Nini maoni yako juu ya upatikanaji wa sera mpya ya Ardhi

Michael Chairman

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
922
583
Na sasa wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi imeanza zoezi la kukusanya maoni ya uboreshwaji wa sera ya Ardhi kutoka ile Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 ili kuiboresha ,zoezi hili limeanza mwaka 2016 ambapo ukusanyaji wa maoni haya unashilikisha kanda nane za Ardhi yaani kanda ya Dar es salaam, kanda ya mashariki, kanda ya ziwa, kanda ya nyanda za juu magharibi , kanda ya kusini, kanda ya magharibi, kanda ya kati na kanda ya kaskazini.
Sasa katika kuondoa changamoto kwenye Ardhi ambayo kwa Tanzania na nchi nyingine za kiafrika imeonekana balaa badala ya Baraka
my take nini maoni yako juu ya upatikanaji wa sera mpya?
 
Tutatoa vipi maoni ilhali hata hiyo sera mpya na sera ya zamani wananchi hatuzijui? Leteni kwanza sera zote kwa wananchi tuzisome na kuzielewa baadaye ndo mje mkusanye maoni yenu. Zaidi ya hapo mnampigia mbuzi gitaa.
Andaeni vipindi kwa television na radio elimisheni wananchi kuhusu hiyo sera waielewe halafu ndio mje mkusanye maoni. Sasa kwa hali hii ya sasa mtu anatoa vipi maoni?
 
1465572334110.jpg
 
Na sasa wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi imeanza zoezi la kukusanya maoni ya uboreshwaji wa sera ya Ardhi kutoka ile Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 ili kuiboresha ,zoezi hili limeanza mwaka 2016 ambapo ukusanyaji wa maoni haya unashilikisha kanda nane za Ardhi yaani kanda ya Dar es salaam, kanda ya mashariki, kanda ya ziwa, kanda ya nyanda za juu magharibi , kanda ya kusini, kanda ya magharibi, kanda ya kati na kanda ya kaskazini.
Sasa katika kuondoa changamoto kwenye Ardhi ambayo kwa Tanzania na nchi nyingine za kiafrika imeonekana balaa badala ya Baraka
my take nini maoni yako juu ya upatikanaji wa sera mpya?

Inaboreshwa kwa sababu iliyopo ina mapungufu gani?..tatizo ni sera mbovu au utekelezaji mbovu?..sera ina miaka zaidi ya 20 lakini walengwa hawaijui na hawajui hata kwa kuipata??...sera iliyopo ilitengenezewa mkakati? Sheria na kanuni? Utekekelezaji wake ulikuaje ktk kipindi chote hicho??..hii iliyopo ilitafsiriwa kwa lugha nyepesi ili hata wananchi wasio na elimu kubwa na walio kijijini waielewe??...hatuwezi toa maoni kwasababu hata kilichopo hatukijui ndugu
 
Umenena vyema moja ya matatizo yanazozikumba nchi za kiafirika ni hayo uliyosema mkuu sasa nini kifanyike kwa maoni yako
 
Na sasa wizara ya Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi imeanza zoezi la kukusanya maoni ya uboreshwaji wa sera ya Ardhi kutoka ile Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 ili kuiboresha ,zoezi hili limeanza mwaka 2016 ambapo ukusanyaji wa maoni haya unashilikisha kanda nane za Ardhi yaani kanda ya Dar es salaam, kanda ya mashariki, kanda ya ziwa, kanda ya nyanda za juu magharibi , kanda ya kusini, kanda ya magharibi, kanda ya kati na kanda ya kaskazini.
Sasa katika kuondoa changamoto kwenye Ardhi ambayo kwa Tanzania na nchi nyingine za kiafrika imeonekana balaa badala ya Baraka
my take nini maoni yako juu ya upatikanaji wa sera mpya?

Kwa sasa wananchi wengi wamekuwa na ardhi ambazo hazina hati licha ya kuwa kununua kwao kumezingatia vigezo vya baraka kutoka Kwa Balozi, Mwenyekiti wa serikali za mitaa na muuzaji wa ardhi ile.
Hivyo basi, Kwa maoni yangu ningependekeza:
  • Serikali ifanye utaratibu kila Raia wa Tanzania aliyenunua ardhi kupimiwa ardhi yake na kupewa hati ya umiliki, Hii itasaidia pia kwa wamiliki ardhi kuweza kulipa Ada ya ardhi na serikali kujipatia fedha vile vile kila mmoja atatambulika ni mmiliki wa ardhi husika.
  • Kwa zile ardhi ambazo hazijauzwa, wala hazimilikiwi na mtu Serikali iwe na taarifa zake na pia wazipime na uwepo utaratibu kuwa raia yeyote atakayetaka kununua ardhi apitie Serikalini, hii mambo ya kununua kienyeji yaishe ili kukwepa kuuziana mara mbili mbili ardhi.
Wananchi wengi wamekuwa na uoga wa kupimiwa ardhi na wahusika wa kazi hizo kwani imekuwa ni kama biashara, Umenunua kiwanja Milinoni 3, anayekuja kukupimia na kufuatilia hati anakuambia umpe Milioni 2, hivyo kupelekea raia wengi kumiliki ardhi zisizokuwa na hati wala hazijapimwa kwa sababu ya gharama hizi kuwa kubwa sana.

Tungeomba utaratibu ubadilishwe, iwe kupimiwa ardhi ni bure, kupewa hati ni bure sababu mwisho wa siku utakilipia kiwanja chako ambacho unamiliki Kodi ambayo inaenda serikalini.

Pia suala la uuzaji ardhi likirudishwa mikononi mwa Serikali yenyewe naamini kutakuwa na mipango miji mizuri, Mitaa katika nyumba na barabara zitapatikana. Na serikali itajua wapi pa kuuza na wapi ambapo hapafai kuuza hasa sehemu za mabondeni n.k.
 
Serikali ngazi ya Wilaya haiwezi kufanya kazi hii nchi nzima. Kuna mambo mengi kwenye maswala ya ardhi. Kuna mtu anataka kujenga, mtu anataka kuuza sehemu ya shamba, anataka kurithisha n.k. Swala hili wangehusisha kamati za ardhi za vijiji/mitaa/vitongoji ili mtu akitaka kuendeleza au kufanya biashara kwenye shamba lake fasta anamwona mtendaji wa kijiji wanatengeneza documenti zinazotambuliwa kiserikali. Halafu hiyo biashara iliyofanyika itangazwe kwenye mikutano ya kijiji/kitongoji ili kuongeza uwazi na kuzuia mianya ya rushwa.
 
Back
Top Bottom