Nipo njia panda naomba msaada kwa hili

sambenet

Member
Mar 5, 2011
47
7
habari zeni Great thinkers, Naanza kama ifuatavyo, Kitambo niliwahi kuomba msaada kupitia Jamvi hili kuhusu Mchumba wangu.
Mimi ni kijana wa Kiume Nilieko Ughaibuni na nilimchumbia Msichana mmoja baada ya kukubaliana, ingawa mwanzo alikuwa na whats so called "sitaki nataka".
Sasa tatizo lipo kwenye mawasiliano maana mimi ndo nipige simu kila wiki na kama sikupiga basi ndo haniulizi naweza kukaa wiki 3 nisipate hata sms 1. nikimuuliza oo simu haina credits, oo mara sim mbovu. Ila akiwa na shida ya kitu lazima atatuma sms na kwa namba hiohio yake. Mama yake aliniambia kweli sim ya mwanawe ina matatizo kweli na namuamini kwa hilo.
Kinachoniumiza na kujiuliza je kweli inawezekana mtu mchumba wake asiwasiliane nae hata sms kwa sim ya mtu mwengine kama ya Mama yake au Baba ake. Nahisi hana feelings kwangu au Mnanisaidiaje Kwa hili?

Jengine ni kwamba nilikuwa na mahusiano au urafiki na msichana mmoja hukohuko Tanzania kabla sijaondoka ila nilikuwa nikiyaona ya kawaida tu,
Kumbe Mwenzangu alikuwa na hisia za Kimapenzi kwangu kwani nilikuja kugundua wakati nishafika huku Ughaibuni, alinimkia mwenyewe baadae baada ya kujua nina mchumba tayari. Lakini anawasiliana nami kila siku ya Mungu mpaka naanza kumuonea huruma Kwa bidii yake.
Hebu jamani nipeni ushauri hapa maana sijui niamue nini mpaka sasa.
 
Pole.
Kiukweli huyo mchumba wako anakuyeyusha tu,cha msingi komaa na huyo mwingine ambaye wewe mwenyewe umekiri kuwa anakupenda na alikutamkia hapo awali.
Be brave!
 
ushauri juu ya nini???mana ka kusoma hujui hata picha tu ka huyu ni mbuzi ama mbwa???
MMMhhh, mbona swali lake kauliza sawa tu mkuu? anauliza hivi: amfanyeje huyo mchumba wake asie wasiliana nae ila tu yeye akipatwa na shida? kweli yawezekana mtu anae kupenda apige wiki 3 bila kuwasiliana? na kama inawezekana mbona huyu dada mbgine anae mpenda anawasiliana nae kila siku?
haya sasa, umesha pata picha, jibu sasa
 
Piga chini mwenyewe nilikuwa naye kama huyo nikaona ananipotezea time hana future,penda ulipopendwa,waambie hata kama kujaribiwa syo hvyo,hata muonja nyama huonja kipande syo unasema unaonja huku unamaliza nyama nzima.
 
Kaka maisha kupendana, wengine hawapendeki. Ukiweza mpenda uyo wapili fanya kweli ila usije muumiza kwa kumbu2 za uyo anae kutumia
 
uuuwiiiiii kesi za mapenzi mungu saidia hili ni janga la dunia..wewe mpende huyo anayekupenda bwana...asiyekupenda achan naye ila mtaarifu kuwa me and you its over nadhani yupo anaye maanisha mapenzi juu yangu ili awe awear .. na machakato mzima ....
 
mpende akupendaye kaka. Huyo anayekupenda mvute na huyo unayemwita mchumba tupa kule wanamchakachua huyo utakaaje wiki 3 bila mawasiliano. Hebu kaa kimya miezi 3 uone kama atakutafuta
 
Jamani ww kaka mbona unapata tabu bure,huyo dada wa watu keshakwambia nakupenda na anatimiza wajibu wake bila kujali umbali uliopo na pamoja na kujua una mchumba still amepata ujasiri wa kukueleza la moyon bado tu unaulizia cha kufanya na huyo anayekutafuta wakati wa shida zake,fungua macho yako usipoteze mda mpe nafasi anayekupenda acha kumbembeleza huyo asiyojua thaman ya penzi lako.
 
Kuna watu hawapendika,fanya utakavyofanya.yeye kukutafuta mpaka awe na shida.
Fanya mpango umchukue huyo anaekupenda
 
pole kaka...ukweli ni hivi kaka....mapenzi ya mbali ni undanganyifu tuu....hata huyo wa pili ambaye anajitiada sii vyema kuanzisha mausiano naye. upo mamtoni tabu ya nini tulizana tafuta wa huko huko au subiria ukirudi bongo utafute.
 
Jamani ww kaka mbona unapata tabu bure,huyo dada wa watu keshakwambia nakupenda na anatimiza wajibu wake bila kujali umbali uliopo na pamoja na kujua una mchumba still amepata ujasiri wa kukueleza la moyon bado tu unaulizia cha kufanya na huyo anayekutafuta wakati wa shida zake,fungua macho yako usipoteze mda mpe nafasi anayekupenda acha kumbembeleza huyo asiyojua thaman ya penzi lako.

yap!....umenena kweli tupu,...halaf hayo mapenzi yenu ya kulimbikiza yanawakosti lakn hamkomi,..kwani ukienda ughaibuni bila kuwa na mchumba tz_ili kusudi ukija uje upate mpya mnaona ubaya gani?...maake nimeona wengi mnalia kwa kutendwa na wachumba wenu,...fungukeni macho bhana
 
tafuta msichana huko huko hawa wa huku wako kimaslahi zaidi,tena huyo anayejua una galfriend na uko ughaibuni muogope.mwizi huyo kamata
mwizi meeeeeeeeeeeeeeeeeeeeen!
hujasema huyo galfriend wako ana kazi yenye kumuingizia kipato????inawezekana kweli anataka kuwasiliana na wewe sema hela hana,kama vipi uwe unamtumia hivyo vidola sijui pounds uone kama hawasiliani na wewe.....kusema ule ukweli mie ningewabwaga wote wawili ningerudi na mzungu....
 
habari zeni Great thinkers, Naanza kama ifuatavyo, Kitambo niliwahi kuomba msaada kupitia Jamvi hili kuhusu Mchumba wangu.
Mimi ni kijana wa Kiume Nilieko Ughaibuni na nilimchumbia Msichana mmoja baada ya kukubaliana, ingawa mwanzo alikuwa na whats so called "sitaki nataka".
Sasa tatizo lipo kwenye mawasiliano maana mimi ndo nipige simu kila wiki na kama sikupiga basi ndo haniulizi naweza kukaa wiki 3 nisipate hata sms 1. nikimuuliza oo simu haina credits, oo mara sim mbovu. Ila akiwa na shida ya kitu lazima atatuma sms na kwa namba hiohio yake. Mama yake aliniambia kweli sim ya mwanawe ina matatizo kweli na namuamini kwa hilo.
Kinachoniumiza na kujiuliza je kweli inawezekana mtu mchumba wake asiwasiliane nae hata sms kwa sim ya mtu mwengine kama ya Mama yake au Baba ake. Nahisi hana feelings kwangu au Mnanisaidiaje Kwa hili?

Jengine ni kwamba nilikuwa na mahusiano au urafiki na msichana mmoja hukohuko Tanzania kabla sijaondoka ila nilikuwa nikiyaona ya kawaida tu,
Kumbe Mwenzangu alikuwa na hisia za Kimapenzi kwangu kwani nilikuja kugundua wakati nishafika huku Ughaibuni, alinimkia mwenyewe baadae baada ya kujua nina mchumba tayari. Lakini anawasiliana nami kila siku ya Mungu mpaka naanza kumuonea huruma Kwa bidii yake.
Hebu jamani nipeni ushauri hapa maana sijui niamue nini mpaka sasa.

Kaka Penda unapopendwa Utakuja Penda usipopenda, akili mkichwa meeeen!
 
waswahili wanasema mpende akupendae,asikekupenda achana nae-
huyu anayesema simu yake ni mbovu ni mwongo-kama mtu anakupenda atafanya means zozote mzungumze,kama mama yake anamtetea kuwa simu ya mwanae ni mbovu-huyo mama pia ni mwongo,maana kuna wamama wasanii pia-inawezekena anafahamu kila kitu-ila anamtetea huyo binti
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom