Nipo kwenye basi naenda zangu mkoani

John W. Mlacha

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
3,504
1,341
Jamani niembeeni safari njema niko kwenye basi hapa jirani yangu anakula mahindi ya kuchoma mayai na anakunywa maziwa ya mtindi haya bila shaka. Sijui hata itakuwaje hapo badae maana safari yenyewe tunafika kesho asubuhi.
 
umeumia wewe.....
Enzi hizooooo nilisafiri kwenda musoma kupitia njia ya kati......
Jirani yangu alikuwa mwanamama na mtoto kama miaka 5 hivi....
Kwanza alimpa chai na andazi........
Then karanga......
Kufika mahali akampa wali....
Then mayai ya kuchemsha
Na vyakula vingine sivikumbuki....

Nakwambia mtoto alikuwa busy kutafuna kama hatoviona tena....
Raha ilikuja tulipoingia ngorongoro....... Si harufu hiyo....
Nilikomaje.......
Mpaka kuja kupata choo na kumsafisha mtoto nilishiba ile harufu........

Toka hapo hakumpa tena mtoto mivyakula hovyo hadi tulipoingia msm!!!!!!
 
mungu ni mwema utafika salama,japo hiyo mixer ni kama unamchokoza uone utafanyaje
 
Jamani niembeeni safari njema niko kwenye basi hapa jirani yangu anakula mahindi ya kuchoma mayai na anakunywa maziwa ya mtindi haya bila shaka. Sijui hata itakuwaje hapo badae maana safari yenyewe tunafika kesho asubuhi.

bila shaka analamba lamba hayo maziwa kama avatar yako Black Bat
 
Last edited by a moderator:
Mbona anakula vitu vidogo tu hivyo?wengine wanabebaga makande,samaki,uji,mandazi n.k

usijali utafika salama salmini
 
Muulize hivi: 'sahani kaka/dada huwa unasafiri sana? Lengo ni kujua kama ana uzoefu wa mitikisiko ya mabasi, kama sio msafiri wa mara kwa mara basi nunua mfuko wa rambo wa sh.500, utakusaidi kujilinda na milipuko...jamaa 'atarudisha chenji' muda sio mrefu
 
kaazi kweli kweli
 
Back
Top Bottom