Nipashe!

kakuruvi

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2009
Posts
770
Reaction score
259
Kuna haja wanaotayarisha magazeti wazidi kuwa makini wakati wanapochapisha matoleo yao, leo nimesoma gazeti la NIPASHE lina kichwa cha habari kinachosema ''Majambazi yatikisa Dar ...yapora milioni 150,000/=, bila shaka walitaka kusema milioni 150. Mhariri kuwa macho!!
 
Mkuu,
haya ni matatizo ya kulala na viroba na Valeur kichwani,halafu unakurupukia kazini bila hata kunywa supu ya kongoro.
 

hapo tuseme hesabu ni ngumu au......ndio maana watotot wetu wanaikimbia!
 
Kwa kweli milioni 150000 ni hela nyingi sana, yaani 150,000,000,000/= hata kama fedha yetu imeshuka thamani kupora pesa kama hiyo tena mtaani si rahisi sijui huko Zimbabwe?
 

inawezekana yeye muandishi hivyo alivyoandika anaona ndio sawa, yaani hesabu zimempiga chenga. sifuri ni herufi ya hatari sana inaweza ikakutia hasara kwenye biashara. na ndiyo herufi imekuwa ikitumika hata kuiba pesa kwa maandishi.
 
halafu hawa waandishi mbona wanalipenda sana hili nenon la 'TIKISA'? wanakuza stori kuliko ilivyokuwa utafikiri mji mzima wa Dar umekuwa ukishuhudia tukio hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…