Nisaidie Kijana Mwenzako

Nisaidie Kijana Mwenzako

Raelish

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2013
Posts
489
Reaction score
162
Habarini hapa.

Namshukuru Mungu naendelea kupumua japo maisha yangu ni kama hayaendi hivi. Kifupi mimi nimekulia katika mazingira magumu sana na nimepata elimu yangu kwa tabu nyingi sana, lakin namshukuru Mungu nimefanikiwa kupata japo elimu hii ndogo. Elimu yangu ni kidato cha sita tu na nilisoma masomo ya sayansi yaani CBG (chemistry,biology & geography) nina uwezo mkubwa na nina kipaji cha kufundisha pia ni rahisi sana kuelewa nikielekezwa chochote cha kufanya.

Waungwana mimi ndo nategemewa na familia yangu lakini nikijiangalia nilivyo ni kama nimekabidhiwa jezi mchezo sijaujua. Maisha yangu ni magumu mimi ni mmoja kati ya wale vijana tunaukula mlo mmoja kwa siku na hatujui kesho yetu. Natamani nianze biashara sina mtaji najianamia nafuta machozi lakini siachi kumshukuru Mungu.

Leo nikapata wazo niwaombe waungwana kama kuna mtu ana kazi yoyote ambayo anaweza kunipa nikafanya ili nipate ridhiki naomba kusaidiwa. kama umeguswa kunichangia chochote nipate mtaji karibu.

Napatikana hapa 0782168784 au 0763223724.
 
Wewe na ndugu zako jaribuni kumtegemea Mungu,mwanadamu hatokusaidia.

Pili kama huna mapungufu yoyote ya mwili,una fursa kubwa sana ya kupiga hatua.usichague kazi ya kupatia mtaji,hata karanga uza.
 
Nakushauri nenda kafanye hata kazi ya ulinzi kwenye makampuni Makunbwa kama Kk, G4s Na Mengine atleast upate fursa ya kupata japo hela ya kujikimu na kugawana na ndugu zako japo kidogo mishahara yao inaweza kukupa uahueni wa maisha kwani wanalipwa kuanzia laki mbili na semanini mpaka laki tatu. Wakati ukiwa huko jitaidi kutafuta ajira zingine ukiwa na pakuegemea ukitegemea mtaji upewe na mtu hiyo sahau mtaji ni nguvu zako kaka na kule kuna form six kibao mpaka wana vyuo ni hayo tu.
 
ahsante sana ndugu yangu, ofisi za hizo kampuni naweza kuzipata wapi? ahsante kwa kunijali.
 
Wewe na ndugu zako jaribuni kumtegemea Mungu,mwanadamu hatokusaidia.

Pili kama huna mapungufu yoyote ya mwili,una fursa kubwa sana ya kupiga hatua.usichague kazi ya kupatia mtaji,hata karanga uza.

mimi sichagui kazi lakini hata kupata hizo kazi za kutokuchagua ni ngumu, kama ipo popote mkuu mi nafanya sichagui
 
Umemaliza form six mwaka gani na ulifaulu au coz cha msingi ilikuwa kuwaza kujiendeleza kimasomo zaidi coz form six without proffesional its nothing naomba utupe hilo jibu ndo tutajua cha kukusaidia zaidi
 
habarin hapa. namshukuru Mungu naendelea kupumua japo maisha yangu ni kama hayaendi hivi. kifupi mimi nimekulia katika mazingira magumu sana na nimepata elimu yangu kwa tabu nyingi sana,lakin namshukuru Mungu nimefanikiwa kupata japo elimu hii ndogo. Elimu yangu ni kidato cha sita tu na nilisoma masomo ya sayansi yaani CBG (chemistry,biology & geography) nina uwezo mkubwa na nina kipaji cha kufundisha pia ni rahisi sana kuelewa nikielekezwa chochote cha kufanya. Waungwana mimi ndo nategemewa na familia yangu lakini nikijiangalia nilivyo ni kama nimekabidhiwa jezi mchezo sijaujua. Maisha yangu ni magumu mimi ni mmoja kati ya wale vijana tunaukula mlo mmoja kwa siku na hatujui kesho yetu. Natamani nianze biashara sina mtaji najianamia nafuta machozi lakini siachi kumshukuru Mungu. Leo nikapata wazo niwaombe waungwana kama kuna mtu ana kazi yoyote ambayo anaweza kunipa nikafanya ili nipate ridhiki naomba kusaidiwa. kama umeguswa kunichangia chochote nipate mtaji karibu. Napatikana hapa 0782168784 au 0763223724.

Vipi mkuu, kwa nini haukuendelea na masomo ili kupata fani? Na sasa unawaza biashara gani, maana usitegemee watu wakurushie tu pesa bile kujua wewe unawaza nini?!! Pia uko wapi, maana masomo uliyosoma hauwezi kukosa shule ya kufundisha tempo wakakupa hata laki mbili!
 
Umemaliza form six mwaka gani na ulifaulu au coz cha msingi ilikuwa kuwaza kujiendeleza kimasomo zaidi coz form six without proffesional its nothing naomba utupe hilo jibu ndo tutajua cha kukusaidia zaidi

nimemaliza kidato cha 6 mwaka 2011 nilijitahd sana kutafuta namna ya kuendelea na masomo imeshindikana. nina div.iv point 18
 
Vipi mkuu, kwa nini haukuendelea na masomo ili kupata fani? Na sasa unawaza biashara gani, maana usitegemee watu wakurushie tu pesa bile kujua wewe unawaza nini?!! Pia uko wapi, maana masomo uliyosoma hauwezi kukosa shule ya kufundisha tempo wakakupa hata laki mbili!

mkuu nimewaza sana kuhusu kuendelea na masomo lakin tatizo ni pesa, nipo dar mbagala, biashara ninayoiwaza ni kununua bidhaa kutoka shamba kama matunda,mihogo,mkaa n.k kuja kuuza mjini hapa.
 
ahsante sana ndugu yangu, ofisi za hizo kampuni naweza kuzipata wapi? ahsante kwa kunijali.

Ofisi za G4s Ziko Moroko airtel ukishuka uliza Campuni ya Erolink ilipo ukifika hapo zimetazamana tu. Au K.K Panda magari ya Kawe Shuka mikocheni kwa Mwinyi Uliza mtu yeyote atakuelekeza ni karibu tu..... Jitaidi kujikwamua muwindaji hachagui poli ukilala tu nyumbani utapoteza mwelekeo kafanye kazi hata mika miwili PPF utapata hata Milioni Moja Achana nao anza biashara zako utakuwa umepata mtaji. Kumbuka siku zote mhangaikaji ndo anaepata.
 
thanks., daah we ni ndugu yangu mkuu, ahsante
 
nimemaliza kidato cha 6 mwaka 2011 nilijitahd sana kutafuta namna ya kuendelea na masomo imeshindikana. nina div.iv point 18
nenda wizara ya afya,kilimo au mifugo wana vyuo vyao wanahitaji sana vijana wakusomea kilimo na afya!tena kwa matokeo yako unaanzia diploma
pia wizara ya elimu wanachukua watu wasayansi waliomaliza kuanzia 2002 ili wakasome diploma ya ualimu!kazi ni kwako mkuu fursa zipo nyingi sana
 
Raelish hebu fuatilia ushauri huu kwanza kabla haujajifunga kwenye kazi za kinyonyaji za ulinzi. Pia usicheze mbali na mitandao kuanzia mwezi wa nne vyuo vingi vinatangaza nafasi za asomo, diploma hata ya ualimu si ghali vyuo vya serikali, tena wewe wa sayansi mkuu. usikate tamaa wanaume wote tunapitia majaribu.
 
Last edited by a moderator:

Sawa mkuu, ngoja nianze hapo kwanza. umenipa matumaini mapya
 
Raelish hebu fuatilia ushauri huu kwanza kabla haujajifunga kwenye kazi za kinyonyaji za ulinzi. Pia usicheze mbali na mitandao kuanzia mwezi wa nne vyuo vingi vinatangaza nafasi za asomo, diploma hata ya ualimu si ghali vyuo vya serikali, tena wewe wa sayansi mkuu. usikate tamaa wanaume wote tunapitia majaribu.

'usikate tamaa wanaume wote tunapitia majaribu' hii kauli imenigusa ndani sana, Mungu nikumbuke na unisaidie mimi uliyeniumba kwa mikono yako.. amina
 
Last edited by a moderator:
pia kama kuna fursa yoyote itakayotokea usisahau kukumbuka kuwa yupo mtu mwenye uhitaji mkubwa., namba zangu hizo hapo. chochote kile mi nafanya. na ushauri wote nitaufanyia kazi mmoja baada ya mwingine
 
Back
Top Bottom