Nipo njia panda katika issue ya mapenzi, mawazo yenu

Elishy

Member
Mar 3, 2017
55
28
Na umri wa miaka 25, historia yangu ya mahusiano in short nilipenda kweli kuwa katika mahusiano ya kudumu but kitu kimoja nilikuwa nikishatembea na mwanamke sijisikii tena kuendelea nae ila ikafika kipindi nikampenda sana dada mmoja ila hakuwa na tabia nzuri ila nilijikuta nimefall na ile hali ya kumpenda na kumchoka mwanamke ikaisha kipindi hicho nipo advance.

Wakati nipo shule kumbe yule dada kutokana na tabia zake alipewa mimba na jamaa mmoja anapesa na nilikuwa nakaa nae jirani mwanzo sikuwa najua mimba ni ya nani kwa sababu alianza kuniambia ni yangu ila nilipokuja kutambua japo nilimpenda sana ila ghafla nikawa sipo tayari kuwa nae ikawa hivi.

Japo yalishatokea nikiwa napata hamu namtafuta tuna do na yeye alikuwa tayari hata nimuoe ila mimi sikuwa tayari baada ya muda nikaona ni upuuzi nikamwambia tuishie pale sasa mtihani ni huu toka nimeachana nae nimejarbu san kutafuta mwanamke ambaye naweza kuwa nae serious katika mahusiano ila imekuwa kama mkosi.

Nikikutana na mwanamke hachomoi kwa sound zangu but now mpaka najifeel kiwango cha kutongoza kimeisha au ni mkosi maana naweza kutana na mwanamke mzuri tukajuana ila nikishamtongoza inakuwa ngumu kukubali wengi unakuta wanasema wapo katika mahusiano wengine wanasema kabisa yupo single but hayupo tayari.

Nimevumilia kwa muda sana pengine yule anayeniambia yupo single atabadili mawazo but imekuwa ngumu sana mpaka sasa nipo njia panda nafikiria hali hii itaisha lini labda nitampata na mimi nitakayempenda na yeye atanipenda au ndo mazima haitatokea mpaka sometime nafeel niwe player but sure sipendi hiyo tabia na kwa umri wangu naamini natakiwa nipate mwanamke wa malengo.

Msaada wenu wana JF, ni mgeni kidogo nimeiona michango yenu nikaona nami niwashirikishe hili.

AHSANTENI
 
Mkuu mshukuru Mungu kwa kukuepusha na hao viumbe. Huwezi jua labda wangekuwa wanaingia kingi wangeshakutoa feeder
 
Katika suala la mapenz brother usiharakishe wala kulazimisha jambo. Tubu kama kwa Mungu wako... kama kuna mwanamke uliwah mkosea.. mtafute umuombe msamaha...
Kisha Muombe Mungu akupe wako... usipaparike na mapenz.. at that age.. jenga maisha yako kwanza
 
Tafuta pesa kila kitu kitanyoooka tu, bila pesa hutaisha kuandika thread za dizaini hii, trust me
 
Acount yako ya bank inatarakimu ngapi? Tuanzie hapo kama hazizidi 7 basi jifikilie upya unataka nini.
 
Katika suala la mapenz brother usiharakishe wala kulazimisha jambo. Tubu kama kwa Mungu wako... kama kuna mwanamke uliwah mkosea.. mtafute umuombe msamaha...
Kisha Muombe Mungu akupe wako... usipaparike na mapenz.. at that age.. jenga maisha yako kwanza
Amina kaka nimeupend ushauri wako
 
Back
Top Bottom