Nipeni mawazo ya Masters degree!

Achukue Masters za Education
 
Sio rahisi kama unavyosema, kwanza siku hizi wanabania mtumishi kwenda kujiendeleza nje ya career yake na ikibainika Mwalimu anasomea uhasibu ana futiwa ruhusa ya kwenda masomoni labda kama una cheza nao sambamba
Na kasheshe zaidi ni pale utakapomaliza alafu ufanyiwe hiyo re-cartegorization ni mtihani kwa kweli
Yeye kama anataka kusoma asome tu For Future personal fights na sio kusema akirudi atakua mtu fulani atapoteza pesa apate stress za kuto kua huyo mtu
N.B Masters ni kama Makeup kwenye Degree yaani ni sawa na kusema Mwanamke mzuri anaongezewa uzuri kwa kupakwa Makeup na hata bila makeup uzuri wake unabaki kua vilevile
Hakuna mshahara wa Masters, na kama unataka kusoma Masters basi uwe na Future plans za kusoma PhD sio uishie hapo Masters, serikalini haina maana sana
 
Huyu mwalimu ni zuzumagic na hajitambui. Mwambie akafanye masters ya cookery itamsaidia. Mwalimu mzima hajui nini cha kufanya maishani hadi achaguliwe na watu asiowafahamu
 
Umesema vyema kabisa mwache ajichanganye ndio atajua ajui.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nani alikuambia ukisoma Business administration ukimaliza unakuwa hujulikani fani yako?Hujui kwamba kwa kozi hii ukifika mwaka wa pili wanafanya specialization?mtu anaweza kuwa mhasibu, Afisa biashara HR officer au Afisa ugavi.
 
Mkuu usiseme Serikalini hakuna Mshahara wa mtu mwenye Masters, be specific kuwa labda idara yako ndiyo haina mshahara wa Masters na sio serikalini kwa ujumla.
Hii ni kwa kuwa kuna baadhi ya idara ninazozifahamu zinaitambua ngazi hiyo ya Elimu na pindi mtu anaposajili Cheti chake huwa Basic Salary yake inabadilika na kulipwa kwa kiwango cha Masters.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Chem+Bios aende Mzumbe akasome Postgraduate ya Public Health, akirudi anapewa idara ya afya hapo hapo Halmashauri.
Halmashauri Kuna ukiritimba kuipats hio nafasi sio mchezo.

Mwaka huu Kuna walimu kibao wenye fani zingine wamerudishwa mashuleni wakashike chako kisa hawana barua za tamisemi.

So uhakika hadi apate barua ya TAMISEMI otherwise ni kupoteza pesa na muda
 
Sio kweli, Mwalimu akitaka kusoma degree ya uhasibu hanyimwi ruhusa isipokuwa ananyimwa mshahara ikitokea anataka kusoma full time masters. na hii ni kwa sababu wanajua ukirudi hutakuwa mwalimu tena na wao serikli watakuwa wamepoteza mfanyakazi wa ualimu na hivyo kulazimika kuajiri mtu mwingine
 
Nani kwa hali hii ya uchumi yupo tayari kuchukua likizo bila Malipo?
Alafu usichoelewa walimu wengi husoma kwa njia ya kuomba mkopo wa bank sasa wewe uchukue likizo bila malipo hilo deni la bank unalipaje?
 
Masters ni ni value added factor not a main Factor, sasa mdanganyeni huyo mwalimu kwamba akirudi atapata mshahara wa Masters
 
Nani kwa hali hii ya uchumi yupo tayari kuchukua likizo bila Malipo?
Alafu usichoelewa walimu wengi husoma kwa njia ya kuomba mkopo wa bank sasa wewe uchukue likizo bila malipo hilo deni la bank unalipaje?
Uoga wako tu mkuu...nina mfano wa watu wengi ambao wamesoma fani tofauti wakati salary zao zikiendelea ku flow na wamefanyiwa re-categorization tayar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…