Adam-street-art
New Member
- Jun 7, 2017
- 2
- 0
Habari zenu wana Jf. Mini ni mtumiaji mpya wa jamii forum ila nina jambo moja linanichanganya na kama kuna mwenye kulijua hili naomba kuelimishwa. Nimekuwa nikisoma habari nyingi kuhusu hawa watu wanaojiita Freemason. Wana history ya kawaida kabisa katika kuanza kwa jamii yao ila nimeshindwa kutambua kiini cha uanzishwaji wa kundi lao ukizingatia kuwa kundi lao limehusisha watu wenye nguvu kubwa kiuchumi kijamii na kisiasa.Wamekuwa wakihubiri dunia huru yenye maamuzi huru kwa kila kitu. Mali na vyote wanadai wanamiliki wao na wanaweza kumpa wamtakae ili hali nikisoma biblia inasema fedha na magari ni mali ya Bwana. Sasa siri yao ni nini? Wanafanya nini? Kwanini wameweza kuteka kundi la watu wenye nguvu duniani? Na dunia huru yenye maamuzi huru maana yake nini? Nimeona kundi kubwa la watu wakiomba kuunganishwa na kundi ilo nikapata wasiwasi kuwa huenda wana nguvu kuliko tunavoweza kufikiria. Naomba msaada Tafadhali.