Nini tafsiri ya kile kinachoendelea Afrika kusini

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,200
56,826
Nikama vile naona mapichapicha yasiyoeleweka!,lkn hii ni dhahiri kuwa Hawa wenzetu wamegeuka mbogo!.kwanza ni Jambo linaloumiza kwani hata Kama ni kufukuzwa si kwa namna hiyo ya kuchomana na kurushiana mawe!
Hii si ile Afrika ya enzi za kina nyerere hasa wakati ule wa kupigania Uhuru ambapo adui yetu alikuwa mmoja!,ambae alitufanya tushikamane na kupambana nae.. hivi sasa mambo yamebadilika,baada ya kuwa huru sasa tumeanza kugeukiana sisi kwa sisi‼,hili tu linatosha kutukana nguvu walizojitoa wazee wetu ktk kupambana Uhuru wa viumbe ambao Leo hii twajizuru sisi kwa sisi hiyo ndio tafsiri yake.
Mbali na hapo yale tuliyoyaita mabeberu ndo kwanza yamekaa pembeni yakicheka kwa tuo kwa kuona watoto walioachiwa uhuru wakiutumia Uhuru huo kwa kujizuru wao!.Hivyo hili linatosha kutoa tafsiri ya udhaifu wetu mbele ya adui yetu.
Watu Kama gadafi na nyerere wao walikuwa na mtazamo wa tofauti kwani walihitaji Afrika kuwa moja‼,lkn kwa hili kikulacho ki nguoni mwako huko Afrika ya kusini kinatoa tafsiri ya kuwa Afrika kuwa moja kwa kuungana ni nadharia ambayo hata ndoto haipo!!.
Tukio Kama hili halijaanza Leo ni kidonda ambacho kimeshahamishia makazi yake eneo husika mpk kufikia hadhi ya kuitwa kidonda ndugu‼,hili pia linatafsiri kuwa viongozi wa eneo husika wameshindwa kutatua tatizo ambapo hata kushindwa kwao ni tatizo pia. Kama pia Afrika kwa ujumla tutashindwa kuchukua hatua dhidi ya Kile kinachoendelea napo pia itakuwa ni tatizo‼.Kama hatujui pia waafrika tumekosea wapi Basi hili pia ni tatizo na Kile kinachotupata ni matokeo ya matatizo.
 
hili pia linatafsiri kuwa viongozi wa eneo husika wameshindwa kutatua tatizo ambapo hata kushindwa kwao ni tatizo pia
Na hii ndio hofu yangu kuu. Wapo waliokemea; lakini je, inawezekana kuwa wengi wao wanaunga mkono huo unyama unaoendelea??
Mungu Ibariki Afrika!!!
 
Na hii ndio hofu yangu kuu. Wapo waliokemea; lakini je, inawezekana kuwa wengi wao wanaunga mkono huo unyama unaoendelea??
Mungu Ibariki Afrika!!!
Bado Kuna sintofahamu ila ni Kama ujumbe unasubiriwa ufike kwa kina ndo wachukue maamuzi na sijui kwanini viongozi wetu hawalitilii maanani ila zile video zinatoa tafsiri mbaya na mbovu.
 
aisee nigeria boko haram wamelipua ubarozi wa sa huko kwao,sijui wakiamua kwenda kuwafuata wasouth nyumbani kwao itakuwaje.
maana naona mmasai kaingia uwanjani na bakora sasa
 
aisee nigeria boko haram wamelipua ubarozi wa sa huko kwao,sijui wakiamua kwenda kuwafuata wasouth nyumbani kwao itakuwaje.
maana naona mmasai kaingia uwanjani na bakora sasa
Huwa naamini Kila utakachofanya kina matokeo yake
 
Back
Top Bottom