Travelogue_tz
JF-Expert Member
- Sep 28, 2010
- 855
- 1,224
Habari wanabodi.
Binafsi, na pengine kwa baadhi yenu mtakuwa mmeshtushwa Au kushangazwa na madai ya Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Taifa kwamba JPM alitaka kuhongwa na Wahujumu Uchumi kwa lengo la kukwepa taarifa ya mchanga wa Dhahabu ( Copper Concentrate). Bila shaka inaweza kuwa lengo la mwenezi ni kujenga taswira kwa umma juu ya Uzalendo JPM na hivyo kuondoa Mashaka Kwa Umma. Lakini pia taarifa yake inaweza kuwa na lengo la kuhukumu watuhumiwa wa Acacia, na washiriki wao kwamba kuna ukweli katika matokeo ya kamati ya Rais, chini ya Prof. Mruma, ndio sababu Wahujumu hao walihangaika kujinasua na kashfa husika. Hili la Polepole sio geni sana katika ulimwengu wa propaganda za kizalendo, katika nyakati fulani Viongozi wa ki Communist wa China waliwahi kuendesha propaganda hizi, tena Kwa kuwataja watu waliotaka kuwahonga katika nyadhifa mbalimbali ili kujijengea heshima kwa jamii yake. Ikumbukwe pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Vita yake ya Shisha aliwahi kudai kuwa kuna watu walimpelekea rushwa ili anyamazie vita hiyo.
Prof. Sospeter Muhongo aliwahi kutoa madai ya kamati ya Bunge kuhongwa, na kupelekea kamati husika kuvunjwa.
Tafsiri pana ya hili ni kwamba kwa takribani miaka 17 imepita, Wawekezaji hawa wamekuwa wakifanya kazi zao kwa ulinzi makini kutoka Serikali za CCM. Ulinzi huu umeanzia katika Sheria za Nchi, Mikataba, Sheria za Kimataifa na taratibu ambapo zote hizi tumeridhia au kutunga wenyewe chini ya utawala wa CCM,na zaidi kupiga na kuua raia kwa kigezo cha kulinda Uwekezaji. Pia, Polepole anafahamu vizuri kwamba katika kila hoja, kuna nadharia kinzani, kwa uelewa wa wengi Rais wa Nchi ndie Mwenyekiti wa CCM, Ndie amiri Jeshi Mkuu, Mwenyekiti wa Baraza LA Mawaziri, Mwenyekiti wa Baraza LA Usalama LA Taifa. Hivyo basi Mwinyi, Mkapa, Kikwete wote hawa wamekuwa na nguvu za kisheria kwa mujibu wa katiba. Kutokana na hili, Polepole anataka kutuaminisha kwamba Mkapa, Kikwete, Wabunge wa CCM, pengine Baraza LA Mawaziri (JPM inclusive) katika nyakati fulani waliwahi kuhongwa na ndio sababu ya kunyamazia usafirishaji wa mchanga nje ya Nchi. Kwamba Wabunge wa CCM walikuwa wamehongwa na wawekezaji ili kupitisha Sheria zinazowapa / kuhalalisha Wezi hawa ambao sasa Polepole na CCM wenzake wanawaona wabaya. Ni vema sasa Polepole, kwa kuwa amekiri hilo ni muhimu kuomba msamaha kwa Taifa.