Nini Tamko la Bakwata katika kadhia hii?

Barubaru

JF-Expert Member
Apr 6, 2009
7,161
2,323
Tokea itokee kadhia ya Kudhalilishwa Qur'an na kupelekea kuchomwa na kuharibiwa kwa kamanisa na misikiti huko Mbagala , Tz. Kumekuwa na matamko mbali mbali yaliokuwa yanatolewa na Viongozi mbalimbali wa taasisi na madh'hebu mbalimbali za dini tofauti.

Mpaka sasa tumesikia Tamko la Sheikh Ponda na jumuiya inayoiongoza, Tumesikia Tamko la NCCR mageuzi, Tamko la Anglican, na Tamko la KKKT.

Napenda kuuliza je vipi mbona hatujasikia Tamko la Sheikh Mkuu wa Bakwata? au yeye alimgusi hilo.

Nawasilisha.

maa salaam
 
Bakwata haitakiwi na waisilamu kwasababu hawana mchango wowote.Kawaida wanatakiwa kuwa mstari wa mbele wa kuwatuliza waisilamu na vilevile kuungana na wengine kwa kutuliza hali ya hasira kutoka kwa wananchi.Ni matukio makubwa yaliyotokea hivo ilitakiwa waache kazi zao na kufuatilia haya pamoja na kukaa pamoja na viongozi wa makanisa ili watengeneze utulivu.Wanalipwa mishahara ya bure lakini hawajibiki ipasavo.Inabidi na wao waonyeshe mchango wao ktk kuweka amani ktk nchi.
 
Wakristo ni wavumilivu sana, Waislamu ni wavumilivu sana japo kuna baadhi ya wahuni na washenzi wanaotaka kutumia mgongo wa uislamu kutaka kuivuruga amani na mshikamano wa watanzania
 
Mkuu, hukumuona na kumsikia Sheikh Mkuu wa Mkoa (BAKWATA) wa DSM wakiwa pamoja na Kamanda Kova, Gavana wa DSM wakitoa matamko yao kupinga vurugu hizi?
Kova, RC, Sheikh wa Mkoa, wanena
Kutokana na vurugu hizo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, walikutana na kuzungumzia tukio hilo.

Katika mazungumzo yao yaliyokuwa yakirushwa moja kwa moja na kituo cha Television cha ITV, walikemea kwa nyakati tofauti vurugu hizo. soma zaidi source: Waislamu wavunja makanisa Dar es Salaam
 
Mimi naona hivi sasa ni WAKTI muafaka kabisa Serikali ya JMTz kutambua kuwa wakala wake kwa waislam BAKWATA hana mvuto wala ushawishi wowote kwa waislam wa Bara.

Sasa kinachotakiwa kifanywe na Serikali hiyo kuacha kabisa mas'ala ya waislam yaendeshwe na kuratibiwa na waislamu wenyewe na kuwataka waunde chombo chao kikuu ambacho ndio utakuwa mkusanyika wa taasisi hizo na kutoa tamko kwa ajili ya waislam..
 
Tamko umeshaoneshwa hapo posti namba 4, sema wee unataka kulisikia kwa namna unavyotaka wewe.
 
Kikwete kuwa jasiri vunja bakwata
Kama nyerere alivunja jumuia iliyo kuwepo kwasababu za usalama basi vunja Bakwata kwa maslahi ya usalama
Hawa ni kundi la ama genge la majizi wao hawafanyi lolote lakin wanauza mali za waislam walizopewa kama trstees
Hizi mali si za Mussa Hadi au Issa Simba
Kwa heshma kubwa livunje na uunde kamai huru ya waislam kazi yao kuhakiki mali za waislam kuunda katiba mpya itayoshirikisha madhehebu yote na uchagui ufanywe kutafuta viongozi wapya
Hili dude Bakwata ni dubwana mzigo
Utakuwa umesaidia sana kutuliza haua makelele yasio isha

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Subiri wapewe kitu kidogo, utawasikia tu. Wameshajua hapa kuna hela!
 
Mimi naona hivi sasa ni WAKTI muafaka kabisa Serikali ya JMTz kutambua kuwa wakala wake kwa waislam BAKWATA hana mvuto wala ushawishi wowote kwa waislam wa Bara.

Sasa kinachotakiwa kifanywe na Serikali hiyo kuacha kabisa mas'ala ya waislam yaendeshwe na kuratibiwa na waislamu wenyewe na kuwataka waunde chombo chao kikuu ambacho ndio utakuwa mkusanyika wa taasisi hizo na kutoa tamko kwa ajili ya waislam..

Hivi nikweli BAKWATA wanabebwa/wanalipywa na serikari?
 
Bakwata ni CCM (C) ,wanasubiri wapewe maelekezo na ccm ili watoe tamko, ingekuwa chadema wamefanya hivi ungewasikia na upuuzi wao,siku zinavyokwenda ndivyo waislamu wengi wanaichukia bakwata
 
Wakristo ni wavumilivu sana, Waislamu ni wavumilivu sana japo kuna baadhi ya wahuni na washenzi wanaotaka kutumia mgongo wa uislamu kutaka kuivuruga amani na mshikamano wa watanzania

Minyukano ya ndani kwa ndani ndo inayo wasumbua hawa jamaa. Nafikiri hata leo hii Mufti akisimama na kusema kitu, nina mashaka kama atapata mwitikio unaostahili mtu wa cheo chake! Kwa hiyo suala la uvumilivu wa waislamu siuoni mahali popote! Kinachoonekana ni uasi ndani ya kambi yao wenyewe!
 
Back
Top Bottom