Pole maa! Wote wanaofanya hivyo ni wagonjwa wanahitaji kutibiwa kama wagonjwa wa mfadhaiko, kuwapa mob justice si kuwasaidia bali kuwaumiza zaidi. Hata kuwafunga jela si suluhisho wanahitaji matibabu na mara nyingi uwezekano wa kupona ni mkubwa kiasi.
Way 2006 kuna mmoja alinichafua kabisa pajani na sp...! Tulikuwa kwenye daladala la Mwananyamala - Posta. Alishukia pale kinondoni Muslim, sikumuambia mtu nilikaa kimya as nilikuwa najua hawa ni wagonjwa. Yeye alichafuka sana, nilijua nikisema wangempiga halafu ni Kinondoni! Nilifika chuo na kuomba jeans ya jirani basi na kuwasimulia yaliyonikuta. Nakumbuka alikuwa mkaka handsome sana kavaa miwani yake poa kabisa na smart attire.