Nini siri ya matumizi ya Kingreza kongamano la Wanawake?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,015
114,360
Jana kulikuwa na kongamano la siku ya wanawake duniani.Walikuwepo wanawake kadhaa wenye Majina makubwa sana hapa nchini.Dr.Migiro,Makamu wa Rais Bi.Samia,Mkurugenzi wa ITV Bi.Mhavile.Lugha ya mawasiliano ilikuwa ni kingreza.Wanawake wale walishindana kuchana kingreza.Mhavile alitisha sana ilikuwa kama kameza kanda ya Bi.Hilal Clinton.Lakini Je,nini hasa lengo la matumizi ya lugha hii?Walitaka kuwalingishia vigogo wa kiume?
 
Mbaya zaidi 90% ya wanaotuongelea Kiinglish hatukijui.
 
nilijiuliza sikupata jibu labda walikuwa foreigners wengi,, au kuonyesha kuwa wanawake pia tunaweza kuongea kiinglishi
 
jana wamenikera sana watatumiaje lugha ya watu badala ya kutumia kiswahili chetu awa akina mama nao sijui vipi au ndio kututambia tusioijua?
 
Bavicha bana kwa kulalamika daah!! Jana rais kahutubia kwa kiswahili wamelalamika kuwa kwa nini akuhutubia kwa kiingereza hawa kina mama wametoa hotuba zao kwa kiingereza Bavicha, wanalalamika tena wao kila kitu kupinga tu ndiyo tafsiri yao upinzani ni kupinga kila kitu.
 
Hivi Ritz kuna mtu aliyepinga??Tunaongelea meseji ilikuwa inatakiwa kwenda kwa wasiojua kiinglish na wao wameongea kiinglish,unataka tufanyeje hapo??Tusiojua kiinglish ndiyo tunaoshangaa na eti ndiyo walikuwa wanatusemea sasa kuhoji imekuwa taabu??
 
Wanawake hawa wamenisikitisha sana kwanza lile kongamanolinamfikishia ujumbe gani mwanamke wa kawaida mwenye elimu ya chini? kuwa mwanamke mwenye kujiamini lazima kujua kiingereza! Hapo walibagua .
 
jana wamenikera sana watatumiaje lugha ya watu badala ya kutumia kiswahili chetu awa akina mama nao sijui vipi au ndio kututambia tusioijua?
Ahahahahahaha kaka wacha watumie walikua wanafanya zoez mana wakiwa na mzungu wanajua kua wanachapia ila wenye kwa wenye tutaonyeshana tunajua vizur wakiwa na mzungu wanataka kiswahili mana wataongea zaid ya ngeli duh kwel atujui tunataka nn ata mi wamenikera sna nakuunga mkono
 
Wanawake hawa wamenisikitisha sana kwanza lile kongamanolinamfikishia ujumbe gani mwanamke wa kawaida mwenye elimu ya chini? kuwa mwanamke mwenye kujiamini lazima kujua kiingereza! Hapo walibagua .

Vituko + Vimbwanga mkuu! Mimi nilidhani ni "tea party" ya wadada wa mujini + wamama!!

**Ndio maana Dunia Imefika ilipo!
 
Kwa hili walilolifanya siku nyingine wakiingia mitaani wawakusanye kina mama ili kuwaeleza jambo lihusulo hii siku ya wanawake wataambulia viti vitupu, wanawake watakimbia maana wamepewa ujumbe kuongea kiingereza ni msingi wa shughuli za wanawake.
 
Back
Top Bottom