Nisaidieni mbinu za kupambana na huyu jirani 'mwizi wa umeme'

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,600
Hii nyumba ninayoishi tupo wapangaji watatu kwenye compound moja. Nimehamia hapo huu ni mwezi wa pili unaenda kuisha.

Ndani ya hizi wiki chache, nimeona mabadiliko makubwa ya matumizi ya umeme. Mwanzoni ilikuwa natumia wastani wa unit 2.4 kwa siku, ila kwa sasa imepanda mpaka 3.6 kwa siku.

Nimeona sio kawaida, mpaka nimehisi kwamba inawezekana kuna jirani ananipiga umeme wangu, na ushahidi nilionao ni kwamba, mahali ilipo mita yangu ipo pamoja na jirani yangu mmoja, ila sasa maajabu nashangaa hii siku ya pili nimechunguza, hiyo mita ni kama unit za umeme za jana ndo zipo leo. Nikimaanisha kwamba, ni kama vile huyu jirani atakuwa anatumie umeme kwenye source ingine ambayo possibly ameconnect umeme wangu.

Nnachokifikiria kwa haraka haraka ni kumleta fundi wiring ili akague system nzima ya umeme wangu.

Naombeni mnipe mbinu zaidi wakuu, nimekereka sana kuligundua hili, kitendo cha mtu kuniibia huwa nakichukulia kama kuniona sina akili na kunitusi.

Nahisi kama nimuadabishe bila kumuambia chochote. Haiwezekani mtu ufikiria kupambana na maisha halafu ufikirie tena kupambana na majirani wezi.

Mbinu safi na chafu nazipokea ahsante
 
Yaani kweli baba nanii unapanga kunikamatisha
emoji7.png
emoji7.png
 
Fanya options hizi:

(1) Subiria umeme uishe 0 units. Hafu ufuatilie zake uone zinaisha au zipo constant. Pia uone kwake kutakua na umeme au kiza.

(2) Muite fundi wiring na ukikuta kuna wizi mshitaki.
Hiyo namba moja ni kama nime prove ni kweli.

Nilikuwa nataka hii kesi kama fundi wiring akigundua, niimalize kimya kimya.

Asante
 
Nnachokifikiria kwa haraka haraka ni kumleta fundi wiring ili akague system nzima ya umeme wangu.

Unamleta fundi wiring aje akague system ya umeme kwa ruhusa ya nani, hiyo nyumba ni yakwako? Unajua ni "system" gani mwenye nyumba ametegesha humo darini za kuhakikisha wapangaji hamuondoki..?😀😀😀 Naona umechoka kuishi kwenye hiyo nyumba. Na kwa taarifa yako kodi hairudishwi...
 
Unamleta fundi wiring aje akague system ya umeme kwa ruhusa ya nani, hiyo nyumba ni yakwako? Unajua ni "system" gani mwenye nyumba ametegesha humo darini za kuhakikisha wapangaji hamuondoki..?😀😀😀 Naona umechoka kuishi kwenye hiyo nyumba. Na kwa taarifa yako kodi hairudishwi...
Kwahiyo jirani ndo umekuja kunitisha na huku ili nisikudhibiti?

Sasa kwa taarifa yako, lazima nilete fundi akague. Kama ulikuwa huna bajeti ya umeme anza mapema kuitafuta.

Naenda kukata mirija ya umeme wa kitonga
 
Hivi, waya wa upande wako unaotoka kwenye mita kuingia kwenye circuit breaker yako unaweza kuuona?
kwenye mita waya nauona ambao unaenda kwenye circuit breaker.. ila sasa ndo sijui kabda kuna diversion imefanyika mahali ambapo mpaka sasa bado sijajua haswa
 
Back
Top Bottom