Nini sababu ya mabosi wengi kuwataka wafanyakazi wao wa ndani kimapenz?

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,286
hili jambo liko wazi, mabosi wengi hususan wa kiume hupenda kufanya mapenzi na wafanyakazi wao wa ndani, ilhali mke yumo mle mle ndani ya nyumba hiyo hiyo, mimi ninauliza je kwa nini inakuwa hivyo? . tena ukizingatia wakati mwingine mke wa mtu wakati mwingine ni kifaa tosha kuliko hata mfanyakazi wa ndani mwenyewe?
ni zipi sababu?

tujadili
 
Muheshimiwa
mada inelemea upande mmoja!
mimi sikubaliani na sentensi ya 'mabosi wa kiume', nafikiri hapa ni wanaume, (labda kama assumption mabosi wengi ndio wenye uwezo wa kuwa na watumishi wa ndani).
Na hali hii hutokea kwa wamama pia kufanya mapenzi na mahouseboy/shamba boy wake wakati mumewe ni kifaa.
Naona umeamua kuanza na wanaume mabosi first?
 
kasana ukiangalia vizuri nimesema mabosi wengi "hususan" wanaume,angalia neno "hususan" sijaexclude wanawake hapo, ila kwa mazingira ya tz, mahouse girl ni wengi kuliko mahouse boy.
kwa hiyo ni likely ishu ipo zaidi kwa baba(wanaume) na mahouse girl.
 
Gamba la Nyoka
Unajua siku hizi wanawake wanaojiita career women, wanabase sana kwa kazi zao za nje na kusahau kazi zao za nyumbani. Matokeo yake ni kuwa inaonekana kuwa msichana wa ndani ndiye anyefanya kazi vizuri ya kukufulia nguo, kunyoosha, hata chakula kizuri na kitamu anapika yeye. Mke yeye anakuwa busy na mengine nje ya nyumba, sasa kama mtoto akikuenzi kuna ubaya gani na wewe ukimuenzi? nadhani hii ni very logical.
Hii same applies kwa shambaboy/ au house boy. Kama yeye ndio yuko home kila siku na kumsaidia mkeo kazi zote za nyumbani na kuwepo anapomhitaji kwani haiwezekani naye kuenziwa, unajua haya ni ya kawaida kabisa, kwa hiyo tunatakiwa kujifunza.!!
 
Nimekupata gamba la nyoka,
Mimi naamini mambo ya kujivinjari na mahouse girl ni tabia ya mtu na inatokana na tamaa za kimwili,
Na watu wanamna hiyo pia hawachelewi kuwalalmba mabinti zao kwa kisingizio wamefanana na mrs.

Yes career (kuwa busy) inaweza kuwa sababu kuwa mtu kashindwa kuhimili mikiki, then anaanza kujenga hisia, hata hivyo kunamambo mengi yanaweza kuchangia ikiwemo na uwezo wa kuchemza mduara.
 
Vituko vya Ma-house girls na Mabosi wao havielezeki kwa urahisi. Ningekataa, lakini siwezi,kila kukicha kuna reports Mzee kazidiwa kalamba house girl. Tujiulize ni kweli kwamba house girl kuwa karibu na mzee ndio iwe sababu?

Tuangalie matumizi ya muda. Muda ambao mwanaume anautumia akiwa nyumbani na ule wa kazini. Kimsingi, muda mwingi anautumia akiwa kazini. Ukaribu wa house girl na baba si zaidi ya masaa matatu au manne. Kule kazini ofisi nyingi kuna wahudumu au sekretari, hawa ni karibu na hao ma-house girl, nao wanahudumia chakula, vinywaji (soft), mafaili, taarifa za hapa na pale, kufagia ofisi ya mzee na kumpokea punde afikapo kazini. Haya sasa, je, rate ya kulabwa hawa watu ni sawa na ma-house girl?

Mimi suala hili naliangalia katika mtizamo huu: Ma-house girl wengi ni watoto wanaochipukia (adolescents)kipindi hiki kila mtu anakifahamu ni cha kutaka kufahamu kila kitu na mwili una-demand sana tu. House girl hana nafasi ya kutoka nje ya nyumba, akitoka anaambana na mtoto anayemlea, angekuwa na uhuru wa kutoka pekee yake angeweza kuyafanya haya na vijana wenzake lakini muda huo hana. Alternative'iliyobaki ni yule aliyeko karibu naye 'Mzee'. Kwa maana hiyo, kubanwa sana kwa ma-house girl kuna wafanya wachukue kilichokaribu yao.
 
Naungana na hoja na nina nyongeza.


1.
Akina mama wengi wanajisahahu kutimiza matakwa ya ndoa hasa wakiwa na shuguli za kufanya (biashara na waajiriwa maofisin).Hurudi nyumbani wamechoka na kujikuta shughuli zote anaachiwa dada wa kazi,mfano kupeleka maji bafuni,kumuandalia msosi bwana mkubwa,mume akichelewa kurudi nyumbani hufunguliwa mlango na dada wa kazi na kumfanyia yote ambayo mama angepaswa kufanya.Hali huii ikiendelea kwa mda furani baba huanza kujenga hisia sa karibu na hatimae huanza uroda.

2.Kipato cha Housegirls ni kidogo saana,wengine hunyanyaswa na mabosi wao hasa akina mama kwa lengo la kuwapunguzia hadhi dhidi ya waume majumbani.Kama njia ya kuongeza kipato na kurevenge kwa mabosi wao(akina mama),Dada wa kazi hutumia ile mianya anayopewa na Mama kumhudumia Baba kutimiza hila na matakwa yake.Ndiyo maana si ajabu baada ya mda mfupi kumkuta dada wakazi akianza kujibizana na Mama.Maana wakati dada na baba wakijinvinjari kimahaba kila aina ya ahadi huanza kutolewa na hivyo kumpa kichwa hausegirl.Kimsingin wengine huamua kuoa kabisa.

3.Visa maofisini vya bosi na wasaidizi wao vipo vingi ila haviripotiwi nafikiri ni kwasababu vya maofisin kuna aina furani ya makubaliano zaidi kuliko aina furani ya ulazima inayotumika kwa mahausegelo.

4.Mama na shambaboy hii nayo ipo saana ila wanume wengi hawareport mikasa hii,kwakuwa kwa wanaume wengi kureport mikasa kama hii inachukuliwa kama aibu​
 
kuna na wale mabosi wanaotumia unyonge wa mahouse girl kiuchumi na kielimu kuwa "blackmail" mahouse girl il watoe penzi, mathalani house girl akikataa ombi la mzee hutishiwa kufukuzwa kazi nalo hili mnalionaje?
 
Ninadhani tatizo ni mme/mke kutokuwa mkweli kwenye ndoa. Kitu cha kwanza kabisa ambacho huvutia watu ki mapenzi ni physical. Jinsi mwanamke/mwanaume anavyovutiwa na mtu wa kawaida mtaani na kuamua kummtongoza ni sawa sawa na mme/mke anavyovutiwa na msaidizi wake wa nyumbani.

Akina mama wengi kwa mfano, wakisha zaa huwa kuna mabadiliko ya kimaumbile. Kutokana na utamaduni wetu, hatuna tabia ya kujitunza kama wenzetu wa magharibi wanavyojitunza. Wasaidizi wa nyumbani wengi huwa katika umri wa mwisho wa miaka kumi au mwanzo wa miaka ishirini. Hichi ni kipindi ambacho mtu anakuwa na anapendeza (nawiri)sana. Ukichanganya na tabia ya mtu kutokuwa muaminifu katika ndoa anaamua kuomba penzi, akionjeshwa basi anataka kila sikuu. Na hili swala la kubadilika ki maumbile lipo kwa wanaume pia wanapokuwa na maisha mazuri.

Kwahiyo, suala zima hapa ni uaminifu katika ndoa.
 
Dah..JF ya zamani watu walikua wanatiririka point za maana..mpka inafurahisha..pongezi kwao ma legendary wakitambo hicho..
 
mke unamtumia kila siku unamchoka ila huyo mrembo kila siku unamuona anang'aa lazima umfuatilie...
 
Mwafrika hasa Mtanzania ana roho chafu sana iliyojaaa tamaa.
Wafanyakazi wa ndani, masekretari ofisini wanafanywa sexy machines. Yaani mwafrika akimwona binti tu karibu yake ufahamu wake unaondoka unabaki wa kinyama. Ngono inayofanywa na mtu ambaye si sahihi/halali matokeo yake mwishoni ni mabaya zaidi ya raha ya dk chache anayoipata mtu wakati wa tendo.
Wanaume hebu tutafakari upya.
Wengi wameharibu familia, kazi na kuvunjiwa heshima katika jamii kwa kuendekeza huu upumbavu.
 
watoto wa kiume pia hufanya ma-housgirl kama jaribio sex baada ya kubalehe. Nyumba nyingine unakuta baba anapiga na mwanae kama mmoja wao ni HIV+ ndiyo hapo sasa.
 
Back
Top Bottom