Nionavyo kuhusu muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nionavyo kuhusu muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kitalolo, Jan 7, 2012.

 1. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ikiwa tutauvunja muungano basi kizazi kijacho kitatuona kuwa tulikuwa wabinafsi na wapumbavu na kitaurejesha muungano, kwamfano watu za Tanzania Visiwani watakiona kisiwa chao ni kidogo sana kwa wakati huo haswa ikizingatia pia ongezeko la watu, hivyo basi watatamani kama bara na visiwani ingerudi kuwa moja ili wapate fursa za kujitanua kukabilia na wingi watu na kuwa na fursa zaidi juu ya mambo mbalimbali ikiwamo uongozi kwa wenye uchu wa uongozi kwani kutokana na udogo wa kisiwa na idadi ya watu kupata fursa kama za kiuongozi itawa adimu sana.

  Tatizo litakuja wapi? Ni pale watakaposhindwa kuurejesha muungano huo ambao wengi wao watakuwa wanautamani, kutokana tu na tuliouvunja tuliuvanja kwa misingi na vigezo vya kutokuurejesha tena, na pia ikiwa visiwani wamevamiwa na mataifa yenye uchu wa onyajaji wa rasilimali za mataifa ya africa kutokana na au kupatikana kwa mafuta zanziba, au kutokana tu na jinsi Zanzibar ilivyo kwa sasa yaani wakaitamani tu kwa njisi ilivyo sasa kwamba panaweza pakawekezwa kwaajili ya shughuli za kiutalia na pakawa kama visiwa vingi duniani ambapo zinafanyika shughuli ya utalii, na hivyo mabwanyeye hayo yakaona kwamba kwa kuwapa fursa kwa sehemu hizi mbili kurudi katika muungano basi kuna maslahi yao yataguswa kwa namna yoyote na hivyo basi kupelekea kunyima fursa hiyo ya muungano na ilihali wananchi wanatamani kuwepo kwa muungano na mabwanyenye yanazuia. basi watanzania visiwani watajiona watumwa ndani ya nchi yao wenyewe.

  Kwavile miongoni mwa faida za muungano ni usalama wa mipaka kwa nchi zote mbili, kuwa na nguvu kama za kiuchumi, hivyo basi Tujaribuni kuuenzi na kuudumisha muungano kwa kuondoa kero zote za muungano na hivyo kuuwezesha muungani kudumu na vizazi vijavyo vikauka na ikiwa vitaamua kuuvunja kwa wakati huo basi hiyo itakuwa ni shauri lao, labda pengine kwa wakati huo kutokana na hali ya dunia itakuwa imewalazimu kuuvunja basi na wauvunje lakini si sasa
   
 2. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ninaposoma thread yako unanikumbusha mwanafunzi wa form six kwenye kipindi cha debate. Unachosema tuenzi muungano kwa sababu tukiuvunja kuna siku wazanzinzabari watajiona wamebanana na kukosa fursa za kujitanua kutokana na udogo wa nchi yao. Hakuna popote ulipoonyesha ni kwa nini na kwa faida gani Mtanganyika auenzi muungano. Sana sana anambiwa safari hii ni zamu ya Mzanzinzabari kuwa Rais wa muungano. Sijui ni lini itakuwa zamu ya Mtanganyika kuwa Rais wa Zanzibar. Swala la kurekebisha mapungufu ya muungano limepitwa na wakati. Watanganyika wachodai ni Tanganyika yao.
   
 3. Born Star

  Born Star JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  unajua kila kitu kinasababishwa na uongozi mbovu kwa hiyo wananchi wanakuwa kama wana bahatisha labda muungano ukivunjika maisha yatakuwa yana ahueni kidogo pili kimsingi kabisa tanganyika tumeipa mzigo mzito zanzabar kwa huu muungano na ndio maana tumekuwa tayari jina letu tanganyika kufa zanzabar lipo palepale utakuta mtu anase muungano wa tanzania na zanzabar badala ya tanganyika na zanzibar au miaka 50 ya uhuru wa tanzania haya yote ni makosa tanzania haijawahi kupata uhuru ila imewahi kuungana tanganyika imewahi kupata uhuru na zanzibar vile vile ila kwa wakati tofauti
   
 4. k

  kicha JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 509
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 180
  kwa vile ndo muono wako napenda kuuheshim sana lakini nahisi una upeo finyu zaidi wa kupambanua mambo kwa pande zote mbili badala ya kujivutia kwako.
   
 5. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  asante kwa maoni yako ila kama umenisoma vizuri nimesema tuondoe kasoro zote za muungano , ikiwa miongoni mwa kere ni serekali tatu basi na ziwepo maana madai ya kuvunjika kwa muungani ni kutokana na kasoro zilizopo kuna watu wanamadai ya msingi sana na ikiwa nataona hayatekelezeki wanaona muafaka ni kuuvunja muungano
   
 6. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  ndio maana nikaleta hii mada hapa ili watu wenye upeo mpana kama wewe muweze kutusaidia sisi wenye upeo finyu. hatuwezi kuwa sawa wote. hata pale mbingunu tu waskaji walitofautiana na Mungu ndio chanzohata cha kusema kuna shetani rejea maandiko sembuse huku dunia?
   
 7. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  inaoneka kuna vijimambo flani flani vinavyoleta hizi chokochoko hizo ndizo zinaitwa kero na ziondolewe. kuliko kuwa na muunganio wenye kero ni bora kutokuwa na muungano
   
 8. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Analysis yako ni nzuri sana ndugu yetu lakini hili jukwaa ni la watu wanaopinga kila kitu ambacho hakihusu chadema! Yani kama mada haihusu chadema au ccm( negatively) watakuponda mpaka unajishangaa mwenyewe. Kiukweli ni kuwa uroho wa madaraka ndo unasababisha wanzazibari wajitenge, na wakisha jitenga hio dhambi itawatafuna wenyewe kwa wenyewe na baada ya miongo kadhaa wataomba muungano tena. Viongozi wetu ni waroho kuanzia rasilimali mpaka madaraka......
   
 9. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,399
  Likes Received: 1,524
  Trophy Points: 280
  .........Kero kubwa kuliko zote ni kurejeshewa Tanganyika yetu, ili na watanganyika siku moja tuseme naam, ni zamu yetu kutoa rais wa Zanzibar, vinginevyo uvunjike ili wakabane makoo wao kwa wao kwamba hii ni zamu ya Wa-unguja na ile ya wa-pemba;
   
 10. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Umenena! Ni vizuri wazanzibari waelewe Watanganyika wanachotaka ni Tanganyika
  Kujidanganya kuwa Watanganyika wanakubali mustakhabali wa nchi yao uwe mikononi mwa Wazanzibari ni wazo lilopitwa na wakati. Njelu Kasaka na kundi lako la G55 mko wapi?
   
 11. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  watu wengine tunasonga mbele ninyi mnarudi nyuma? kwa hali hii usitegemee Africa kuja kuungana hata siku moja. Vinchi viwili vimeungana lakini maneno kila siku... tanganyika tanganyika! cha muhimu ni katiba tu ambayo itatusaidiA KUONGOZA NCHI YETU VIZURI. LAKINI UROHO WENU NA WIVU WENU WA MADARAKA NDO SUMU INAYOWASUMBUA KILA SIKU HUMU.VIONGOZI WETU NDO WANA UCHU KWELI NA RASILIMALI ZETU NA WANAOMBA KILA SIKU MUUNGANO UVUNJIKE ILI WAFAIDIKE VIZURI. TUJENGE NCHI YETU SISI NI WAMOJA NA TUSIIBOMOE. ILA HUMU JF KUNA WADINI WENGI AMBAO HAWAPENDI KUONA WANZAZIBARI WAKIENDELEA AU WATANGANYIKA WAKIENDELEA.
   
 12. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #12
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  na wakishindwa kukabana makoo wataamua kujitenga kuwepo na raisi wa waunguja na raisi wa wapemba, tumeona mifano hiyo kwenye visiwa mbalimbali vinataka kujitenga vijitegemee ili tu kuweza kupata madaraka ya uraisi
   
 13. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Sijaona ulichokiandika hapa mtoa mada, katika mazoba we kilanja wao!
   
 14. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  wazanzibari na Watanganyika wanajuwa vilivyo nini wanataka. Na kama Muungano ni kitu muhimu hivyo basi tusiwe wagumu kufanya Federation itakayowapa Wakenya, Waganda ,Waburungdi na Warwanda acceess ya ardhi ya Tanganyika
   
 15. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  sijakupata vizuri ndugu
   
 16. T

  Topical JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Muungano unahitajika isipokuwa mfumo wa muungano ni mbovu kabisa

  1. Tunataka mfumo wa serikali tatu

  Serikali ya Tanganyika yenye makao yake makuu Dodoma, Serikali ya Zanzibar makao makuu unguja na serikali Tanzania (muungano) makao yake makuu Dar es Salaam..

  2. Tutaka kuvichambua mambo ya muungano

  Katika muungano huu mambo mengi yameongezwe kinyemela bila ridhaa ya wananchi wa nchi hizi mbili, uwepo utaratibu wa kura kwa kila jambo la muungano linapotakiwa kuwekwa ndani ya muungano ili watu waridhie tusiwe na kulazimishana..
   
Loading...