Yimakatso
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 6,974
- 9,334
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 26 nilitokea kuzaa na binti akiwa bado anasoma kidato cha nne.baada ya kujifungua aliendelea na masomo mwishowe alifanikiwa kumaliza masomo yake ya chuo.Kwasasa ana kazi yake hivyo tunasaidiana kulea mtoto wetu pasipo wasiwasi.Bahati mbaya tena mwishoni mwa mwaka jana nilijikuta kwenye mahusiano na binti mwingine na kinachoniumiza kichwa zaidi ni kwamba huyu binti ana ujauzito wangu na amekataa kutoa amesema yupo tayari kulea hata peke yake ili mradi tu niikubali mimba na aje nyumbani kwetu kutambulishwa kama mke mtarajiwa.Tatizo lipo kwa huyu mpenzi wangu wa mwanzo ambaye nilizaa naye awali aliwahi kunionya endapo akisikia nimempa mimba msichana mwingine basi yeye ni shurti anywe sumu pamoja na mwanangu wapotee duniani ili aepuke aibu ya mimi kumdhalilisha kwa kumpa mimba msichana mwingine.Kwa upande wa huyu msichana wa pili amesisitiza hayupo tayari kuachana namimi kwa namna yoyote ile kwa maana akitarajia ndoa.Hofu yangu ni kwamba huyu mpenzi wangu wa awali akisikia juu ya kumpa ujauzito bnti mwingine anaweza kutekeleza azma yake ya kujiua yeye na mwanangu,je nifanye nini kunusuru tishio hili lililopo mbele yangu?Kisa ni kirefu ila nimejaribu kufupisha sana japo wadau mpate namna ya kunishauri.Natanguliza shukrani kwenu.