Sahihisho kidogo, zilitaifishwa 1971 chini ya sheria ya Acquisition of Buildings Act. Ni kweli nyingi zilikuwa za wahindi kwanni sheria ililenga wamiliki ambao walikuwa hawaishi nchini (abstentee landlordism)
Mpeni Bwana Mdogo muda, nadhani ataweza - ile ni biashara, yeye ni CEO na CEO anapaswa kwa maono yangu awe ni mtu mwenye taaluma isiyoshabihiana na wale watendaji wengine. Unajua Injinia kwa Injinia wanavimbishiana maguvu, Architect humponda architect mwenzie, na the more specialised hawa watu ni kadiri hiyo wanavyopondana. Ukiweka juu yao kiunganishi basi inawezekana umefanya vizuri, ni mapema mno mwache bwana mdogo afanye kazi.
Kama amemchukua mwanae Karume yule wa Knight Frank sio vibaya, kale kabinti ukiacha makidai kama kina dada wengi waliokwisha kula kuku kwa mrija, hakajambo, kanajua kazi yake ni mwana-taaluma yule, usimhukumu kwa kuwa baba yake ni Karume au kwa kuwa katoka Zanzibar, angeweza pia kutoka Nigeria kama alivyokuwa yule Bw wa Tanroads kabla ya Mrema.