Nipo katika mahusiano kwajili ya kupata faraja

selina mrembo

Member
May 18, 2020
54
68
Nilikuwa na mahusiano lakini badaye yakavunjika, yalivyovunjika nikawa na wakati mgumu sana ku-recover lakini ikanibidi niwe na mahusiano mapya kwajili ya kupata faraja. Kwakweli sikuchukua mda maumivu yote yakaisha na nikamsahau kabisa X wangu.

Mahusiano ya sasa nampenda sana huyu mwanaume na anaonesha kunipenda pia lakini shida tuko dini tofauti, kosa dini kwakweli niliridhika kwa kila kitu yaani kupanga naye maisha muda mwingine huwa namtumia text nikimwambia tuachane kwasababu naona mahusiano yetu hayana future. Utakuta anakosa raha na kulalamika sana kwamba ananipenda na ananihitaji na hiyo siku atatuma meseji nyingi sana za kulalamika kwanini naamua kuutesa moyo wake n.k na anaonesha kukosa raha.

Huyu mwanaume ana sifa ninazozipenda na ninampenda kupitiliza mara nyingi inatokea namtumia meseji za kumwacha akilalamika tunaanzisha tena mahusiano, nimemwacha kama mara 4 namtumia text za kumwacha akilalamika namwomba sorry tunakuwa tena pamoja na hatuchukui hata masaa kupatana tena.

Shida hawa waislamu wanakuwa na wake zaidi ya mmoja ndio maana inaniwia vigumu sana kujiattach moja kwa moja angekuwa kama msabato T.A.G etc yani angekuwa na dini inayorelate

Na mimi kwakweli nilishamkabidhi maisha yangu all in all bado tupo kwenye mahusiano lakini nimekuwa mtu ambaye nipo for temporal tu not permanent.

Napoteza hadi mood sometime kwajili tu ya dini yake ila nampenda sana jamani.
 
Daaah? Maisha haya bhna. I wish kusingekua na matabaka duniani, yaani mambo ya dini sjui kabila, tajiri na maskini n.k. i wish wote tungekua kitu kimoja... Imagine, mtu anataka kuvunja mahusiano kisa dini?
 
Hii tunaita "kutoa la rohoni" maana shida yako ulitaka kulitoa tu na wala si ushauri.
All in all wanasema "mapenzi hayashauriki"
 
Mwanamke akishapataga mtu wa kumletea drama na anamvumilia anajionaga kayapatia sana maisha 🤣🤣🤣🤣🤣!!!

Ndugu mtoa mada, kuna wenzio hawapati hata muislamu wa kudolishia we umepata bwana unaanza kuleta pigo za kishamba!?

Kama jamaa anakupenda na ana nia ya dhati mtayamalizia bomani kwa DC! Acha mambo ya kijinga.
 
Mwanamke akishapataga mtu wa kumletea drama na anamvumilia anajionaga kayapatia sana maisha !!!

Ndugu mtoa mada, kuna wenzio hawapati hata muislamu wa kudolishia we umepata bwana unaanza kuleta pigo za kishamba!?

Kama jamaa anakupenda na ana nia ya dhati mtayamalizia bomani kwa DC! Acha mambo ya kijinga.
Naunga "mkonyo hoga"
 
Mim nitakua tofauti na baadhi ya comments, mimi ni muislamu, nakuhakikishia mkuu madhara ya kuwa na dini tofauti ni makubwa kuliko faida..nlikua na mahusiano na msichana aliekua na kila sifa niliyoitaka ila tukakaa, tukazungumza and friendly tukaachana japo kwake haikua rahis kama hivyo wew. Kwenye mambo ya mahusiano kuelekea ndoa, msijiangalie nyinyi tu kwa vile mnapendana, angalieni na kizazi chenu especially pale ambapo mmoja ataondoka, watoto huwa wanayumbishwa sana! Subir wa likely imani yako dada, na utapata!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mim nitakua tofauti na baadhi ya comments, mimi ni muislamu, nakuhakikishia mkuu madhara ya kuwa na dini tofauti ni kubwa kuliko faida..nlikua na mahusiano na msichana aliekua na kila sifa niliyoitaka ila tukakaa, tukazungumza and friendly tukaachana japo kwake haikua rahis kama hivyo wew. Kwenye mambo ya mahusiano kuelekea ndoa, msijiangalie nyinyi tu kwa vile mnapendana, angalieni na kizazi chenu especially pale ambapo mmoja ataondoka, watoto huwa wanayumbishwa sana! Subir wa likely imani yako dada, na utapata!

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ujinga haujawahi kuniingia akilini!

Unajua kitu kinaitwa "Liberty" kwenye swala la haki za binaadamu? Iko pia kwenye sheria za uraia.
 
Inawezekana kwa mtazamo mwingne ila kwenye uislamu 'ndoa' ni ibada na ina misingi yake, na kamwe haiwezi kuwa kwa watu wenye imani tofauti! Kama uhuru kwa mujibu wa haki za binadamu sipingani nawe, ila kwa maana na tafsir ya ndoa kwa msingi ya kiislamu watoto wao watakuja pata shida nyingi kuliko faida kwenye ishu za mirathi n.k. otherwise sijui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom