Nini tafsiri ya madai ya Polepole, kwamba John Pombe Magufuli alitaka kuhongwa na Wahujumu Uchumi?

Threesixteen Himself

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
8,210
2,000
!
!
Bila kutafakari amejikuta karopoka... Tafsiri ya harakahaka ni kwamba the system was corrupt, it corrupt and it will be corrupt bila Magu. Lakini pia Tafsiri nyingine ni kwamba kuna watu wapo juu ya sheria na wataweza fanya lolote na wasifanywe lolote. Kujaribu Kumhonga askari ni kosa kisheria, nadhani pia na rais
 

Msororo69

JF-Expert Member
Feb 27, 2016
2,728
2,000
Ndio maana nimekuuliza kwa fikra zako alichokifanya Mkapa kilikuwa sahihi simply because ya kuvutia investors. Sasa kwa nini mnatupigia kelele za Kuibiwa? Yaani mlango mmeacha wazi kwa kigezo cha kuvutia wageni halafu mnaanza kupiga kelele za Wezi? CCM imepitisha Sheria ya madini kwa hati ya dharura in favour of investors, mlikuwa mmehongwa? Mikataba bado ni siri, mmehongwa?
Matatizo yote tunayoyashughulikia mengi hayahusiani na sheria wala mikataba bali ni kutokuwajibika kwa watendaji wetu kama wenye mali.
Huwezi kuhongwa na mtu unayemuhitaji kwa hamu na ghamu tumia akili. Labda nikupe mfano ambao akili yako imelalia. Chukuwa mfano kuna msichana unayemshawishi uwe naye halafu unategemea akuhonge ili uwe naye. Ni wazi hutafanikiwa. Ndivyo ilvyokuwa kwa Mkapa. Utawala wake ulikuwa unawashawishi wawekezaji kwa vyovyote vile haikuwa rahisi kwa anayebembelezwa kuja akuhonge unayembembeleza. Dangote kwa kuwa sasa hivi anabembelezwa hakuhonga kupewa kitalu ndani ya siku tatu. Mazingira kama hayo ndiyo alikuwa nayo Mkapa. Tumia akili basi kufikiri.
 

Kadhi Mkuu 1

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
10,082
2,000
Ni sawa na kusema majenshi yote yameenda rogue maana yameshindwa kumkamata huyo mtoa rushwa. Raisi ana TISS pale pale magogoni maana msimamizi wake ni waziri wa ofisi ya raisi, ana mkuu wa majeshi, ana mkuu wa polisi, magereza, uhamiaji, ffu,halafu anashindwa kuwakamata hao watu au walimjia kwa njia ya upepo nini?
Mkuu Drama za CCM hazikuanza leo. Wakati wa EPA tuliambiwa bilioni 40 zilirejeshwa na watu wasiojulikana. Maana yake wafanyakazi wa mabenki waliokota mabilioni milangoni na askari walinzi hawakujuwa nani kayaweka ila serikali ikayaagiza mabenki yapokee hizo pesa maana ni za EPA. Kwa hawa waliobeba bilioni 300 wakampelekea Mh Rais bila kuonekana na akayakataa ni kweli maana haya maajabu siyo mara ya kwanza kutokea TZ.
 

Mgango

JF-Expert Member
Oct 27, 2016
2,344
2,000
Tafsiri ni kuwa siku wakipokea hongo hawaji kututangazia kwenye vyombo ya habari.
Kitendo cha msemaji mkuu wa CCM kuropoka tuhuma kubwa kama hizo bila ushahdi concrete na angalau kuweka wazi solid proof ni jambo la ajabu sana.
Inaonesha ni jinsi gani tunaongozwa na watu wasiopenda kujiridhisha na kuwa thorough.
Mpaka atakaporudi Bwana Yesu hapatatokea kiongozi mwadilifu hata mmoja. Hicho chama kimeoza kabisa. Hata wafanye je, waseme je.
 

Mgango

JF-Expert Member
Oct 27, 2016
2,344
2,000
Huyo msemaji wao ni muongo sana unless a tuambie huyo aliyetaka kutoa hizo pesa ni miongoni mwao au ni mstaafu ambaye jina lake likitajwa chama kitaumbuka
 

Mgango

JF-Expert Member
Oct 27, 2016
2,344
2,000
Labda anamaanisha Prof Muhongo ndo maana kaondolewa madarakani. Otherwise ni wenyewe kwa wenyewe. Lakini hata hivyo huyo mtoto ni muongo sana na wala hayaishi yale ayanenayo
 

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,394
2,000
Sasa
Matokeo ya report ile hayakutokana na kupiga ramuli kama wafanyavyo waganga wa kienyeji.Vile vile Kamati ile haikujifungia chumbani na kuanza kufanya maombi kama wafanyavyo vikundi vya kidini vya "mwendokasi" ili ijulishwe na kuonyeshwa mule ndani ya Makontena kuna nini na kwa kiasi gani.Walichukua sampuli na kuelekea maabara.Kupinga matokeo ya Maabara ni kutaka kutuambia kuwa wewe ukiuguaga na kwenda hospitali huwa hukubali matokeo ya maabara yanayoonyesha kuwa uling'atwa na mbu siku kadhaa zilizopita walipokuwa wanatafuta damu ya kustawisha mayai tumboni mwao na hivi umeambukizwa vijududu vya Malaria.
Sasa padre hivi hujawahi kwenda hosp kupima ukaambiwa huna malaria, lakini kutokana na dalili unazojisikia ukaamua kwenda hosp nyingine kuhakikisha kama ni kweli huna malaria, na unakuta una malaria. Kuna hosp na hosp na pia kuna maabara na maabara! Matokea ya uchunguzi yanadefy common sense na hata logic! Pamoja ba yote hayo tuendelee tu kuiamini ripoti!?
 

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
6,550
2,000
Mwenyekiti kwa heshima na taadhima mfukuze kazi huyo polepole hakufai na hakifai chama.
Yawezekanaje idara ya habari ikulu ikose taarifa hizi yeye pole×2 azipate? Au Lumumba ndio kituo cha kuchukulia rushwa? Tuambizane ukweli hapa, ni kwanini hawakukamatwa hao watu ambao tayari walikuwa na nia ya kuvunja sheria?
Au tiss ilipata ganzi tena Kama ile ya escrow?
Hapa hampenyi hivihivi ni lazima msemaji Wa magogoni aje na taarifa sahihi ya nini kilitokea na hatua zilizochukuliwa vinginevyo piga chini wakuu Wa idara zote za ulinzi na usalama kwa kushindwa kazi.
Kama no propaganda za ccm basis zipo too low kuliko betri ya kisimu changu cha tochi.
Hamtudanganyi kijinga tena.
 

Angry Bird

JF-Expert Member
May 3, 2016
514
500
Najiuliza hapa, kama ni kweli kwa nini JPM hakuchukua hizo fedha? 300B? Raisi asiyeogopeshwa na lolote na aliye tayari kwa chochote angezichukua azitangaze wazi wazi alipie vile vi terrible teens huku mhongaji achukuliwe hatua. Afterall ni pesa zetu wametuibia. Mimi tu nawaza hapa au labda ninaota.
 

Kimweri

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
4,001
2,000
Sijawahi kusema popote kuwa nchi hii imewahi kuongozwa na watu wengine nje ya CCM.Ninapo-address Lema na CDM siwatizami kama watu pekee maadui Wa CCM bali watu wenye mtizamo tofauti na wale wanaounga mkono hatua zilizopendekezwa na Kamati iliyochunguza Makanikia.Hata wana-CCM wapo wanaopingana na suala hili.Kwa mantiki ya kawaida ukipikiwa chakula kibovu jambo la kwanza ni kuhakikisha unapata mbadala wa chakula ili usife njaa.Huwezi kuendelea kutumia nguvu ulizo nazo ku-blame na kuuliza uliza tu kilichotokea.Fanya fingerpointing baada ya kuwa umekula.Kuhusu mimi kuwa na mawazo ya Ki-CCM nadhani fanya utafiti kidogo.Wanaonijua akina Mnyika, Mdee, Kafulila, Reg, Mbowe wnafahamu vizuri tabia yangu.Hata katika CCM wako watu kama mhe.Mkasa wanafahamu mimi niko zaidi ya kulalamika tu bila kupendekeza suluhisho chanya.


I do not qualify or respond to your comments based on who you know. I write back based on what you know and white you write. Kama kuna walakini i will address that as that.

Kuwavua CCM lawama za ujinga walioufanya kwa miaka nenda rudi ni kuwapa mashada ya maua wasiyostahili.
Rule number one of progress is accepting responsibiliyt NOT deflecting it. CCM is simply deflecting its entire responsibilities in putting the country in this mess. Then, it wants the entire country to mourn on its behalf. Thats shaddy.

Mfano wa mpishi aliyepika chakula kibichi, wanafki watakula chakula kibichi. MIMI sio MNAFKI. sihitaji kumjua mbowe, mdee or anyone to call a spade a spade.

Way forward zimeshapendekezwa na wengi, lakini selective amnesia ya CCM imesababisha kukosekana kwa suluhisho.

WEKA MIKATABA WAZI, HAKIKISHA MIKATABA YOTE INAJADILIWA NA BUNGE KWA UWAZI.

wamefanyeje?wameendelea kuficha mikataba na wanaendelea kusaini mikataba mipya (refer mkataba wa bomba la mafuta wa juzi na wa boeing) juu ya sheria zetu mbovu, halafu wakiboronga wanataka tuje hapa kuwalilia. COUNT ME out of huo unafki.
 

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
6,550
2,000
Ni kutujlisha ukweli wa mambo na pia hao... wafahamu nini kimo kwa Awamu ya tano hii...yaani hapokei hongo eeeeeh

Hapa kazi tu

Magufuli 2020
acha kutuongopea. Tuthibitie kama hajawahi kupokea rushwa tangu azaliwe. Na kwani aseme polepole na siyo msigwa? Au ilipitia Lumumba ikapigwa panga?
Mwenye kumjua mtoaji aniletee mimi nitampelekea na kwa ushahidi sijawahi kumhonga MTU akaikataa hongo yangu. Njooni nayo nitampelekea mnayetaka aipokee!
 

ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,412
2,000
Ni kweli Pole pole aliombe taifa msamaha kwa kutoa kauli kama hiyo, pia naomba kukuuliza polepole hao watu waliotaka kutoa rushwa ni akina nani? Wewe ulipataje taarifa hizi na alikuambia nani,?? Je hao watu wamechukuliwa hatua gan za kisheria? ? Kwani kutoa na kupokea rushwa ni kosa sasa hatua zipi zimechukuliwa dhidi yao? ?
Na kushawishi pia ni kosa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom