GE2020 Nipeni miaka mitano muone maajabu

Nasikitika sana siamini kama hizi makitu zinatoka kwako arif.
Mkuu tuikubali demokrasia kuanzia kwa mtu mmoja mmoja. Hii ndiyo demokrasia na political tolerance yake.

Usinishangae ukinishangaa unaniambia nami nikushangae. Mwisho wake utakuwa sio mzuri.
 
Hakuna maajabu yoyote jiwe anaweza kufanya zaidi ya kupoteza watu katika mazingira ya kutatanisha.
 
Mkuu tuikubali demokrasia kuanzia kwa mtu mmoja mmoja. Hii ndiyo demokrasia na political tolerance yake.

Usinishangae ukinishangaa unaniambia nami nikishangae. Mwisho wake utakuwa sio mzuri.
1.Political tolerance, Yes!!
2.Demokrasia hell no!!

Kila la kheri. Btw uko bongo land au kule kwa siku zile?
 
Mkuki siku zote kwa nguruwe lakini si kwa binadamu! Halafu unaandika ujinga ujinga wako. Kwa vile waliodhalilishwa hawakuhusu!
......
 
Jana mlisema Dodoma hakuna nyomi, leo
Mnaifufua ile corona mliyo izika! Mmeshikwa kunako ubaya, mtaweweseka sana!
 
Kama rais ni mtu sio Mungu kwani ni lazima uyo mtu awe Jpm?.Isitoshe kama ni kua raisi tayari kashakua kwahiyo anaweza akapatikana mwingine na nchi ikaenda vile vile.
 
Kama rais ni mtu sio Mungu kwani ni lazima uyo mtu awe Jpm?.Isitoshe kama ni kua raisi tayari kashakua kwahiyo anaweza akapatikana mwingine na nchi ikaenda vile vile.
Ndiyo maana wagombea wapo wengi mkuu zaidi ya watano.

Kinachofanyika tarehe 28 0ctoba kila mmoja anaenda kumchagua wake.

Atakaechaguliwa na wengi anatuongoza. Sina shida kabisa na atakayeshinda tofauti na JPM.
 
Wanafunzi wa Yesu na watu waliokua wanamfuata kujifunza kuna siku walishikwa na njaa.

Walipomfuata Yesu kuwa wana njaa wanahitaji Chakula ,Yesu Kristo Mwana wa Mungu aliye Juu ya Yote na mfalme wa wafalme aliwapa chakula.

Cha ajabu kabisa Mwana wa Mungu aliyejua mahitaji makubwa ya binadamu hakuwapa Reli au Daraja au Majengo ya maofisi.

Wana wa Israel kuna wakati walipokuwa jangwani walikosa Chakula Mungu muumba wa vyote aliwapa Mana lakini hakuwanunulia ndege ya kuwahi kufika Kaanani. Alitaka kuwajengea misingi ya kumjua Mungu na kuzishika amri zake kwa Haki.
Haki inapotafutwa pale ilipokosekana ina gharama kubwa sana mana Mungu hapendezwi na hofu inayowafanya wanadamu kufanya uovu dhidi ya wengine.

CCM na viongozi wa dini ambao ni makada wa CCM wanaoiona CCM kama dhehebu la dini wajue wazi kabisa kuwa bila Haki kusimama kwenye Taifa hili amani itakua ni ya muda sana. Majengo ,mareli ,madaraka makubwa,misafara ya kifahari,kugawa mapesa majukwaani,kutoa masadaka ya kujenga makanisa na misikiti haitasaidia mana hata Gadaf na Sadamu walifanya makubwa sana na kujenga nyumba za ibada lakini Chuku haikutoka kwa wale waliogandamizwa na kufanywa daraja la kukanyaga kwenda juu ili hali wenzao wakiwaona kama takataka naawazo yao kuonekana kama ya kijinga yasiyofaa alimradi wao watulie tu watapewa chakula kama kuku wa kisasa na sio binadam. Mungu haoni shida kuruhusu jambo lolote kuinuka juu ya nchi na wanadam wasiotenda haki.

Wenye madaraka wanajipenda wao sana na ndio maana wanaona sifa kuamuru majeshi kuwaangamiza wengine huku wao wakijilinda kwa kila aina ya ulinzi.

Labda tuwakumbushe CCM na viongozi wa Dini maelekezo ya Mungu wa Haki ni kuwa kila Mtu ampende jirani yake kama nafsi yake.
Na kile usichopenda kutendewa usimtendee mwenzako.

Tukiyapuuza haya na kuipigania CCM ili ishinde wale wenye madaraka wajihakikishie kuendelea na madaraka na Teuzi zao huku wao wakiwatendea mabaya Wapinzani wao hakika hata Mungu hawezi kukaa kimya. Hata shetani hatakaa kimya mana ndiyo furaha yake itatimia huku Mungu akihuzunika kwa mabaya yanayotendeka.

Kwa Muda Mrefu tumeibiwa na CCM kwa sababu ya kupuuza haki na sheria.
Mikataba mingi mibovu imetokana na kupuuza sheria na kutoisoma kwa umakini.
Ni Yeye Lisu aliyesema wakati wezi wanaiba. Wengine walikaa kimya tukaibiwa wakisubiri zamu yao nao waibe kwa mbinu mbaya zaidi ya kuwanyamazisha watchdog.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…