Nipo tayari kwa mapambano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nipo tayari kwa mapambano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OTIS, Mar 28, 2012.

 1. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu watanzania wapenda maendeleo ya nchi yetu.
  Nawaombeni tuweke kando tofauti zetu za vyama nk na tuungane kwa pamoja na Mhe Waziri Mkuu Mstaafu ndugu Edward lowassa kupambana dhidi ya Umaskini,ujinga,maradhi na hasa ufisadi.
  Tukiungana kwa dhati tutafanikiwa.
  Niko pamoja nawe kwenye mapambano haya
  Hii si vita yake peke yake ila ni ya kila mzalendo alipendae taifa hili.
  OTIS
   
 2. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  You can't be serious!! Huyu ndiye aliyetufikisha watanzania kwenye umaskini huu! RICHMOND ilikuwa inachota million 152 kwa siku! tukimpa Urais si ndo atatuuza kabisa na kuwa watumwa!!!!
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Legwanani Only Fisadi Succeed(OFS)
   
 4. T

  Tanzaniaist Senior Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ONLY THE ILLUMINATI SUCCEED.! ILLUMINATI=FREEMASONS..,Jamani mzee wa watu alishasema enough is enough naona mshaanza kumuhusisha na mambo ya kipuuzi eti Illuminati wakati yy ni mtu wa mungu
   
 5. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kasema yupo tayari kwa mapambano
  Kwanini tusimuamini?
  OTIS
   
 6. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  OTIS ni mie
  Yeye utamkuta kanisani
  Tunasubiri ratiba ya mwaka mzima itoke
  Mapambano ndio yanaanza
  Mafisadi kaeni chonjo
  OTIS
   
 7. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watanzania kama kuna jambo tutajutia ni kumwamini na kumpa nchi huyu jamaa! tutarudi enzi zile za kuvaa katambuga!!
   
 8. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Huna imani kwamba mafisadi wote atawanyoosha?
  OTIS
   
 9. m

  mareche JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 475
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  makada wa magamba washalipwa na fisadi lowasa kuja kumnadi hapati kura yyangu kamwe
   
 10. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Msijali kuhus wa kumuunga mkono lowasa 2015, mi nipo tayari kunuunga mkono Lowasa 2015 but ikiwa kama CDM itamsimamisha mzito kabwela kugombea urais badili ya slaa.
  PAMOJA SANA MKUU.
   
 11. GIB

  GIB JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  OTIS wewe ndiye rich nini?
  huyu mtu nifisadi kila mtu analijua hilo. dhambi hiyo aliyoitenda imeingia hadi kwenye vina saba (DNA) za watanzania wote hivyo hata watoto wakiwa bado kwenye matumbo ya mamayo (placenta) wanajua kunafisaidi. linalo umiza vichwa vya watanzania wote. Natutaendelea kuridhishana (inherit) kizazi hadi kizazi mpaka kizazi cha tano cha watanzani wataendelea kujua ubaya wake.
  Ameingia kwenye historia ya Tanzania.
  Mungu Ibariki Tanzania mapambano yanaendelea, Mungu wahukumu mafisadi yote tena mchana peupe , amen amen.

   
 12. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Uzalendo ndio utuongoze mkuu

  Na kiboko ya mafisadi ni Lowassa
  OTIS
   
 13. GIB

  GIB JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  , Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Cahadema), amemvaa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, akimtaka kuacha kutumia matamanio yake ya kuwania urais mwaka 2015 kuwadanganya wananchi, kwa kuwaaminisha kuwa anaumizwa na tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana nchini. Akiwahutubia mamia ya wananchi katika mikutano ya kampeni inayoendelea katika Jimbo la Arumeru Mashariki jana, Mdee alisema kuwa Lowassa anataka kuwaghilibu Watanzania kuwa anaumizwa na tatizo la ukosefu wa ajira wakati akijua ni matokeo ya kushindwa kwa sera na mipango ya chama na serikali yake, ambayo yeye mwenyewe amekuwa sehemu ya uongozi wake kwa muda mrefu.
  Akiwa katika Kijiji cha Ndatu katika Kata ya Poli, Mdee aliwaambia wananchi kuwa kama Lowassa ana uchungu na vijana na nchi hii kwa ujumla, alipaswa kuwa ameonesha hilo kwa kutoa ushauri anaoutoa sasa wakati akiwa madarakani, na si wakati huu ambapo amekuwa akiandamwa na tuhuma za ufisadi hata ndani ya chama chake.
  Mdee aliongeza kuwa kama kweli Lowassa, ambaye alijiuzulu uwaziri mkuu Februari 2008 kwa kashfa ya ufisadi wa kampuni tata ya Richmond, hataki nchi ilipuke, basi akishauri chama na serikali yake kuziba mianya yote ya ufisadi na kuwachukulia hatua za kisheria watuhumiwa wote wa ufisadi nchini ambao wametumia nafasi zao kuwaibia Watanzania na kuifilisi nchi.
  Mbunge huyo alisema kuwa Lowassa anawadanganya wananchi akionesha kuwa ana uchungu na tatizo la ajira kwa vijana, bali ana matamanio ya urais, kwa kuwa alikuwa serikalini na ndani ya chama chake kwa muda wote huo, na wala tatizo la ukosefu wa ajira halikuanza leo wala halikuchipuka kama uyoga.
  "Hili limesababishwa na kushindwa kwa mfumo, sera na mipango ya chama kilichoko madarakani sasa lakini pia mafisadi wamesababisha vijana kukosa ajira, hivyo ufisadi ndio tishio kubwa kabisa kwa nchi kwa sasa.
  "Namwambia Lowassa kabla tatizo la ajira kwa vijana halijafikia kilele cha kulipua nchi, ufisadi unaofanywa na viongozi wa CCM na serikali utakuwa umeshailipua nchi hii, hivyo azungumzie ufisadi kwanza…tena asiende mbali, apekue tu nyaraka za CHADEMA aangalie tamko letu la Mwembeyanga mwaka 2007, ambapo tulitaja orodha ya aibu ya mafisadi na ufisadi ndipo apige kelele," alisema Mdee.


   
 14. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Jamani mtu alieshiriki kuiingiza nchi kwenye umasikini mkubwa na kuongezeka kwa maradhi tunahimizwa kushirikiana nae? jamani kama angekuwa ni mpambanaji kweli kwa nini alikubali kujiudhulu ilhali anaujua ukweli wote kuhusu Rich na Dowa?
  Angekuwa anapambana asinge subiri tume ya akina Mwakyembe imuumbue,leo hii wanajitokeza akani OTIS kutuhimiza kushirikiana nao.Dhambi ya kuifahamu inauma kuliko dhambi ya bahati mbaya SIWEZI KUMUUNGA MKONO EL.HAYO NI MAWAZO YAKO NA HAYA NI MAWAZO YANGU
   
 15. GIB

  GIB JF-Expert Member

  #15
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu kwa kutajwa katika kashfa ya mdadi wa umeme uliohusisha kampuni tata ya Richmond Development LLC, Edward Lowassa, amelipwa mamilioni ya fedha na wafanyabiashara wa Kisomali, Fikra Pevu imethibitisha.Uchunguzi wa muda mrefu wa Fikra Pevu umeonyesha kwamba Wasomali hao kupitia kampuni ya Integrated Properties Investment (T) Limited walimlipa Lowassa Sh milioni 450 kupitia kampuni yake ya Barare Limited. Malipo hayo yalielezwa kuwa ni deni ambalo Lowassa kupitia Barare alikua akiidai kampuni hiyo ya Integrated ambayo kwa Tanzania imekuwa ikijihusisha na uwekezaji katika majengo.
  Uchunguzi wa Fikra Pevu umethibitisha kwamba malipo hayo yalifanyika miezi michache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, na Lowassa na mkewe Regina Mumba Lowassa, walikubali malipo hayo kwa kupewa hisa 7,500 zikiwa na thamani ya Sh 60,000 kwa hisa moja.
  Uchunguzi wa muda mrefu wa Fikra Pevu umeonyesha kwamba Wasomali hao kupitia kampuni ya Integrated Properties Investment (T) Limited walimlipa Lowassa Sh milioni 450 kupitia kampuni yake ya Barare Limited. Malipo hayo yalielezwa kuwa ni deni ambalo Lowassa kupitia Barare alikua akiidai kampuni hiyo ya Integrated ambayo kwa Tanzania imekuwa ikijihusisha na uwekezaji katika majengo.[​IMG]

   
 16. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #16
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Eleza anavyopambana......anapambanaje!!
  Alisema yupo fit kupambana (afya) kwahiyo mapambano yake yanahitaji nguvu?
  kama ndivyo, basi akawaajiri jamaa wa WWE wrestling

   
 17. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #17
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  OTIS u cant be serious, huyu ni moja kati ya watu waliosababbisha umaskini miongoni mwa watanzania leo unasema tuungane naye kupambana na umaskini? How can we? Kumbuka suala la umeme linavyoifilisi nchi? ni vijana wangapi wanakosa ajira kutokana na tatizo la umeme? Naye ana mkono wake mrefu hapo kwenye umeme. Mwambie arudishe pesa zetu kwanza bana

   
 18. m

  mzizi dawa Senior Member

  #18
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sizani kama huyu mtu ana akili timamu kutuletea huu upuuzi apa.jitu akili zake zakufikiri zimeishia apo anatulea upumbavu apa.
   
 19. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #19
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mapambano dhidi ya nini, sikuelewi. Ufisadi au umaskini.
   
 20. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #20
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Angalia usichinje mbwa!maana hiyo njaa ilipokufikisha pabaya!usiliendekeze tumbo ndugu!uchafu mwenzetu kwako pilau.njaa!
   
Loading...