''Nipe Macho Nione''

''Nipe Macho Nione''

Omary Sameer

Member
Joined
Oct 17, 2018
Posts
6
Reaction score
9
Nipe macho nione kionavyo na wengine ambacho najitahidi kukiona,

Nione mafanikio ya awamu hii tuliopo, awamu ya #hapakazi tuu , awamu ya serikali ya viwanda na ndoto ya uchumi wa kati kufikia 2020.

Macho yangu hayaoni wala akili yangu haitafsiri sawa vile ninavyoambiwa ni mafan ikio ya awamu hii pendwa kwa ''waunga mkono juhudi za mheshimiwa.

Niliambiwa wanaunga mkono Elimu bure kuanzia la kwanza hadi kidato cha nne,

Macho yangu hayaoni kwani nijuavyo kabla ya awamu yetu pendwa tulikuwa hatulipi ada shule ya msingi na sekondari tulikuwa tukilipa ada elfu ishirini kwanini isisemwe kuwa imetolewa ada ya sekondari yaani kidato cha kwanza hadi cha nne michango mingine ipo pale pale na hiyo ada imekuwa ikipunguzwa kila awamu nakumbuka tulikuwa tukilipa elfu sabini(kumbukumbu hazipo sawa hapa) ikashuka arobani kisha ishirini na awamu yetu pendwa ikaitoa hiyo ishirini gharama nyingine zipo kama kawaida.

Nipeni macho niuone huo ubure jamani.
Tunaunga mkono ujenzi wa reli kwa fedha zetu ambazo pengine zingeajiri askari polisi kwani tangu awamu yetu pendwa ianze sijui wameajiriwa polisi wangapi maana kuna bosi wa benki alisema alitumia wanajeshi kwa kuwa pilosi walisimamia mitihani ya kidato cha pili kule Arusha je, hali si mbaya?

Nipeni macho nione walimu ambao licha ya uhakiki usioisha wamekuwa wakiahidiwa kulipwa stahiki zao mwaka wa tatu sasa achana na wale waliopelekwa kufundisha shule za msingi kwa kuwa sekondari zina ziada ya walimu wa 'sanaa' hivi lile lengo la wanafunzi 40 kwa walimu mmoja ilifia wapi?

Nipeni macho nione kuwa shule za msingi zikiwa hadi na walimu wa ziada kwani katika miaka mitatu walioajiriwa hawafiki hata elfu hamsini sitaki hata kuona kuhusu hicho walichokiita kiinua mgongo ambacho kimeupa umaarufu msamiati ''kikokotozi'' badala ya kuwapa watumishi 50% yao wanayoitaka.

Nione maradi wa bomba la mafuta ala waganda ambalo linasifiwa kuwa ni mafanikio ya awamu yetu huku tukiwa na ''tantalila'' nyingi kuhusu TAZAMA.

Nione tukiuza unga badala ya mahindi kisha turuhusu kuuza mahindi nje ya nchi baada ya wanunuzi kusema hawahitaji unga pekee bali wataka mahindi wayafanyie watakavyo kama vile tutakavyozifanya hela watazotupa.

Nione viwanda vitoavyo ajira lukuki kutoka mikopo isiyo na masharti kutoka Uchina huku tukiona kilichowakuta Zamibia na Kenya juu ya mikopo hiyo isiyo na mashariti.Nisione kuwa China wasichozingatia ni Demokrasia nasi kumbe hatuipendi Demokrasia kama wao.

Nione wahitimu wakiambiwa wajiajiri huku kosi za machinga tuu ni zaidi ya mtaji wake , kweli nitaunga mkono juhudi zenu.
Nione vijana wakiambiwa watoe milioni moja ili wajisajiri kutoa huduma online tv ili wapate faida ya shilingi laki moja, nipeni macho jamani.

Nipeni macho nione wabunge wakiwa mhimili ambao haujachimbiwa na mhimili mwingine chini yake huku nikiona madege yankinufaisha watanzania.

Nipeni macho nione serikali ikibana matumizi huku Chopa zikizunguka huku na kule kila alipo mheshimiwa mpendwa wetu mtetezi wa wanyonge. Nipeni macho jamani nione fedha zikitumika kurudia uchaguzi wa waliojihudhuru kisha kuomba nafasi walioipoteza, nione mafweza yanavyopukutika katika hizo chaguzi.

Nipeni macho nione jinsi Tundu Lissu anavyohangaika kitandani huku Bunge likililia utaratibu waka Mpendwa wetu kwa utu wake kamsamehe Babu Seya aje uraiani badi autumie kushinikiza jeshi la polisi ambalo lipo chini yake kama Amiri jeshi mkuu lifanye uchunguzi walau waliojaribu kumuua kwa zile risasi wapatikane watendewa walau waridhike, kumtibu tumeshindwa hata kuwasaka majambazi hao.

Nipeni macho nione elimu iwe mkombozi badala ya mateso badala ya wahitimu kuishia kwenda kuomba vibarua vya ''saidia fundi'' ili wapate mitaji ambayo nayo yaenda kuishia kwa wakusanya ushuru huku wakiwazibia wale wasio na ujuzi kuzifanya dili hizo.

Nipeni macho nione jamani.

Naendelea kuwaombea wote mnaotupigania ili tusiwe wanyonge daima......
Dtf8xsdXcAo1n_m.jpg
 
Back
Top Bottom