Nipo njia panda

Nipo njia panda

Ndugu wakuu nina mchumba ambaye tumedumu kwa miaka miwili,kiundani nampenda sana ila yeye hanionyeshi mapenzi ya kweli yaani nisipopiga simu anaweza kukaa kimya hata siku nzima pia hapendi kujishusha na kukubali makosa yake hata kuomba msamaha ni vigumu mwezi uliopita nimekutana na msichana mwingine anayenivutia sana(very cute) na anadai yeye ni bikira ambaye ameweka nadhiri na Mungu kutofanya mapenzi mpaka ndoa kwa uzoefu wangu kweli inaonyesha hajawahi kuwa na mtu maana aibu imemjaa usoni na pia kwa umri wake(20yrs) kuna uwezekano anachosema ni kweli,mimi pia msichana niliyenae ndio wa kwanza napata shida kumkubali huyu dogo maana niliyenae nampenda sana najisikia hatia kumsaliti na kumwacha na huyu ndio muda mwingi ananitafuta,kiukweli nipo kwenye njia panda

Kupigiwa simu au kuandikiwa sms siyo kipimo cha kupendwa sana hupaswi kumhukumu kwa hili ila mjengee mazoea ya kufanya hivyo. Kuhusu kujishusha na kuomba msamaha kuna baadhi ya wanaume na wasichana hawajui au hawana hiyo hulka japo wanakuwa wamejutia waliyoyafanya...hili nalo mnapaswa kuliongea ili taratibu muendane. Hili la bikra ambayo umegundua kwa aibu na umri mdogo kwa huyu mpya utakuja lizwa, kwanza siyo jambo la busara kuongelea swala la bikra na mwanamke. Aibu na umri mdogo siyo kipimo cha bikra, pia waogope sana wanawake wanaotumia bikra kama silaha ya kuolewa kwani unapaswa kutambua hiyo bikra haitakuwepo maisha yenu yote ila upendo wenu utadumu milele. Najua umeona haya mapungufu baada ya kumpata mwingine ila usijaribu kukimbizana na hawa watoto watakuliza mchana kweupe. USHAURI, mfanye huyo uliye naye kuwa mwanamke wako kwa kuvumiliana na kumwambia yale unayotaka kwake hadi mfanane kwa kiasi fulani...pia usijione malaika bali angalia mapungufu yako na umpe nafasi ya kukubadilisha. Achana na huyu mtoto kwani atakupeperushia njiwa wako kumbe yeye bundi.
 
dont complicate things hata kama hajakupigai sim siku nzima

it doesn't mean that she doesnt love you.......,

anataka kila baada ya nusu saa aone simu screen yake inaita "my swty" loh shughuli si ndogo hapa
 
Sema umemchoka sio njia panda miaka hiyo miwili mlokua nayo hukuona km hilo tatizo ila kwakuwa leo umepata mwngne ndo unaona tatizo?? Usisahau zimwi likujualo na pia fagio kuu kuu ndo linajua kona zote ndani ya nyuma shauri yako maradhi mengi

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
hahahaha na haya ni makavu live......source Mpoki ze comedy

Yaani kanikera sana huyu mwanaume mwenzangu....

Unakaa na mtu muda wote huo kumbe moyoni una hila...

Mtu ambaye una mpango wa kuishi naye, miezi 6 tu ya mwanzo inatoa picha kuwa ni mtu huyo anafaa au hafai...
 
Yaani kanikera sana huyu mwanaume mwenzangu....

Unakaa na mtu muda wote huo kumbe moyoni una hila...

Mtu ambaye una mpango wa kuishi naye, miezi 6 tu ya mwanzo inatoa picha kuwa ni mtu huyo anafaa au hafai...

hizi mbwembwe kazianza bado kila mtu anakaa kwake je wakiishi miaka mitano ya ndoa,ndani ya nyumba moja si ndo atasema mwanamke mchawi nk.
 
katika mahusiano changamoto ni lazima , vumilia mueleze then ndiyo uamue usijengwe na tamaa kila binadamu ana mapungufu yake .
 
Acha umalaya wew.kisa haku sms unasema hakupendi,mwache ndo utajua umuhimu wake jinga wew
 
huyo wa miaka miwili uliyemzoea ni bora kuliko wa siku mbili usiyemjua... acha tamaa
 
Back
Top Bottom