Nini Taswira ya Dua/Sala ya kuliombea Bunge

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,789
Kila siki asubuhi kabla shughuli za Bunge kuanza, Spika analiongoza Bunge katika Dua/ Sala maalum la kuliombea Bunge kwa Mwenyenzi Mungu alioumba mbingu na dunia (ardhi) ili awape busara na hekima katika kutekeleza majukumu yao.

Lakini cha kustaajabisha kinachoendelea kuanzia hapo, ni kinyume kabisa na dua ilioombwa. Busara na hekima zinatoweka. Maamuzi makali yasokuwa na hekima na busara ndio yanatamalaki.Hali inayotoa taswira kinyume na matarajio na hali isiyopendeza kwa Bunge letu Tukufu.

Tafsiri yake ni kwamba ima Mwenyeenzi Mungu amewasusa waja wake kutokana na kuusoma uaminifu na imani zao kuwa daifu au sala zao kuonekana kama dhihaka kwa mola wao aliowaoumba.

Kwa kuhofia kunakamishwa sote nashauri dua/sala ya asubuhi iondoshwe na badala yake usomwe/uimbwe wimbo wa Taifa letu
 
Back
Top Bottom