Nini tafsiri ya hii kauli ya Kigwangala?

Abuwhythum

JF-Expert Member
Jan 7, 2015
837
495
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla kwa mara ya kwanza ametoa sababu ya yeye kushindwa kuweka wazi orodha ya watu wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja (mashoga)

Amesema hakuaua kuyataja hadharani majina hayo kwa kuwa nikusikiliza ushauri aliopewa na jamii inayomzunguka.

“Mimi nashaurika, sikuweka majina hadharani kwa sababu nashaurika, listi ya watu ninayo na tunachukuwa hatua kimya kimya hili ni kosa la jinai na mtu anayekutwa na hatia anafungwa kifungo cha miaka 30 jela” Amesema Dkt. Kigwangalla
Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema, hayo wakati akiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Ustawi wa Jamii Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Dar es Salaam, katika maadhimisho hayo Kigwangalla ameeleza kuwa kufanya mapenzi ya jinsia moja ni kosa kibaiolojia na hairuhusiwi mtu kuvutiwa na mtu wa jinsia yake.

Aidha, amesema katika sheria iliyotungwa mwaka 2012 ya kukazia adhabu ya mapenzi ya jinsia moja, kuna kipengele kinachotaka mtu achukuliwe hatua endapo ikithibitika amekaa mapozi yasiyoeleweka na ikabainika kuwa ni kwa lengo la mapenzi ya jinsia moja atafunguliwa mashtaka.

Mhe. Kigwangalla amewaonya wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja na kusisitiza kwamba serikali inawachukulia hatua kimya kimya.
 
hapo kuna walengwa wasio shaurika na ndio maana yeye kajitoa...ile kauli ya Nape "hekima" ni muhimu sana.
 
Ila kwakweli kigwangala,akimuacha bashite ktk hili,inabidi nae vyeti vyake vikaguliwe.manake bashite akihucshwa tu na kukaliwa kooni,atamtaja mpenzi wake,na ndo tunachokitaka.sheria ichukue mkondo kwa wanamapenzi wa jinca moja bila kujali vyeo au vitisho vyao.
 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla kwa mara ya kwanza ametoa sababu ya yeye kushindwa kuweka wazi orodha ya watu wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja (mashoga)

Amesema hakuaua kuyataja hadharani majina hayo kwa kuwa nikusikiliza ushauri aliopewa na jamii inayomzunguka.

“Mimi nashaurika, sikuweka majina hadharani kwa sababu nashaurika, listi ya watu ninayo na tunachukuwa hatua kimya kimya hili ni kosa la jinai na mtu anayekutwa na hatia anafungwa kifungo cha miaka 30 jela” Amesema Dkt. Kigwangalla
Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema, hayo wakati akiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Ustawi wa Jamii Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Dar es Salaam, katika maadhimisho hayo Kigwangalla ameeleza kuwa kufanya mapenzi ya jinsia moja ni kosa kibaiolojia na hairuhusiwi mtu kuvutiwa na mtu wa jinsia yake.

Aidha, amesema katika sheria iliyotungwa mwaka 2012 ya kukazia adhabu ya mapenzi ya jinsia moja, kuna kipengele kinachotaka mtu achukuliwe hatua endapo ikithibitika amekaa mapozi yasiyoeleweka na ikabainika kuwa ni kwa lengo la mapenzi ya jinsia moja atafunguliwa mashtaka.

Mhe. Kigwangalla amewaonya wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja na kusisitiza kwamba serikali inawachukulia hatua kimya kimya.
Ni madaraka pekee yanayounganisha ccm , vinginevyo hiki chama kimegawanyika haijapata kutokea .
 
Huyu nae hivi idara ya afya matatizo yameisha?
Hakuna matatizo zaidi ya ushoga?
Ndo maana aliulizwa "kwenye kampeni waliahidi kulinda miknd ya wanaume"
 
Back
Top Bottom