mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,767
- 7,115
Wana jamvi,
WaTanzania wamekuwa na msemo wa kula mlo mmoja chini ya dola 1, hili limebadilika sana, kwa hivi sasa hatujui katika bajeti hii wanayoita tukufu watanzania wanaishi chini ya dola ngapi? kwa siku?
Bado kuna kitendawili cha kujua hawa mawaziri watatu wa wizara ya fedha wanavyotuletea bajeti ya mtanzania kuishi kwa milo mingapi kwa siku au nusu mlo, hapo tutegemee watoto kuendelea kudumaa kwa makande na ndimu, kwa bajeti hii tunategemea kuona watanzania kukondeana kama wasomalia walioko kwenye vita.
Mpaka sasa Tanzania sio salama kabisa, licha ya kuongezeka kwa dola kutoka 1600 mwaka jana na kufikia leo 2350 bado maharage na mahindi yazidi kuwa juu.
Bado tunagoja tarehe 1 July Siku ya mateso kwa watanzania kila mwaka kwani ndiko kila kitu kinakuwa bei juu, hii inatakiwa iwe tarehe ya uzuni tanzania kwani siku hiyo mlala hoi uwa anadumazwa kwa kunyofolewa kila sehemu matajiri waliolimbikiza mali wananeemeka.
Haya bwana nyie mawaziri watatu mnataka Mwenye nchi aliyepo magogoni aage vibaya kwa kuacha kila kitu kinapanda , ukiuliza kisa mafuta, mafuta ya taa yanafanywa dili wakati mjini hawatumii tena.