Vituko vya Ma-house girls na Mabosi wao havielezeki kwa urahisi. Ningekataa, lakini siwezi,kila kukicha kuna reports Mzee kazidiwa kalamba house girl. Tujiulize ni kweli kwamba house girl kuwa karibu na mzee ndio iwe sababu?
Tuangalie matumizi ya muda. Muda ambao mwanaume anautumia akiwa nyumbani na ule wa kazini. Kimsingi, muda mwingi anautumia akiwa kazini. Ukaribu wa house girl na baba si zaidi ya masaa matatu au manne. Kule kazini ofisi nyingi kuna wahudumu au sekretari, hawa ni karibu na hao ma-house girl, nao wanahudumia chakula, vinywaji (soft), mafaili, taarifa za hapa na pale, kufagia ofisi ya mzee na kumpokea punde afikapo kazini. Haya sasa, je, rate ya kulabwa hawa watu ni sawa na ma-house girl?
Mimi suala hili naliangalia katika mtizamo huu: Ma-house girl wengi ni watoto wanaochipukia (adolescents)kipindi hiki kila mtu anakifahamu ni cha kutaka kufahamu kila kitu na mwili una-demand sana tu. House girl hana nafasi ya kutoka nje ya nyumba, akitoka anaambana na mtoto anayemlea, angekuwa na uhuru wa kutoka pekee yake angeweza kuyafanya haya na vijana wenzake lakini muda huo hana. Alternative'iliyobaki ni yule aliyeko karibu naye 'Mzee'. Kwa maana hiyo, kubanwa sana kwa ma-house girl kuna wafanya wachukue kilichokaribu yao.