa Dar es salaam tukiwa ndo tumehamia tu miaka miwili iliopita tulikaribishwa na jirani mmoja matata yeye na mwanamke wake huyu jirani mwanaume nilisoma nae hivyo tukafurahiana sana huyu mwanamke alikua akija kulala pale mara chache alikua ni mwanachuo ila ndio mke mtarajiwa.

Mume wangu alikua masomoni hivyo hawakumfahamu, tulizoeana sana kiasi cha kuitana anti, siku zinavyoenda nikagundua stori za uyo mke za kimalaya sana, nilijikaza kwa uvumilivu nisiharibu ujirani wetu baada ya muda mume wangu alirudi hivyo tukaanza mipango ya kutafuta kiwanja atlist tuanze kujenga.

Nilifanya hilo kwa usiri mkubwa ila cha kushangaza alijua vitu vyetu vingi hata tulivyoongea kwa siri nilimhisi mumewangu labda vile anavyoongea na mwanaume mwenzie labda anamshirikisha basi nilimuonya mume wangu ila akashangaa akiniambia labda mimi ndio nimesema.

Baada ya tukio hilo jirani me& ke walianza kupunguza ukaribu kwetu, sikujiskia vibaya ila tulijiuliza sana.baada ya muda wakanunua gari ndo kabisaaa full kutupotezea pia hatukuuliza ila kushangaza jirani hasalimii anawezakusafiri familia ikapatashida tukawasaidia ila akirudi hatambui hata hashukuru kageuza wajibu wetu kumsaidia mkewe na ndugu waliopo.

Juzi wamevamiwa sijui mume kawazulumu nini wakaja tulisaidia sana hadi kupeleka hospitali walioumia ila tulipojaribu kuulizia wanavyoendelea hawakutujibu kwenda hospitali tunaambiwa hawapo. Kweli nimefundwa kuishi na watu ila hili nafikiri tuachane nao au ntakua nakosea?

Nisaidieni mawazo tafadhali kama hunawazo la kujenga tafadhari kaa kimya
 
unapotoa usihesabu ww potezea kwasababu anayeweza kukulipa fadhira zako ni mungu tu ucjari mungu yuko nawe katika majaribu yk yote ipo siku watajua humuhimu wako
 
hao ni kuwakimbia mapema tu kabla hawajakuletea matatizo..watakuja kukuundia zengwe mwenyewe ukashangaa
 
fanya jambo kama msaada ucngoje shukrani,laiti kama YESU KRISTO angesubiri shukran zetu,basi mengi yacngetokea ata tujifunze....ucngoje shukran
 
Achana na nao,usipoteze mda wako kufikiria watu.
 
Fanya yale yanayokuhusu mengne waachie wanaoweza kuyafanya...
Maisha ya mtu mwingne sidhan kama yanakuhusu...

Ukijifanya unahuruma ipo siku itakuponza...

.............. Ipyana igogi.....................
Hilo neno la chini waite Apologise lady au miss strong watakwambia maana yake
 
Last edited by a moderator:
Unataka kulazimisha ujirani mwema ili iweje? Usingiziwe unamtongoza mumewe au mumeo asingiziwe anamtongoza huyo shangingi? Mind your own business please. Chezeni nao mbali, waswahili wanasema hayawahusu.
 
Kwani lazima uwe nao karibu????
Halafu ujirani wa kufuatanafuatana ndio unaoletaga shida .....
 
Ungechelewa kidogo tu ningeiandika mimi hii post......
 
Jirani wa kota ishi nae kimagutu...hawana maana
 
Wadau heshima zenu,mwenzenu naishi kwenye nyumba za kota za watumishi wa uma some where hapaa dar es salaam tukiwa ndo tumehamia tu miaka miwili iliopita tulikaribishwa na jirani mmoja matata yeye na mwanamke wake huyu jirani mwanaume nilisoma nae hivyo tukafurahiana sana huyu mwanamke alikua akija kulala pale mara chache alikua ni mwanachuo ila ndio mke mtarajiwa, mumewangu alikua masomoni hivyo hawakumfahamu, tulizoeana sana kiasi cha kuitana anti, siku zinavyoenda nikagundua stori za uyo mke za kimalaya sana.nilijikaza kwa uvumilivu nisiharibu ujirani wetu baada ya muda mume wangu alirudi hivyo tukaanza mipango ya kutafuta kiwanja atlist tuanze kujenga.nilifanya hilo kwa usiri mkubwa ila cha kushangaza alijua vitu vyetu vingi hata tulivyoongea kwa siri nilimhisi mumewangu labda vile anavyoongea na mwanaume mwenzie labda anamshirikisha basi nilimuonya mume wangu ila akashangaa akiniambia labda mimi ndio nimesema ,baada ya tukio hilo jirani me& ke walianza kupunguza ukaribu kwetu, sikujiskia vibaya ila tulijiuliza sana.baada ya muda wakanunua gari ndo kabisaaa full kutupotezea pia hatukuuliza ila kushangaza jirani hasalimii anawezakusafiri familia ikapatashida tukawasaidia ila akirudi hatambui hata hashukuru kageuza wajibu wetu kumsaidia mkewe na ndugu waliopo.juzi wamevamiwa sijui mume kawazulumu nini wakaja tulisaidia sana hadi kupeleka hospitali walioumia ila tulipojaribu kuulizia wanavyoendelea hawakutujibu kwenda hospitali tunaambiwa hawapo.kweli nimefundwa kuishi na watu ila hili nafikiri tuachane nao au ntakua nakosea? nisaidieni mawazo tafadhari.kama hunawazo la kujenga tafadhari kaakimya

Uandishi gani huu. Hakuna nukta, hakuba paragraph. Sentensi hazieleweki. Ndo tumefikia hapa.
 
Kitu kikubwa kinachofanya maisha tuyaone magumu ni kwa sababu tunasumbuliwa au kushughulishwa sana na mambo ya wengine huku tukijisahau kuwa furaha za maisha yetu zipo ndani yetu.....wapendwa wetu waliokaribu nasi ndio wanaotupa tabasamu katika nyuso zetu kwa upendo wao kwetu....si vyema kujihangaisha na vitu vilivyo nje ya uwezo wetu...kwani vinaweza kutupa msongo usio na ukomo huku tusijue la kufanya.....jambo la msingi ni kujaribu kwa kila hali kutafuta furaha maishani mwetu.....kwani furaha ndio injini ya afya njema....
 
Back
Top Bottom