.Ushauri ni uhame hapo kwa jamaa yako, nenda hotelini. Over
Mkuu umesema umeenda kibiashara, je kama huyo jamaa yako asingekuwepo ungekaa wapi siku zote hizo? Unapokuwa na mashaka sehemu siyo vizuri kuendelea kuishi hiyo sehemu..
Sawa lakini hujanisaidia binafsi kwamba nahama kwa kukimbia nini. Hotel nazo ni ghali sana. Ni nchini Angola ambapo hoteli ya dola mia na hamsini kwa siku ni ya kiwango cha chini sana.
.Mkuu umesema umeenda kibiashara, je kama huyo jamaa yako asingekuwepo ungekaa wapi siku zote hizo? Unapokuwa na mashaka sehemu siyo vizuri kuendelea kuishi hiyo sehemu.
mkuu biga mishe aise nasikia kuna fursa mbalimbali huko angola sema maisha yao ghali sana duuuu ila usiogope hakuna tatizo lolote hapo.
Sawa lakini hujanisaidia binafsi kwamba nahama kwa kukimbia nini. Hotel nazo ni ghali sana. Ni nchini Angola ambapo hoteli ya dola mia na hamsini kwa siku ni ya kiwango cha chini sana.
.Hakuna panya humo? Angalia vizuri maana panya ni uchawi tosha wanakulaga jina tu kwenye cheti na namba tu kwenye hela
.Mkuu kuna kipindi nilikuwa napenda kuangalia kipindi cha " Unsolved mysteries" kwenye television nguri.Mambo yaliyokuwa yakisimuliwa ni kama hayo uliyoyabaini hapo juu.Mimi pia ni mtu nisiyetikiswa na mambo ya uchawi uganga au ushirikina lakini kuna sikuamua kulala kwenye nyumba ambayo iko kwenye hatua ya finishing, lakini haijapigwa ceilling board.Nilichokifanya nilichukua chandarua chenye pembe nne nikaunganisha na kamba kisha nikafunga kwenye mbao za ceilling nikalala hadi asubuhi yake. Kesho yake cha kushangaza kamba moja kwenye pembe moja kati ya nne haikuwepo kwenye ceilling wala kwenye chandarua. Nilitafuta mabaki ya hiyo kamba kwa siku kadhaa hadi siku ya leo sina jibu la hicho kitendawili na maisha yanaendelea. kwenye ceilling hadi leo zile kamba tatu zilizobaki zinaning'inia.Sina majibu ni nini kilijiri.