Nini sababu ya TANESCO kung'ang‘ania kuwa wao tu ndio wazalishaji pekee wa nishati ya umeme

Hiyo kuwa TANESCO kuwa Sole distributor ndo ukiritimba unapoanzia kwa wasipewe mamlaka na uwezo wa kutusambazia umeme wao unaweza shangaa wakatuuzia kwa vunja bei price kitendo cha kuwauzia TANESCO tunarudi kwenye kupeana huduma kibabe bila sababu.We angalia TTCL inavyolazimisha kunyanyuka ila inashindwa bado Kuna mkonga wa Taifa jumlisha HAYATI kulazimisha kila mtumishi atumie line ya TTCL bado imeshindikana
wana wauzia tanesco ili waweze kupata pesa ya uhakika na kupunguza idadi ya rasilimal watu ambyo ni gharama ktk uendeshaji

kuna watu wana sambaza maji pia mijini na vijijini kwa kutumia magari na pipes...

huduma zipo, nenda pale uwekezaji watakuambia jinsi ya kupata leseni hizi na zipo ktk fomu ya biashara...
 
Hakuna muwekezaji anayetaka kuzalisha na kusambaza umeme, wakati wa JK iliwahi kutolewa ofa hiyo lakini hakupatikana hata mmoja.
Woote wanataka kuzalisha Halafu waiuzie TANESCO isambaze kwa sababu kwenye usambazaji ndipo hasara ilipo,mfano wizi wa umeme na kuharibika njia za umeme.
Kimsingi suala la umeme liko connected moja kwa moja na usalama wa nchi hivyo ni lazima serikali iwe mbia mkuu
 
Huku nilipo kuna mgao wa umeme ambao naona hata sio rafiki na maisha ya utafutaji ya kila siku ya watanzania Mfano Welding, wauza vinywaji, mafundi wote watumia nishati ya umeme, wauza samaki, fresh foods n.k

Ndipo nikaja na swali je kipi kipo nyuma ya pazia TANESCO kuwa monopoly producer wa umeme hapa nchini huku kila mtu anajua serikali haina uwezo wa kufanya biashara kwa sababu ya kukosa uwezo wa usimamizi staffs wake ni wezi, wasiopenda kujituma, walalamishi.

Ni nini kinatulazimisha TANESCO awe ni yeye tu mzalishaji wa umeme hapa nchini huku tukijua hii nishati ina muhimu karibia sector zote za kiuchumi na maendeleo. SHIRIKA LA TANESCO tukubali limeshindwa kuwahudumia WATANZANIA kwa sababu hatuwezi kumaliza mwaka bila kuwa na mgao wa umeme sababu ni zile zile kushuka kwa kina cha maji, mabwawa ya umeme kujaa michanga. Unajua TANESCO isingekuwa imeng’ang‘ania kuwa wao pekee tu ndo wazalishaji tungenufaika na mambo mengi sana ikiwemo kuuziwa UNITS kwa bei poa kwa sababu ya ushindani, Huduma zingeboreshwa kiasi kwamba kusubiria ishu kama nguzo na mita kwa muda mrefu kusingekuwepo.

Tungeweza kununua units kama vile voucher ukinunua sio mpaka uende kwajirani kujiombereze upachike kale kadude ka Luku ili uingize tokens. Kwa kifupi wazalishaji wangekuwa wengi tungenufaika na ushindani wao ni kama unavyoona mitandao ya simu TIGO wakizingua unahamia AIRTEL hivyo unalazimisha tigo wajitafakari dhidi ya kupoteza wateja wao.
USHAURI WANGU : Serikali iache kuwa na mbinu za kizamani kwenye kupambana na matatizo ya kisasa .Hivyo naomba kuchukua nafasi hii kuiomba serikali ialike makampuni ya kimataifa kutoka nje ili kuja kuwekeza hapa nchini kwenye hii sector nyeti ya NISHATI ili TANZANIA iweze kusonga kwa speed nzuri.

Kama serikali itaamua kukomaa na H.E.P basi itoe nafasi kwa makampuni kuwekeza kwenye umeme wa UPEPO, GASI,JUA,MAKAA YA MAWE,MIKONDO YA BAHARI,URANIUM N.K alafu TANESCO libaki kama regulatory board.Sioni sababu ya msingi ya TANESCO kukumbatia sector hii peke yake kwa sababu inazalisha hasara kwenye biashara za watu na inafanya inchi yetu pendwa kuwa na mdororo wa uchumi pasipo na sababu ya msingi.

SWALI: Nini kinalindwa mpaka TANESCO analindwa asiwe na mpinzani?
kwenye uchumi tunaita Monopoly
 
Ninavyojua hiyo ni huduma kwa jamii km barabara,maji nk
Ukiruhusu huduma ya jamii imilikiwe na mtu binfsi ni hatari hata kwa usalama wa nchi
Wanasiasa wamekuwa wakuwatumia wahindi na waarabu kujaribu kubinafsisha tanesco ili wavune mapesa
Elimu ni Huduma kwa jamii lakini Kuna shule na vyuo vya serikali na binafsi
Afya Kuna hospital binafsi na za serikali
Hadi ulinzi Kuna kampuni binafsi za ulinzi
Usafiri napo
Kwa nini umeme na maji ndio vionekane vina viashiria vya usalama WA mustakabali WA taifa??
Total bullshit
 
Mitandao ya simu mbona ni huduma za jamii na hapo ndo kwenye kuvuja kwa taarifa muhimu za kiusalama ila hilo sio tatizo.WAWEKEZAJI KUZALISHA NA KUTENGENEZA NISHATI YA UMEME WANAHATARISHAJE USALAMA WA NCHI HEBU FAFANUA
Umeme ni kila kitu, watu wanapata mwanga, pampu za maji zinafanya kazi, huduma za hospitali zinaendelea, mitambo ya ulinzi inafanya kazi, majokufu na majiko yakupikia yanafanya kazi, treni za umeme zinatembea, radio ,Television na minara ya simu inafanya kazi, gharama za matumizi ya umeme lazima zizingatie huduma kuliko faida. Huduma ya nishati ya umeme huwezi linganisha na makampuni ya simu. Kwa mawasiliano ya kimataifa serikali haitaji Tigo au vodacom au airtel.
 
Ninavyojua hiyo ni huduma kwa jamii km barabara,maji nk
Ukiruhusu huduma ya jamii imilikiwe na mtu binfsi ni hatari hata kwa usalama wa nchi
Wanasiasa wamekuwa wakuwatumia wahindi na waarabu kujaribu kubinafsisha tanesco ili wavune mapesa
Nchi za wadanganyika ndio wenye mawazo haya.
 
Back
Top Bottom