Ninunue gari lipi kati ya Rav 4 vs Vanguard?

Jul 29, 2018
96
237
Naombeni Msaada wenu wadau,

Nataka kununua Gari mojawapo kati ya hizi mbili RAV4 na Vanguard ya mwaka 2010. Kwa mtazamo wangu naona kama haya magari yamefanana kwa kila kitu, sasa basi mwenye kuyafahamu vizuri haya Magari naomba anichagulie nichukue lipi

Asanteni.

Capture-00036-750x469.jpg

MAONI KUTOKA KWA WADAU
Kwa uelewa wangu, Vanguard na RAV4 ni gari lile lile. Tofuati kubwa kati ya hayo magari mwili ni kitu wanaita wheelbase, na majina tu. Vanguard ni long wheel base ya RAV4. RAV4 ilikuwa ikilalamikiwa saana US kwa engine ndogo na ukosefu wa third row seat (uwezo wa kubeba watu 7). So kwenye third generation, yaani model ya kuanzia 2006 Toyota wakatengeneza RAV4 ya kawaida ya engine ya cylinder 4, na hiyo ndefu ambayo kwa US ilikuwa na cylinder 6.

Sasa kwa Japan nafikiri na baadhi ya masoko, hiyo RAV4 ya long wheelbase ilibadilishwa jina na kuitwa Vanguard, sababu ile short wheelbase ilipendwa saana Japan, so wakaamua waichae iendelee sokoni, ila wanaotaka long wheelbase wakapewa Vanguard. Ni kweli Vanguard ilikuwa na features baadhi ambazo hazikuwa kwenye RAV4 ukizingatia ilianza kutengenezwa miaka miwili baada ya 2nd gen RAV, ila ni chache saana, nyingi zinafana. Kasoro mbele tu, hasa kwenye bumper na nyingine zinakuja na CVT. Vingine vinafanana.

Kingine kikubwa kilichokuwa introduced kwenye Vanguard, na baadhi ya RAV4, nafikiri ya mwaka 2009 ni kitu wanaita Run Flat Tyre (RFT) ili kuweza kupata nafasi ya kuweka third row seat. Hili ni tairi ambalo haliishiwi upepo hapo hapo linapopata pancha. Kiuhalisia, upepo unaisha, ila walichofanya ni kuweka kuta ngumu za pembeni za tairi hizo kiasi kwamba hata likipata pancha tairi halibonyei kwa umbali kadhaa mpaka utakapofika kwenye sehemu ya kuzibia pancha. Ndio maana Vanguard nyingi hazina spare tyre kwa nyuma kama RAV4 (Ni chache saana nimeona zina spare tyire). Mara nyingi unakuta zina vifaa vya kuzibia pancha, na ki mini compressor cha kujaza upepo.

Hizo RFT kwa kweli huwa sizipendi, as zinafanya gari inakuwa uncomfortable. Na sijui kama zinapatikana huku kwetu. So inamaana tairi zinazokuja na gari zikiisha, inabidi uanze kubeba spare tyre kwenye boot ambayo inachukua nafasi ya mizigo, sababu Vanguard inayokuja na RFT haina sehemu ya kuwekea spare tyre.
.
 
Prince Kamugisha,

Mimi naomba nikupe ushauri wa kitaalamu, iliuweze kufanya maamuzi mwenyewe

Toyota Vanguard ime base sana kwenye model ya Toyota yenye long wheelbase, yaani hilux surf!

Vanguard hujulikana kwa kuwa sawa na version model zote za hilux surf. Hii gari (Vanguard) ni gari yenye uwezo mkubwa na inaweza kubeba hadi abiria saba.

Na ina vitu vingi vizuri vya nyongeza vinvyomfanya mtumiaji azidi kuipenda haswa kwenye maambo ya usalama ambayo ni S-VSC (Steering ASSISTED VEHICLE STABILITY CONTTOL SYSTEM) Ambayo humsaidia abiria kubaki salama ndani ya gari iwapo kwa namna yeyote ike, dereva atapoteza control (kutokea ajari)

TUKIANGALIA UPANDE WA EQUIPMENT
Tumeona kuwa vanguard ina S-VSC yaani ( Stability steering assisted vehicle stability control system )
Intelligsnt system, torque distribution , enhanced drive system , na brske system ya suv!
Wakati equipment za rav4 ni
Color-keyed rear spoiler, halogen projector-beam headlight, Automatic Limited-slip differential, roof mounted shark-fin antenna na rear window defogger with timer.

TUANGALIE ENGINE
Gari zote mbili (Rav4 na Vanguard) zote ni hua zinamfumo wa 4WD na 2WD , zote zikiwa zinamfumo wa gear ya automatic sambamba na engine yenye 2AZ-FE DOHC four cylinders na 16 valves. Yenye ukubwa wa 2,400 Cubic Centimeters (CC)
Gari zote (Vanguard na Rav4) Engine zake ni mbele, pamoja na front wheel drive. na 4WD
Wakati huo huo, powertrain ya rav4 ni 2.0 liters engine yenye manual gear 5, au 4WD yenye auto!

UTUMIAJI WA MAFUTA
Consumption ya rav4 ni karibia 30 MPG wakati vanguard ni 28 mpg!
 
Na mimi ninahamu ya kujua hili hasa kwenye uimara. Lipi linaweza kuhimili mikiki zaidi ya lingine.
 
Kama unapenda vitu vipya chukua Vangurd, kama OLD is still Gold chukua Rav 4 otherwise Vanguard ni modified RAV4
 
Kwa uelewa wangu, Vanguard na RAV4 ni gari lile lile. Tofuati kubwa kati ya hayo magari mwili ni kitu wanaita wheelbase, na majina tu. Vanguard ni long wheel base ya RAV4. RAV4 ilikuwa ikilalamikiwa saana US kwa engine ndogo na ukosefu wa third row seat (uwezo wa kubeba watu 7). So kwenye third generation, yaani model ya kuanzia 2006 Toyota wakatengeneza RAV4 ya kawaida ya engine ya cylinder 4, na hiyo ndefu ambayo kwa US ilikuwa na cylinder 6.

Sasa kwa Japan nafikiri na baadhi ya masoko, hiyo RAV4 ya long wheelbase ilibadilishwa jina na kuitwa Vanguard, sababu ile short wheelbase ilipendwa saana Japan, so wakaamua waichae iendelee sokoni, ila wanaotaka long wheelbase wakapewa Vanguard. Ni kweli Vanguard ilikuwa na features baadhi ambazo hazikuwa kwenye RAV4 ukizingatia ilianza kutengenezwa miaka miwili baada ya 2nd gen RAV, ila ni chache saana, nyingi zinafana. Kasoro mbele tu, hasa kwenye bumper na nyingine zinakuja na CVT. Vingine vinafanana.

Kingine kikubwa kilichokuwa introduced kwenye Vanguard, na baadhi ya RAV4, nafikiri ya mwaka 2009 ni kitu wanaita Run Flat Tyre (RFT) ili kuweza kupata nafasi ya kuweka third row seat. Hili ni tairi ambalo haliishiwi upepo hapo hapo linapopata pancha. Kiuhalisia, upepo unaisha, ila walichofanya ni kuweka kuta ngumu za pembeni za tairi hizo kiasi kwamba hata likipata pancha tairi halibonyei kwa umbali kadhaa mpaka utakapofika kwenye sehemu ya kuzibia pancha. Ndio maana Vanguard nyingi hazina spare tyre kwa nyuma kama RAV4 (Ni chache saana nimeona zina spare tyire). Mara nyingi unakuta zina vifaa vya kuzibia pancha, na ki mini compressor cha kujaza upepo.

Hizo RFT kwa kweli huwa sizipendi, as zinafanya gari inakuwa uncomfortable. Na sijui kama zinapatikana huku kwetu. So inamaana tairi zinazokuja na gari zikiisha, inabidi uanze kubeba spare tyre kwenye boot ambayo inachukua nafasi ya mizigo, sababu Vanguard inayokuja na RFT haina sehemu ya kuwekea spare tyre.
.
 
Kwa magari ya kijapan unaweza kukuta engine za magari yote hayo zinafanana utofauti ni body kwahiyo ni wewe kuangalia body ipi inakuvutia,mfano,Toyota Harrie na Ipsum zinazotumia engine ya 2AZ-FE ,Toyota Landcruiser Prado zinazotumia engine ya 2AZ-FE ,Toyota Landcruiser Prado na mode zipo zinazotumia engine ya 3RZ-FE..

r
1540455563015.jpeg
th
zipo
1540455670617.jpeg
l
th
 
Hapo kwenye upande wa spare tyre nimeona pale Shaurimoyo wakibadili mlango OG ulokuja na Vanguard wakifunga mlango wa Rav4 wenye spare tyre holder. Siku zote wabongo ni watu wa short cuts
Inawezekana kabisa. Bonge la shortcut hilo. Duu.
 
MAGARI7
Nimepitia maelezo yako, ila sijaelewa kwa nini umeifananisha Vanguard na Hilux Surf. Hizo gari ni platform mbili tofauti kabisa. Surf ilikuwa unashare platform na Land Cruiser Prado ile ya mwanzo, ila sio Vanguard. Surf ni very capable off road kulinganisha na Vanguard maana ile ni body on frame kwamba ina chassis kabisa wakati Vanguard ni unibody. Hata engine zinapishana kabisa. Na Surf ujue ina 4WD sio AWD ya kwenye Vanguard. Hebu angalia vizuri.
 
MAGARI7,
Mkuu umetoa wapi ulinganisho wa Vanguard na Hilux Surf? Surf na Vanguard havina ufanano wowote ule Vanguard ni Rav 4 sema Vanguard yenyewe haina spare tairi tu maana hata Chasis inayotumila ni sawa sawa na ya Rav 4
 
RugambwaYT,
Hata mimi nimeshangaa kabisa maana ukizisimamisha pamoja Surf na Vanguard unaona kabisa hizi ni gari mbili tofauti engine ya kwenye Surf ni 2.7L, 3.0L, 3.4L na 4.0L wakati vanguard ni 2.4L na 3.0L na 3.5L
 
Yes, Vanguard ni long wheelbase ya Rav4. Kwenye masoko ya Ulaya na Marekani Rav4 za 3rd generation zinalingana na Vanguard. Ila Surf ni level nyingine kabisa.
 
Back
Top Bottom