Nipeni pole,wakaka/wababa nisaidien kujua 7bu ya baadhi yenu kufikia kufanya upuuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nipeni pole,wakaka/wababa nisaidien kujua 7bu ya baadhi yenu kufikia kufanya upuuzi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Cantalisia, Oct 12, 2011.

 1. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Habari zenu wadau,leo nimekuwa na asubuhi mbaya sana na hata itapelekea kuifanya siku yangu nzima ya leo kuwa mbaya,nikiwa njian nakuja kazini asubuhi kutokea mwenge kuja posta,nashukuru nilipata siti sio ya dirishan,gari ilikuwa imejaa sana watu wengi walikuwa wamesimama,pembeni yangu alikuwepo mbaba kwa kumkadiria ni km miaka 35-40 hivi alikuwa nadhifu na shati lake lilikuwa na jina la benki moja kubwa hapa mjini,yule baba kadri safari ilivyoendelea alizidi kunisogelea mpaka akawa ameegemea kile kiti na kunigusa kwenye bega la kushoto akiwa anatizama dirishan.

  Kutokana na hali ya hewa ya leo ya mvua kulikuwa na folen sana tulipofika maeneo ya moroco nikawa nasinzia ila sio usingizi mzito,nikawa nahisi km kuna kitu kinanipapasa au km kusugua kwa mbali nikafumbua macho nikamwangalia yule baba naye akaniangalia nikawa sijaelewa kitu nikaendelea kulala,baada ya muda tena ile hali ikaanza nikisikilizia kwa muda nikiwa bado sijagundua kinachoendelea nikamtizama tena yule baba hakunitizama akawa anaangalia nje,nikendelea kulala ila nikiwa nasubiri ule msuguo uanze,na kweli haikupita mda ukaanza tena kwa nguvu na kwa kasi nikafumbua macho nakuangalia ile sehemu, yule baba alikuwa amefungua zipu ya suruali yake na anasugua uume wake kwenye mkono wangu kati ya kiwiko na bega,kwakweli nilishituka sana na yeye wala hakujua km nimemuona akaendelea na mchezo wake.

  wandugu gafla sikujua nifanyeje nilipata hasira nikajikuta nimesimama gafla na kumchapa kofi kali yule baba kabla hasema kitu nikapiga na lingine akabaki amepigwa butwaa suruali iko wazi watu bado wanamshangaa mie nikamwita konda nakuomba asimamishe gari yule baba ndio akastuka na kukimbilia mlangoni akitashuka watu wakamzuia wakanza kumpiga wakizani ni mwizi na ameniibia nikawaambia sio mwizi msimpige akashuka huku akiwa anafunga suruali maeneo ya ubalozi, watu wakanza kuniuliza kwann nimempiga niliwaelezea kilichotokea walishangaa na baadhi kunilaumu kwann sikuacha wampige sikuweza kusema kitu nilinyamaza nikiwa na hasira kupita kiasi,

  kwanza nipen pole balaa hili ambalo nimekuwa nikisikia story tu kwa watu na magazetini, na nawauliza wababa/wakaka ni kitu gani kiasababisha baadhi yao kufanya vitendo hivi,ni makusudi au ni hali inayowakuta bila kujitambua au nikuendekeza tamaa za kijinga?nawasilisha.
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  duh pole sana sana
  hiyo kali mpaka kiwiko mtu anataka kumaliza haja zake
  ni ukame wa aina gani huo
   
 3. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Kwanza pole,..hata kwa hili mimi bado nafikiri nistory uliyoipika_maake sidhani ama sifikirii kama inawezekana kwa mtu mwenye akili timamu kufanya hivyo,....mimi kama mbaba sina mchango kwa hili zaidi ya kudhani ni kastory ka kijiweni,...pole sana da canta
   
 4. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante Mr Rocky,yani hata mie mpaka sasa nashindwa kuelewa kbs!kwan hali hiyo husababishwa na nn?
   
 5. s

  shalis JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona kama yakijiwe hivi ...i dont think if its true... :shock:
   
 6. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Amini usiamini huu ni ukweli na imenitokea mwanyewe leo hii,na kwa mwonekano ni mtu mzima na mwenye akili timamu kbs,na ndio maana mpaka mda huu nashindwa kuelewa aliamua au alitumwa labda na mganga yani sielewi hata hapa oficn kuna watu hajaamin kbs lkn ndio ukweli wenyewe Igwe, asante kwa kunipa pole!
   
 7. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  best pole sana, mi kuna mmoja alikuwa nyuma yangu yuko bize mwenywe habar hata hana mimi ile kugeuka nilimuhaibisha basi zima lilimuona mpumbavu, sio siri watu kama hao wapo sna. ila sijui tatizo nini hasa
   
 8. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Niliangalia Forum gani nikakuta sio chit chat ni MMU, hata mimi sijaamini labda mimi ni tomaso maana bora ingekuwa wameshika bomba kidogo ningeamini lakini mtu aliyekaa anafungua zipu anakula mkono bila watu kumuona kidogo inautata. Lakini Kama ni kweli pole sana Dada, huyo jamaa akiri yake itakuwa sio sawa.
   
 9. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Pole mwaya, haya mambo yanakera asikwambie mtu! Mi mwenyewe niliwahi nusurika na hii kitu, tulikuwa tumesimama kwenye daladala na nyuma yangu alikuwepo huyo mbaba alotaka kunifanyia huo ubazazi. Yaani ka bahati ikatokea nikageuka, my dear nilibaki kuduwaa........!!
   
 10. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  kama hili lipo basi ni zaidi ya udhalilishaji,...anyway poleni sana wadada
   
 11. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Pole sana da Canta,...ila nafikiri huyo jamaa ni punguani,...amejidhalilisha na kutudhalilisha watu wa jinsia yake
   
 12. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Yeah_something is clicking in ma head!..inawezekana hivi vitu vipo na vinafanyika kwenye jamii yetu_maake naona watu wengi wanashuhudia,.....ila its more than inhuman...ngoja namuona naye Bebii anachungulia hapa chini alete ushuhuda wake na namna alivyo deal nalo,....poleni sana
   
 13. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  dah pole sana cantalisia uwe unatembea hata na kiwembe ungemtoa hata sikio akome
   
 14. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  ahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaa!..nilikuona ukichungulia_nikajua ni lazma utaleta suluhu ya hili jambo,.....mm nakukubali kwa self defense
   
 15. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Shalis sweetie, unaweza kuona kama ni utani but haya mambo yapo sana dear. Sijajua tatizo la hao watu!
   
 16. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Bora ww uliyewahi kutokewa coz inawawia ngumu sana watu kuamini,ila ndio ukweli japo watu wanaona kama nimetunga, asante mwaya!
   
 17. bombu

  bombu JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,134
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  yeah, ni kweli haya mambo yapo saaana, na yanatokea kila siku, katika daladala zetu. Mbona tunayashuhudia, anayekataa anataka tuu kuendeleza mjadala, Ila pole sana Cantalisia, coz huyo naona alifika mbaali hadi kufungua zip, shame on them kwa kweli
   
 18. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante kwa kunisaidia,ila ianaiuma coz watu hawaamini kbs but siku ikimtokea mtu ndio ataamini!
   
 19. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante ila najua siku ukishuhudia au mtu wako wa karibu ikimtokea ndio utaami tu!
   
 20. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  yani kama amelala mzungu wa nne na mkewe ndo akuharibie siku asbhi yote iyo dear loh pole sana wanaume hawa khaaa........................
   
Loading...