Nipo stendi narudi mjini Dar! Niliyoyaona kijijini yanatisha kwa kweli

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Kila uchao naamini uhalali wa ccm kuendelea kuitawala tz hii kwa mgongo wa K/nyanya unafika kikomo!

Hali ya maisha vijiji inatisha ndugu zangu na watu wameanza kuamka, sasa wanasema bila kutafuna manene kuwa ccm ijiandae kuwa chama cha upinzani na wanapendekeza kuwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani atakuwa Nape!

Kwakweli sijawahi kuona Wanyalu wakiwa na hasira na ccm kiasi kile! Wanadai maisha yamekuwa magumu kupita kiwango!

Utafiti nilio ufanya ktk vijiji sita vya kata yetu juu ya mahitaji muhimu ya binadamu yapo juu kuliko hapa dar.
Mafuta ya taa lita 2,700/
Sukari kg. 2,500/
Chumvi kipaketi 500/
Sabuni kipande (komoa)400/
Kibiriti 100/
Lita moja ya ULANZI 200/
Bia 2,000/
Soda 600/
Usafiri umbali wa km 12 wenyeji wanatembea kwa miguu mpaka stendi,kukodi gari 25,000/
Zahanati ipo kila ukienda uwe 5,000/ mkononi
Shule ya msingi ipo na imefaulisha 28 kt 88
Shule ya sekondari ipo bado ni mpya!

Maisha ya wakaazi ni ya wakulima na walevi waliochoka na maisha, kijana wa miaka 20 ukimuona utadhani ni mzee wa miaka 60!

Hali ya hewa ni baridi na ukungu la kufa mtu!

Hali ya chakula si nzuri watahitaji msaada mda si mrefu!

Nimeamua kurejea mjini ili kupambana vizuri na serikali dharimu ya ccm na Kikwete wao baada ya kuwahamasisha na kutoa elimu ya uraia kwa vijana wote ktk kata yetu! Nimewafahamisha kuwa vyama vingi si uhalifu na nikawaambia vijana kwa wazee ccm haiongozwi na Nyerere kama wanavyo dhani,ila inaongozwa na muhuni fulani aliyempigu Vasco Dagama!

Nashukuru wamenielewa wakafanya tambiko la nguvu na kunituma nije town kulikomboa taifa!

Nimewaahidi kila mwaka nitakwenda kuwaelimisha na kuuweka wazi uozo wa ccm mpaka 2015!
 
Your trip and even feedback have no meaning coz Tanzanians are strange people who would die na tai shingoni waiting for another round of vitenge na kofia from CCM just before electionMie nahamia zambia kabisaaaaaaaaa
Mtanzania usiiche tz mikononi mwa mabakauchumi, hima tukomae kuikomboa sisi wenyewe!
 
Hizo ni habari njema kwangu, Sasa mikakati iendelee siyo kuishia hapa jamvini.
 
Umoja ni nguvu.

Je,ni wakulima au wafugaji/wavuvi?..mazao na wanyama wanawatumiaje?
Inaonyesha elimu si tatizo,je quality ya hiyo elimu ikoje?...madarasa,madawati,ratio ya walimu/wanafunzi.
Zahanati kama ipo,umewashauri nini kuhusu bima ya afya au mfuko wa kijiji wa afya?
Kuhusu ulanzi,bia na soda...hivo sioni kama vya kulalamikia sana kwani havina umuhimu.
Kuhusu chakula,nawapa pole sana ila nguvu zaidi hutokana na ushirika/ushirikiano wa wananchi.Kupunguza makali ya bei za sukari,chumvi na sabuni,mtaji wa milioni mbili unaweza ukaanzisha duka au ghala lenye 200kg za sukari(500,000).lita 100 za mafuta ya taa(270,000),miche 100 ya sabuni komoa(200,000),usafirishaji na gharama nyingine 1,000,000/-.
Vitu hivi vinunuliwe moja kwa moja kutoka kwa wauzaji wa jumla ili kumkata middleman,na kuuziwa kwa wanakijiji kwa faida robo ya mfanyabiashara.Hii itapunguza ukali wa bei kidogo.
Najua siasa ni muhimu lakini inakuwaga maridadi sana ukiwaonyesha jinsi ya kupambana na wenye nguvu,ni kwa wanyonge kujiunga pamoja kama ndugu wa damu na ku launch a counter attack through cooperation.
Next time punguza hotuba,huwa hazishibishi.
 
Your trip and even feedback have no meaning coz Tanzanians are strange people who would die na tai shingoni waiting for another round of vitenge na kofia from CCM just before election

Mie nahamia zambia kabisaaaaaaaaa
Do not underestimate the people of Tanzania.
 
Your trip and even feedback have no meaning coz Tanzanians are strange people who would die na tai shingoni waiting for another round of vitenge na kofia from CCM just before electionMie nahamia zambia kabisaaaaaaaaa
Wewe ndo umeongea PUMBA humu nyie ndio msiopenda maendeleo kilichokufanya uandike uchafu wako humu ni nini kama ungetaka kujibu si ujibu hoja nini kumsema mwandishiMtu katoa maoni au hujaona alichoandika alichoona? Fikiria kabla ya kupurukuka kujibu PUMBA
 
Mtanzania usiiche tz mikononi mwa mabakauchumi, hima tukomae kuikomboa sisi wenyewe!
niemshajaribu hadi nikafikia kupewa warning na "watumishi wa serikali" na nimegundua watanzania wengi ni wanafiki, unacheka nao kesho wanaenda kusema yule jamaa anataka kuharibu amani

wacha nikajaribu kwingine, hata yesu alizaliwa kwingine akafia kwingine na mtume muhammad (SAW) vivyohivyo.... so i have taken a gloabl approach to Tanzania solutions

I AM BROKEN HEARTED HADI LEO SI CHADEMA, SI NANI ALIYEHIMIZA WANANCHI KUIAMBIA SERIKALI KWA VITENDO KWAMBA INAUMA SANA HADI KWENYE MAKALIO HALI YA MAISHA

SABABU TU YA VIKAO VYA BUNGE VYENYE JENERETA, VIYOYOZI, KUKU WA CHAKONICHAKO NA GOUT YA MNADANI WAKO BIZE WANANAFUNA MINOFU NA KUACHA TUNATESEKA SANA

NINA HASIRA NA KILA MWANASIASA NA HATA MUNGU ANGEKUA MWANASIASA BASI NA YEYE NINGEMCHUKIA

So long Tanzania ya Nyerere,............
 
Wewe ndo umeongea PUMBA humu nyie ndio msiopenda maendeleo kilichokufanya uandike uchafu wako humu ni nini kama ungetaka kujibu si ujibu hoja nini kumsema mwandishiMtu katoa maoni au hujaona alichoandika alichoona? Fikiria kabla ya kupurukuka kujibu PUMBA

Ni kweli kabisa, mara nyingi kibinadamu, mtu aliyeumia au kuathirika kwa namna yoyote ile huwa na pumba zaidi ya busara and my pumba confirms my depression

Una dawa yoyote ya kuondoa hizi pumba kichwani mwangu??

Je na wewe tangu usome bandiko kuna unafuu wowote uliotoa kwa mtanzania wa kawaida??
vipi kuhusu mchango wako kwa ujumla kwenye post number 1??? maana labda ungechangia positively na mimi ningefunguka kidogo lakini naona umeruka juu kama Angela MAo kwenye muvi za bruslii lakini umetua na sauti tuu ya mgumo bila hoja kwa mleta mada

Ukiweza kunipa dalili za nafuu ntashukuru sana lakini kwa sasa i am depressed .... Na naskia kuna show ya kuchangamsha wabunge wikendi ilikua nzuri kwenli aisee
 
Mkuu upo Dom nini?
 
Kwa Pawaga, Tungamalenga, Mtera/Migoli. Kuwa stendi muda huo nakubali,lakini huko kuna joto. Labda makete hasa maeneo ya bulongwa na ujuni. Njombe nadhani kule lupembe. Hata hivyo jaribu kujiuliza maeneo hayo ni lini wamethubutu kuchagua nje ya ccm?
 
Sasa wakisubiria mpaka uchaguzi ujao si watakua wameisha?!Ungewaambia mapambano ni leo na sio kesho.
 
Kila uchao naamini uhalali wa ccm kuendelea kuitawala tz hii kwa mgongo wa K/nyanya unafika kikomo!

Hali ya maisha vijiji inatisha ndugu zangu na watu wameanza kuamka, sasa wanasema bila kutafuna manene kuwa ccm ijiandae kuwa chama cha upinzani na wanapendekeza kuwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani atakuwa Nape!

Kwakweli sijawahi kuona Wanyalu wakiwa na hasira na ccm kiasi kile! Wanadai maisha yamekuwa magumu kupita kiwango!

Utafiti nilio ufanya ktk vijiji sita vya kata yetu juu ya mahitaji muhimu ya binadamu yapo juu kuliko hapa dar.
Mafuta ya taa lita 2,700/
Sukari kg. 2,500/
Chumvi kipaketi 500/
Sabuni kipande (komoa)400/
Kibiriti 100/
Lita moja ya ULANZI 200/
Bia 2,000/
Soda 600/
Usafiri umbali wa km 12 wenyeji wanatembea kwa miguu mpaka stendi,kukodi gari 25,000/
Zahanati ipo kila ukienda uwe 5,000/ mkononi
Shule ya msingi ipo na imefaulisha 28 kt 88
Shule ya sekondari ipo bado ni mpya!

Maisha ya wakaazi ni ya wakulima na walevi waliochoka na maisha, kijana wa miaka 20 ukimuona utadhani ni mzee wa miaka 60!

Hali ya hewa ni baridi na ukungu la kufa mtu!

Hali ya chakula si nzuri watahitaji msaada mda si mrefu!

Nimeamua kurejea mjini ili kupambana vizuri na serikali dharimu ya ccm na Kikwete wao baada ya kuwahamasisha na kutoa elimu ya uraia kwa vijana wote ktk kata yetu! Nimewafahamisha kuwa vyama vingi si uhalifu na nikawaambia vijana kwa wazee ccm haiongozwi na Nyerere kama wanavyo dhani,ila inaongozwa na muhuni fulani aliyempigu Vasco Dagama!

Nashukuru wamenielewa wakafanya tambiko la nguvu na kunituma nije town kulikomboa taifa!

Nimewaahidi kila mwaka nitakwenda kuwaelimisha na kuuweka wazi uozo wa ccm mpaka 2015!

Umekumbuka kuwaambia kirusi aina ya CCM ni hatari kwa maisha yao?na hayo ndio madhara ya kukichagua kirusi hicho?
 
Sasa wakisubiria mpaka uchaguzi ujao si watakua wameisha?!Ungewaambia mapambano ni leo na sio kesho.
Nimeanza na elimu kwanza! Nadhani mpaka 2015 uadui kati ya wananchi wale na kirusi kiitwacho ccm itakuwa sawa na ufisadi na cdm!
 
Back
Top Bottom