Nini mustakabali wa siasa za Tanzania na vikundi vya "Wanamgambo" wa Vyama?

NewDawnTz

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
1,667
362
Hakuna kitu kinachonipa mashaka sasa ninapotafakari siasa za Tanzania zinapopeleka usalama wa nchi yetu kama swala la hivi vikundi vyao vya "askari" vinavyofanya kazi chini ya vyama vya siasa (Militia groups affiliated under Political parties). Hapa nazungumzia Green Guards ya CCM na Red Brigade (kama sijakosea jina - naweza kurekebishwa) ya CHADEMA.

Nimejiuliza maswali mengi sana hasa baada ya matukio ya hivi karibuni ambayo yanahusisha vikundi hivi kuhusika ikiwemo matukio kadha wa kadha huko Igunga pamoja na yaliyotokea jana huko Mwanza kama yalivyowasilishwa na baadhi ya members wa JF kuhusu Green Guard kupiga watu hadi kuwajeruhi huko Mwanza.

Naomba tujadili mwelekeo wa siasa ya Tanzania na kuwepo kwa vikundi hivi chini ya vyama kwa kuzingatia mambo yafuatayo.

  1. Hawa watu ni wakina nani? Je kuna sheria yoyote inayotoa uhalali wa kuwepo kwavyo?
  2. Je katiba za vyama vya siasa zinasehemu yoyote inayozungumzia kuwepo kwa vikundi hivi? Na kama ndiyo, je zimeanishaje majukumu ya vikundi hivi? Na je kuna uhalali wa kisheria unaotoa mwanya kwa vyama vya siasa kujianzishia vikundi kama hivi? Je inakubalika kuwepo kwa sheria ya namna hiyo?
  3. Je sheria ya vyama vya siasa inaruhusu kuwepo kwa vikundi hivi ndani ya vyama vya siasa? Kama sivyo je huu sio uvunjaji wa Sheria za Uanzishwaji wa Vyama vya siasa unaohitaji kuchukuliwa hatua? Au ndio tuseme "When the State is corrupt then the laws are most multiplied?"
  4. Je kuna wakati wowote ambao kuna kiongozi yoyote mwenye mamlaka ya usimamizi wa vyama vya siasa (Hapa namzungumzia Msajili wa Vyama vya Siasa ndugu John Tendwa) ametoa kauli ya kuzuia vikundi hivi? J e wale wenye mamlaka ya kusimamia usalama wa Taifa na Raia wake (Nazungumzia Jeshi la Polisi Tanzania na Jeshi la Wananchi wa Tanzania) wametoa kauli dhidi ya vikundi hivi ambavyo ni hatari kwa usalama wa Raia na Taifa kwa ujumla wake? Au ndio "Polisi Jamii" wenyewe?
  5. Je kuwepo kwa vikundi hivi ni ishara ya jeshi la polisi kushindwa kusimamia usalama wa shughuli za vyama vya siasa na ulinzi wa wanasiasa na kulazimisha kuanzishwa kwa vikundi hivi na vyama vya siasa ili kujihakikishia usalama?
  6. Je sisi kama Watanzania tunaona ni vema kwa vikundi hivi kuendelea kuwepo na kufanya kazi chini ya vyama vya siasa tena pasipo sheria halali wala majukumu yanayoeleweka? Viongozi wa vyama vya siasa mlioko hapa, bila kutafuna maneno, je mnadhani siasa yetu inahitaji sana vikundi hivi na wala sio polisi kusimamia yale ambayo vikundi hivi mmevianzishwa "kihunihuni"?
Niemuliza maswali haya kwa kuzingatia kuwa hapa tuna manguli wa mambo ya kisiasa wenye uzoefu wa siasa za kitaifa na kimtaifa, wanausalama wa Raia na Taifa na zaidi kuna viongozi wa Vyama vya siasa na wengine wakiwa kwenye Idara ya Uenzi na Itikadi ambao naamini kama hawatafungwa na ile kauli "Affection binds reason" wanaweza kutusaidia kupata picha ya vikundi hivi ambavyo kama sitapata msaada wa kuelewa kuwa vinaishi kihalali basi kwangu mimi ni "magenge ya wahuni" waliohalalishwa na "wahuni wenzao" wachache bila kuangalia mustakabali wa nchi hii.

ANGALIZO:
Hapa sizungumzii unstructured group kama vile kundi la watu ambalo halikuwa limejipanga kufanya kitu fulani ila imetokea ghafla wakajikuta kuwa na common interest na kujiunga kufanya jambo fulani.

Hapa nazungumzia kundi la watu ambalo limeandaliwa, limepewa jina, linafahamika na wanapatiwa hadi usafiri na nafasi ya kusimama mstari wa mbele au "kulinda usalama" huku wahusika wakiwa wanajua lipo kundi la namna hiyo na wakitolerate existence yavyo na utekelezaji wa "shughuli" zao.

Na pia tujadili kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa na sio kwa "maslahi"ya vyama vyetu vya siasa nikikopa msemo wa Invisible "Tujadili kiuhalisia na sio kisiasa"


Naomba niwasilishe kwenu kwa mjadala zaidi......

UPDATE: April 2015 > IGP Mangu: Marufuku kuwa na Vikundi vya Ulinzi vya Vyama vya siasa kwani ni kinyume cha Katiba na Sheria ya nchi
 
Inategemea Kazi ya Green Guards na Red Brigade. LAbda utupatie kazi zake. Maana kuna ambao wanamiliki Tindikali na wengine ni wanaohamasisha vijana wenzao kuleta umoja wa Tanzania mpya!. Sasa tatizo ni Madhumuni husika. Yale ya Mwanza ya mtu kuzomewa then kifuata kipigo.
 
Inategemea Kazi ya Green Guards na Red Brigade. LAbda utupatie kazi zake. Maana kuna ambao wanamiliki Tindikali na wengine ni wanaohamasisha vijana wenzao kuleta umoja wa Tanzania mpya!. Sasa tatizo ni Madhumuni husika. Yale ya Mwanza ya mtu kuzomewa then kifuata kipigo.

Mkuu ukinisoma vizuri hapo utagundua sizungumzii "kuhamasishana" na kwa kufuatilia haraka haraka utagundua kuwa hawa Green Guard hawafanyi hiki unachokiita kuhamasishana kuleta umoja wa Tanzania mpya.

Kwa haraka haraka pia naweza kusema kazi hii ya kuhamasishana ipo kwenye vyama kupitia vyama vya vijana, wanawake na wazazi/wazee lakini sio kazi za hawa Guards ndio maana najikuta nina maswali mengi na hofu juu ya hivi vikundi
 
Hivi vikundi si muafaka kwa mustakabali wa siasa za Tanzania. Vipo vyombo vinavyotambulika kikatiba na kisheria kufanya kazi ya ulinzi (polisi, usalama wa taifa, mgambo, n.k.). Mimi naviona kama ishara ya militant politics ambazo mwisho wake ni hatari kwa Tz. Mfano, chama kimoja kikishindwa uchaguzi, halafu kikagoma kwa jeuri kukabidhi madaraka, hivi vikundi ndivyo vitakuwa vikitumiwa kuchochea fujo na vurugu kwa raia. Sioni tofauti yake na banyamulenge, janjaweed, n.k.
 
Hivi vikundi si muafaka kwa mustakabali wa siasa za Tanzania. Vipo vyombo vinavyotambulika kikatiba na kisheria kufanya kazi ya ulinzi (polisi, usalama wa taifa, mgambo, n.k.). Mimi naviona kama ishara ya militant politics ambazo mwisho wake ni hatari kwa Tz. Mfano, chama kimoja kikishindwa uchaguzi, halafu kikagoma kwa jeuri kukabidhi madaraka, hivi vikundi ndivyo vitakuwa vikitumiwa kuchochea fujo na vurugu kwa raia. Sioni tofauti yake na banyamulenge, janjaweed, n.k.

Kinachonipa wasi wasi ni tofauti kati ya nchi nyingine za wenzetu zilizokuwa kwenye vita na sisi....wao vikundi vyao vya waasi baada ya kupatanishwa na kurejea hali ya amani vimegeuka kuwa vyama vya siasa.....Je hiii sio ishara sahihi kuwa vikundi hivi vya hapa kwetu vitaenda kinyume yaani kutoka kwenye vyama vya siasa na kuwa waasi hasa inapotokea vyama vile vilivyovianzisha vinaposhindwa kwenye uchaguzi?

I am worried kweli juu ya kunyamazia watu hawa na kutengeneza bomu jipya la "banyamulenge siku zijazo"
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mimi ninakisikiaga kikundi kimoja tu cha Green Guard ambacho kimekuwa kikihusishwa na matukio ya kihalifu sehemu mbalimbali hasa kupiga watu na kuwajeruhi.Kikundi hiki kimekuwa kikivuma sana kwenye uchaguzi wa Igunga hasa matukio haramu ya kuteka watu.

Jina la kikundi hiki limechafuka sana machoni mwa jamii na watu wamekuwa wakikifananisha na Mungiki wa Kenya au Intarahamwe! Hiki kikundi cha Red Brigade sijawahi kukisikia katika matukio kadhaa ya kihalifu, lakini naomba mwenye taarifa zake kamili atujuze ili watanzania tuchukue tahadhari.
 
Molemo,

Ni kweli kuwa Green Guard inavuma kuliko na wanaangaliwa kwa kuwa Serikali ni ya Chama chao.......

Sisikitiki sana wao kuachwa na Chama chao kuendelea kufanya hivyo (nikiamini kuwa huenda wanatekeleza maagizo) ila kinachonisikitisha ni wa kina Shimbo, Mwema na Tendwa kukalia kimya jambo hili..........kwao vikundi kama hivi na mambo wanayoyafanya sio hatari kwao, ndivyo niaminivyo kwa kuwa sijawahi kusikia kauli yao.....ni hatari kwa kweli kama vitaendekezwa na kuendelea kuwepo, tena chini ya ufadhili wa vyama vya siasa
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli, si jambo la kujivunia kwa ustawi wa Tanzania. Upande mwingine, Green guard ndio kikundi rasmi,na kambini kinakaa kama jeshi,mafunzo wanapewa nk. Hiyo red brigade ni vijana wakakamavu waliochoshwa na uhuni,wizi na upuuzi wa Ccm. Kimsingi sidhani kama ati wanapewa mafunzo kama hao wa magamba. Ninahisi vitaibuka vikundi vingi tuu,hasa pale itakapo onekana dola haishughuliki na uovu wa vijana wa ccm.
 
Ni kweli, si jambo la kujivunia kwa ustawi wa Tanzania. Upande mwingine, Green guard ndio kikundi rasmi,na kambini kinakaa kama jeshi,mafunzo wanapewa nk. Hiyo red brigade ni vijana wakakamavu waliochoshwa na uhuni,wizi na upuuzi wa Ccm. Kimsingi sidhani kama ati wanapewa mafunzo kama hao wa magamba. Ninahisi vitaibuka vikundi vingi tuu,hasa pale itakapo onekana dola haishughuliki na uovu wa vijana wa ccm.

Kama kuna hadi hatua ya kuwapatia mafunzo maana yake hili ni kundi rasmi na ni sawa na jeshi kamili? Sheria zetu zinasemaje? Kwa nini wameachwa kuwa kimya tu? au kwa kuwa wanalinda maslahi ya chama chenye kushika dola?

Uganda waliliona jambo hili na wamelipiga marufuku, sisi bado tumekalia kimya na kuwaangalia tu kama mashujaa fulani...NI HATARI SANA
 
Ndugu yangu,

CCM wapo radhi kufanya chochote ,hasa inapokuja habari ya kuwatoa madarakani. Kumbuka kituko kile cha masharubu Mukama, ati makomandoo, magaidi wameingizwa na anawajua majina, idadi, hata nyumva walimo jificha; bado Serikali, polisi, jeshi, tiss, wanaona poa tuu,?

Upande wa sheria, hili lipo wazi. Law enforcers, ni hivyo vyombo nilivyotaja. Cha ajabu, mpiga domo, hata katibu tawi wa CCM ana mamlaka juu ya RPC, what do u expect?

Ukichunguza kwa mbali, unaweza kuona kuwa watakao sababisha vita ni hivi vyombo vya usalama.
 
Ndugu yangu,Ccm wapo radhi kufanya chochote ,hasa inapokuja habari ya kuwatoa madarakani. Kumbuka kituko kile cha masharubu Mukama, ati makomandoo,nagaidi wameingizwa na anawajua majina,idadi,hata nyumva walimo jificha,bado Serikali ,polisi,jeshi,tiss,wanaona poa tuu,???? Upande wa sheria,hili lipo wazi. Law enforcers,ni hivyo vyombo nilivyotaja. Cha ajabu,mpiga domo,hata katibu tawi wa Ccm ana mamlaka juu ya Rpc,what do u expect? Ukichunguza kwa mbali,unaweza kuona kuwa watakao sababisha vita ni hivi vyomba vya usalama.

Ninakubaliana na wewe kaka kwa asilimia 100 maana kwa mtazamo wangu kukalia kimya vigenge hivi vya wahuni ni hatari kuliko kuwepo kwavyo......nashindwa kuelewa ni kwamba mamlaka bado hazifumbuka macho kuona hatari au zimeamua tu kuziba masikio na macho zikijidai hazioni?
 
Kuna jambo moja muhimu ambalo naona wachangiaji hawajaliona - ni kwamba kama mtu umewahi kuishi nchi za nje hasa zile zinazoitwa ulimwengu wa kwanza au kama unafuatilia mambo ya nchi hizo utafahamu kuwa wakati wenzetu wanaongozwa kwa sheria sisi ni ile inayoitwa "a lawless jungle". Ninaamini kabisa kuwa kama kuna orodha ya nchi kumi duniani ambazo watu wake wanaishi bila kujua na kufuata sheria basi Tanzania lazima iwepo.

Matokeo yake ni kuwa watu wanajiamulia mambo wanavyotaka na hakuna kuadhibiwa wala kuwajibika, in fact wavunjaji wa sheria ndiyo wanaoonekana wajanja na wanatukuzwa. This country is daily slipping into a state of total anarchy because no one is in control and even worse those charged with the duty to enforce the law are ignorant of the law and even worse severely corrupt.

Ninachoamini ni kwamba as long as CCM continues to hold power, for sure civil war is a guaranteed outcome. Tusiamini kabisa kwamba sisi ni kisiwa cha amani na mfano wa kuigwa, la hasha, nchi nyingi zilizotumbukia kwenye vita nazo zillikuwa na amani kama hii lakini zikatumbukia hatua moja baada ya nyingine.
 
Ni kweli kuwa Green Guard inavuma kuliko na wanaangaliwa kwa kuwa Serikali ni ya Chama chao.......

Sisikitiki sana wao kuachwa na Chama chao kuendelea kufanya hivyo (nikiamini kuwa huenda wanatekeleza maagizo) ila kinachonisikitisha ni wa kina Shimbo, Mwema na Tendwa kukalia kimya jambo hili..........kwao vikundi kama hivi na mambo wanayoyafanya sio hatari kwao, ndivyo niaminivyo kwa kuwa sijawahi kusikia kauli yao.....ni hatari kwa kweli kama vitaendekezwa na kuendelea kuwepo, tena chini ya ufadhili wa vyama vya siasa

Ipo siku hicho green guards kitagawanyika kama mtandao ulivyo gawanyika na ndipo hapo watajua kuwa maharage si mboga bali dawa ya mbu!
 
Kuna jambo moja muhimu ambalo naona wachangiaji hawajaliona - ni kwamba kama mtu umewahi kuishi nchi za nje hasa zile zinazoitwa ulimwengu wa kwanza au kama unafuatilia mambo ya nchi hizo utafahamu kuwa wakati wenzetu wanaongozwa kwa sheria sisi ni ile inayoitwa "a lawless jungle". Ninaamini kabisa kuwa kama kuna orodha ya nchi kumi duniani ambazo watu wake wanaishi bila kujua na kufuata sheria basi Tanzania lazima iwepo.
Matokeo yake ni kuwa watu wanajiamulia mambo wanavyotaka na hakuna kuadhibiwa wala kuwajibika, in fact wavunjaji wa sheria ndiyo wanaoonekana wajanja na wanatukuzwa. This country is daily slipping into a state of total anarchy because no one is in control and even worse those charged with the duty to enforce the law are ignorant of the law and even worse severely corrupt.
Ninachoamini ni kwamba as long as CCM continues to hold power, for sure civil war is a guaranteed outcome. Tusiamini kabisa kwamba sisi ni kisiwa cha amani na mfano wa kuigwa, la hasha, nchi nyingi zilizotumbukia kwenye vita nazo zillikuwa na amani kama hii lakini zikatumbukia hatua moja baada ya nyingine.

Kwa asilimia kubwa sana nakubaliana na wewe kuwa changamoto kubwa ni kwa watekelezaji wa sheria kwa sababu kama wangekuwa makini wasingenyamazia ujinga kama huu.

Nitofautiane kidogo na wewe kuwa hawa jamaa sio wajinga wa sheria ila tatizo ni wapuuziaji tu kwa kuwa kikundi hiki hakiathiri maslahi yao....laiti ingekuwa ni kikundi kinachoathiri maslahi yao tungeshasikia kauli kibao za kulaani na hata tishio la JWTZ
 
Historia inatufundisha kwamba tawala kongwe zinapo karibia kusambaratika huwa watawala wanaunda makundi kama haya kuwatisha wapinzani wao,kuwatia hofu wananchi,kupora,kubaka na kuua. Mfano mzuri zaidi ni Interehamwe!
 
Suala la Vyama vya Siasa kuwa na vikundi vya Ulinzi halikubaliki kabisa.

Kama nchi yetu ingekuwa na Uongozi makini naamini kabisa suala hili lingeshapigwa marufuku siku nyingi.

Kuwa na Vikundi vya Ulinzi ie Green Guard, Red Guards, Cobra nk ni namna mojawapo ya kutengeneza mazingira ya umwagaji damu, uvunjifu wa amani na vitendo vya kikatili.

Nadhani ungewekwa utaratibu kwa vyama kutumia Jeshi la Polisi kwa ajili ya Ulinzi. Tumeshashuhudia matukio mengi ya kikatili yanayofanywa na vikundi hivi.
 
tunatengeneza magenge ya uhalifu kama Mungiki sasa ulu yawe yanatumika katika muda wa uchaguzi kutishia watu, uhalifu wa kura, kuharibu kampeni huru na za haki.

Yaani Tanzania inaelekea wenzetu wa mataifa mengine walipotoka au wanapojitahidi kutoka, sisi tunapiga spidi kuelekea huko.
 
Kumekuwa na Vikundi vyenye mtazamo wa Kijeshi ndani ya vyama vya siasa hapa nchini.

Mfano mzuri ni Green Guard,Janja Weed, nk. Mimi sina matatizo na Umoja wa vijana, isipokuwa vikundi hivi ambavyo vinamtazamo wa kijeshi. Je kila chama kikiwa na jeshi lake, matokeo yake ni nini? Vita itaepukika?

Wana janvi mnasema je?
 
Kabla ya mwaka 1992, tulikuwa na chama kimoja tu (CCM). Pamoja na kuwepo kwa chama kimoja tu, kulikuwa na kitengo cha Green guards (Askari wa Kijani) kitengo kilichodaiwa kuwa ni kitengo cha kulinda chama. Kutoka mwaka 1992 ambapo vyama vingi viliruhusiwa na hasa kuanzia 1995, Chama cha CUF ndicho chama Kilicho kuwa na nguvu katika vyama vya upinzani nacho kikaunda kitengo cha Blue Guard(Askari wa bluu) kwa hoja hiyo hiyo ya kujilinda. Jana baada ya CHADEMA kutangaza kuimarisha kitengo chao cha Red Guard(Askari wekundu), wakidai ni kwa lengo hilo hilo la kujilinda, umeibuka mjadala mkali kwamba ni nini lengo la CHADEMA kuwa na kitengo hicho na tena wakiimarishe sawa sawa.

Kimsingi kuna maswali ya msingi ambayo watanzania tulitakiwa kujiuliza kabla hata ya kauli ya CHADEMA jana.Jambo la kushangaza ni kwamba hakuna alie hoji wala kushangaa kilichokuwa kinaendelea hadi jana CHADEMA walivyozungumzia suala la kujiimarisha ki ulinzi ndio watu waka gutuka hee!.Hebu tusaidianeni kutafakari mambo yafuatayo.

1. Katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ina kataza mtu,chama au taasisi yoyote kuunda jeshi au chombo chenye muelekeo wa kijeshi “Para-millitary groups” ispokuwa serikali yenyewe. Kwa mfano; Katika sura ya tisa ya Katiba; inaeleza ;147.-(1) “Ni marufuku kwa mtu yoyote au shirika lolote aukikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali kuunda au kuweka Tanzania jeshi la aina yoyote” .Sasa pamoja na kifungu hiki cha katiba; CCM, CUF na sasa CHADEMA wana vikosi vya ulinzi ndani ya chama. Je inamaana ni ukiukaji wa katiba? Ikiwa ni ukiukaji wa katiba;

(a) Kwa nini CCM waliamua kukiuka,CUF walivyowaona nao wakakiuka na sasa CHADEMA nao wanakiuka?

(b) Ni kwa nini hili linaonekana sasa wakati CHADEMA imetangaza kujiimarisha katika kujilinda?

2. CCM ndiyo imetawala kwa kipindi chote toka tupate uhuru. Mwenyekiti wa CCM huwa ndio anakuwa Rais katika kipindi chote. Rais huwa ndio Amiri jeshi mkuu (wa majeshi yote) kwa mujibu wa katiba.Je! Green guard wana kazi ya kuilinda CCM dhidi ya nani?

3. Matendo yaliyowahi kufanywa na Green guards (CCM) tumeshawahi kuyaona, yaliyo fanywa na Blue Guard (CUF) Tumeshawahi kuyaona.Je;kwa vile yanavyoonekana ni matendo sahihi? Kama si sahihi, tumeshawahi kuyakemea?

4. Kazi za Jeshi la Polisi ni kulinda raia (wote bila kujali siasa) na mali zao, kulinda amani, kuhakikisha sheria zinafuatwa,kuzuia na kupeleleza uhalifu na kukamata uhalifu.Sasa;

(i) Je! CCM wana imani na jeshi la polisi?

(a) kama wana imani na Polisi kwa nini wameunda kikundi jeshi ndani ya chama kwa hoja ya kujilinda?

(b) Kama hawana imani; kwa kuwa wao ndio wenye serikali, kwa nini wasiliboreshe jeshi la polisi kinyume chake wanaanzisha vikundi vingine nyume ya pazia?

(ii)Kwa sasa CHADEMA wanadai hawana imani na Polisi na hata kudai kwamba wanaowashambulia wakati mwengine ni Polisi waliotumwa,Ikiwa ndio hivyo;kwa kuwa polisi ndio waliotakiwa wa hakikishe ulinzi lakini hawafanyi hivyo, na CHADEMA hawawezi kuwalazimisha kufanya hivyo,

(a)Waachetu waendelee kutokuwa na ulinzi na hatimae waendelee kudhuriwa? Au

(b)Waunde kikundi ulinzi (hata kama ni kinyume na katiba) lakini wajihakikishie usalama na hasa ukizingatia wa kabla yao walishaunda?

5. Kwa kuwa CHADEMA Wanaamini anaye washambulia mara nyingi ni Polisi (kwa maagizo ya viongozi wa CCM), Na sasa wanatangaza kuunda kikosi ulinzi kwa ajili ya kujilinda, na wakati huo huo CCM nayo ilishakuwa na vikosi vya Green guards toka siku nyingi na kazi zake mnazijua. Je;tutaraji,

(a) Kuona vikosi vya ulinzi vya Chadema vikiwadhibiti washambuliaji (ambao wanaweza kuwa Polisi)? Ikiwa ndio hivyo basi, na Polisi nalo ni jeshi tena halali na lenye zana kali za kivita tutaraji nini?

(b) Tutarajie kuona CHADEMA wakiwadhibiti wanaodhani wanataka kuwadhuru (yaani CCM) Na kwa kuwa CCM nao tayari wana vikosi vya Green Guard ambavyo mnavijua, Tutarajie mambano kati ya“ Two paramilitary groups”? (kwa kuwa vikundi ulinzi wakati Fulani huwajibika kutumia nguvu!).

Ushauri; Namshauri Rais kikwete aiangalie tena nchi hii. Ageuze uzo wake tena na tena azitizame mbio hizi zinazoendelea. Asichukulie mzaha hata kidogo kwa kudhani kuwa ni kuinusuru CCM kumbe mwishowe itakuwa dhahama kwa Taifa. Namsi Mh.Rais akumbuke kuwa kwa yeyote anaeshambuliwa. Ana machaguo mawili tu. Aache auawe, au ajikinge kwa njia anayoweza (hata kama ni kupambana).

Jambo la afya ambalo ni muhimimu kwa Rais; ni kukufanya juu chini kuhakikisha analirudisha tena jeshi la Polisi kuwa ni jeshi la watu (umma) na hivyo kufanya watu wote kuwa na imani nalo tena. Kwa kufanya hivyo kakuna Chama kitakacho fikiaria kuhusu habari za kujilinda . Hili linawezekana kwa kutoa amri moja tu ya kulitaka jeshi lisipendelee chama chochote hata kama ni CCM.
 
Nilimsikia msemaji wa Polisi akihojiwa jana na BBC. Alilaani sana Chadema kuunda kikosi cha ulinzi na kuwa ni uvunjifu wa sheria. Lakini alipoulizwa mbona CCM ina GreenGuard alishindwa kujibu kabisa pia kuhusu sungusungu alikosa pia majibu.
Tatizo la polisi ni kuona kila kifanywacho na CCM ni sawa kwa mujibu wa Sheria ila wengine sio sawa. Nawapongeza sana Chadema kwa kuliona hilo.
 
Back
Top Bottom