Nisadieni wakuu; Tumetofautiana imani na wazazi hawataki hata mmoja wetu abadili dini

kisikinumber

Member
Jul 24, 2014
94
68
Habari zenu wana JF, ni matumaini yangu kuwa mko pouwa!!
Lengo la kuandika huu uzi ni kutokana kushindwa kufikia maamuzi sahihi .
Kuna binti nlikutana nae mwaka mmoja umepita hadi sasa ilikuwa ni mwezi wa 6/6/2016, Muda kidogo nlianzisha uhusiano nae!

Kiukweli ninampenda na hitaji langu ikibidi awe mke wangu. Tatizo ni dini yeye ni muislam na mimi ni mkristo. Swala la imani nadhani mnalifaham jinsi lilivyo kifupi wazazi wake waliishakataa hilo swala la yeye kutaka kubadili dini na upande wangu pia ni hivyo

Kiukweli nampenda na yeye ananipenda ila hicho ndo kikwazoo
Nipo njia panda hadi sasa
[HASHTAG]#mawazo[/HASHTAG] yenu wakuu#
 
Mwanamke hana dini
Kama ungekuwa Mkristo kweli usingekuja na swali hilo hapa labda ungeleta ushuhuda wa kumpeleka kondoo zizini mwa Bwana lakini sio kwa ahadi ya ndoa bali kwa injiili na elimu kwamba anaabudu miungu ya Waarabu
 
nilishawahi pata tatizo kama lako, ukweli kwa mwanaume kubadili dini ni ngumu sana.

alinishauri nimpe mimba kama kigezo cha kufanya wazazi walainike nikawaza akijifungua kwa matatizo ama yeye au mtoto kufariki itakuwaje? ntampeleka wapi

nikaachana nae, kama wazazi wamegoma mkuu nakushauri mpotezee. siku likitokea tatizo utakosa kuungwa mkono na upande wa ukweni
 
Shukhrani mkuu pia kuna jamaa kaniambia nimpe mimba ndo itakuwa rahisi kwa wazazi wake kukubali
 
Nawaona ila ujue mke ni jambo lingine mkuu
Shukhrani
Ndio nafahamu, lakini je unataka kuniaminisha kuwa haiwezekani kupata mwingine mwenye vigezo tafauti na huyo? au unawaza kuanzisha mahusiano mapya...Kwa maana sasa suala la dini ndio kikwazo pande zote mbili
 
Shukhrani mkuu pia kuna jamaa kaniambia nimpe mimba ndo itakuwa rahisi kwa wazazi wake kukubali
shida yake ni pale atakapo jifungua kwa matatizo (hatuombei) yeye ama mtoto na wazazi wakakataa kukupa ushirikiano utakuwa na khali gani?

kuna wazazi wana msimamo utatia mimba wanamfukuza na hawataki kumjua kwa lolote

pia waweza mpa mimba akajifungua mtoto mlemavu (siombei ivo ) ukamkimbia. akapata mapigo mawili ya kukimbiwa na ww na kutengwa na waZazi

cha muhimu muache tu mkuu
 
Unampenda mtu kikwazo dini unajiuliza mara nyingi ya nini?

Badili dini tu haina kujiuliza maswali mengi.
Niamini mimi wewe hautakua wa mwisho.
 
Back
Top Bottom