Pi Network
JF-Expert Member
- Mar 22, 2016
- 290
- 319
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, huduma zote zimesimama ikiwa ni pamoja na utoaji dawa kwa wagonjwa hali ambao imepelekea watu kukaa kusubiri umeme.
Kutokana na hali hiyo binafsi ikabidi nijipe jukumu la uandishi wa habari wa mda kwa kuzungumza na doctor mmoja ambae alikuwa karibu na eneo nililokuwepo ili kujua undani wake.
Kwa mujibu wa maelezo ya dokta huyo (jina kapuni), anasema tatizo la kukosekana kwa umeme hapa hospitalini si jambo lililo anza leo, anasema hili ni tatizo la mda mrefu na mara kwa mara wamekuwa wakililalamikia kwa mda mrefu bila mafanikio.
Swali la kipima joto kwa wote mliopo humu; inawezekanaje hospitali kubwa namna hii na inayotegemewa, Tanzania nzima kama sio (Africa Mashariki) kukosa umeme wa uhakika?