Nipeni Ushauri JF: Huyu Jamaa si Anataka Kuniibia!!?

Nipeni Ushauri JF: Huyu Jamaa si Anataka Kuniibia!!?

Junius

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Posts
3,180
Reaction score
149
Wadau JF naomba ushauri kuhusu huyu jamaa amekuwa akinitumia e mail akinitaka kumsaidia kuhamisha fedha kwa kutumia akaunti yangu. Hii ni mara ya pili kupata e mail ya namna kama hii, mara ya kwanza nilipata kwa jamaa ambaye kwa mujibu wa jina lake nahisi ni kuoka Afrika ya Maghribi, baada ya kuisoma tu nikaifuta. Leo nimeona e mail nyengine kutoka kwa mtu mwengine nahisi vilevile kutoka Afrika Magharibi, kinchonishangaza vp wanapata e meil yangu.Najua kama huu mchezo ni wakitapeli ninachowataka kunijuulisha kama naweza kumjibu nikamueleza kuwa akome kunitumia e mail za kitapeli, au nikikontakti nae itakuwa ndo nimejiuza.Nawasilisha na haopo chini ni e mail yenyewe.



Dear Friend

Greetings to you. After getting your contact information through a personal search and I have this strong personal conviction that you can handle this transaction perfectly on my behalf; I am Mr. Ahmed Owusu, a retired banker.

I am writing to solicit your assistance in the transfer of US$5,300.000.00 dollars to your nominated bank account. This fund is an excess of what my branch in which I am the manager made as profit before I retired from office. Since then, I have placed this $5,300.000.00 on Escrow call account without a beneficiary in our bank. I contacted you for assistance after getting your information during my personal search.

As a manager with the bank then, I cannot be directly involved in this money, thus I am impelled to request for your assistance to receive this money into your bank account. I intend to part 50% of this fund to you While 50% shall be for me. This transaction is legal and practically no risks involve, it will be a bank-to-bank transfer. All I need from you is to stand as the original depositor of this fund.

Await your reply for more details.

With Regards,

Mr. Ahmed Owusu.
00233242213059
Note: I am dealing with you on a personal note, Hence you have to keep this transaction confidential.
 
Junius,
Wala usipoteze muda kumjibu, hao ni matapeli. Next time huna haja kusoma content nzima kutambua kuwa hayo ni magumashi.
 
Junius, Junius, mpaka leo hujajua hizi scam za Wanigeria? Achana nao haraka sana, au watakuliza!
 
Hawa ni macybers man wala usipoteze muda wako, Kuna frauders kibao achana nao na usifanya wala kuwarudishia majibu katika email yako, Wapo kila sehemu hata Africa, Senegal, Mali, Na hasahasa West Africa, Na wanashikiana na watu wao wako Ulaya, Achana Nao
 
Nasikia kuna mtu ambaye hakuwa anawafahamu vizuri, walienda naye mpaka akawapa details za akaunti yake ya benki na baadaye alikuta wameiba pesa kwenye akaunti yake.

Na yuko jamaa mwingine yeye aliwashtukia akawaambia kama wanataka kuhamisha pesa kupitia kwake basi wamtumie angalau hata dola 1000 ili afungue akaunti ya kupitishia hizo pesa wale jamaa wakamwambia kuwa hayuko serious basi ndo ikawa mwisho wa mchezo.

Mimi nimeshapokea pia emails zao zisizo na idadi. Na ukitaka kujua kuwa ni za utapeli utakuta kuwa wakati mwingine hiyo email imetumwa kwa "undisclosed recipients (ina maana imetumwa kwa watu wengi si wewe peke yako)

So Junius hao ni matapeli na wezi wa hali ya juu, achana nao.
 
Mazee mbona unaanza kutuaibisha wana-jamvi? Kumbe ujanja woote mwisho ni JF tu..aaarrghh.. Wewe msaidie msela kuhamisha 'ela' zake kwenye akaunti yako halafu za utatupa simulizi iliyokamili hapa JF ili ibaki kumbukumbu humu jamvini..
 
Usijibu hao ni 419 scam!

siku hizi tunawaita "Yahoo Yahoo".....

Junius....if you fall "Mugu"...i will be your "Master ooohhh".........me go chop ya dollar ooohh
 
Mazee mbona unaanza kutuaibisha wana-jamvi? Kumbe ujanja woote mwisho ni JF tu..aaarrghh.. Wewe msaidie msela kuhamisha 'ela' zake kwenye akaunti yako halafu za utatupa simulizi iliyokamili hapa JF ili ibaki kumbukumbu humu jamvini..
On the other hand, I only want to share this infos with others in JF.
Lakini Mkuu kama utanipa akaunti namba yako tujaribu poa tu.
 
Usiwe na wasi wasi Mkuu Junius.Hii ina maana mbili
1 Kuna jamaa(anaweza kuwa Mnigeria au any West African) ambaye ameona email yako ukifanya international tranzaction na hivyo anajua una fedha

2 Huyu jamaa lazima atakuomba bank details zako-USITHUBUTU KUFANYA HIVYO

3 Kwa vile ana email address yako unaweza kumuandikia the roughest language you have.

4 Akipata majibu matatu au manne kama hapo no.3 atajiju

Mimi nimepata hizo emails nyingi sana na kuzifuta peke yake haitoshi MJIBU as in no3.
 
Back
Top Bottom