Iko hivi, na nadhani wengi hawajui, ila ujuzi huu utaupata kwenye nondo za zamani, speed ya processor ni combination ya processor yenyewe na front bus ya mother board, kiufundi processor ya 2 GHz ili uipate speed hiyo ni lazima clock speed za motherboard ikiwemo front bus, pci bus, na memory ziwiane, hivyo sio kila processor itafanya kazi na kila mobo, despite the interface.
RAM ni eneo amabapo data na program zinakia loaded wakati zinafanyiwa kazi, operating system yenyewe unapakiwa humo inapowasha pc yako, hizi ram pamoja na uwezo wake kwa maana ya capacity mfano 1gb,pia zina speed tofauti, na ziko ambazo ni static mwa maana hazifuti baadhi ya data ukizima mashine na ziko ambazo ni volatile zinafuta ukizima mashine hivyo kila kitu lazoma kipakiwe upya kila unapowasha.
Ni muhimu kufahamu speed ya ram kama pia inaendana na motherboard na process pia ili upate good performance.
Kuna virtual memory au virtual ram sometimes inaitwa paging, hii ni sehemu ya hard disk inayotumiwa na operating system kama ram. Kwenye window os by default hii vm hiandaliwa kwa kuchukua kiasi cha physical ram iliyopachikwa kwenye motherboard zidisha kwa 1.5 mfano kama ram ni 1gb zidisha 1.5 utapata hiyo vm ni 1.5g lakini unaweza ongeza manually.
Kwa ujumla kasi ya compyuta inategemea vitu vingi sana, kabla processor haijachungulia kwenye ram ili ianze kuchakata mambo kwanza inangaalia level 1 cache, hii huwa ndogo na hiwa karibu na processor na siku hizi wanaijumuisha kwenye processor yenyewe kabisa, kula level2 cache, na kama iko level 3 nayo itaaangaliwa then ndio unakwenda kwenye ram, then inakwenda kwenye hard disk,
Vyote hivi vinapaswa kuwa katika ubora fulani, so unaweza kuwa na ptocessor nzuri tu na ram ya kutosha lakini hard drive ikawa slow na uk experience slowness..
Kuna mengi ya kujifunza hapa.