moodykabwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2015
- 625
- 602
Nipende kutoa pole zangu za dhati kwa Watanzania wote pamoja na Waafrika kwa kupoteza Kiongozi jasiri na shupavu, Hayati Dk. John Pombe Joseph Magufuli ambaye alikuwa ni Rais wa Tanzania awamu ya tano.
Lakini tukiwa bado kwenye mwendelezo wa maombelezo ya siku 21 ya kitaifa ndipo anaibuka Mdhamini wa Klabu ya Simba ambaye nguvu yake ya kimkataba wa mahusiano yao ni umiliki wa hisa wa asilimia 49 huku Wanamsimbazi ikibakiwa na asilimia 51.
Napenda tuanzie hapa kwenye hisa kwani hizo namba 51 na 49 si namba tu bali zina maana kubwa sana ikiwa pamoja na nguvu ya kimamlaka, uamuzi na mapendekezo katika kuenenda ili kufanikisha mambo baina ya pande mbili husika.
Katika hali ya kawaida Klabu ya Simba wana nguvu kubwa kwani wao ndio wana sehemu kubwa ya umiliki ikiwa ni zaidi ya nusu ukiangalia kwa namba.
Hivyo napenda kwa pamoja tujiulize Mo Dewji anapoibuka na kuanza kudhihaki udhamini wa Sportpesa na Simba; tena amefanya hivyo tena kienyeji kabisa kwa kutumia ukurasa wake binafsi huku akiwa si Mwenyekiti wa Simba. Unajiuliza hiyo nguvu ameitoa wapi?
Katika hali ya kawaida na kiungwana udhamini wa Simba na Sportpesa umedumu kwa zaidi ya miaka mitano sasa huku Sportpesa wakihusika katika kulipa mishahara na huduma zingine za kiuendeshaji na kupata nafasi ya kuweka tangazo lao katika jezi za klabu husika.
Uwepo wa Sportpesa umesaidia mengi kwenye maendeleo ya Klabu ya Simba jambo ambalo ni la kushukuriwa hata kama kuna maeneo yana upungufu.
Katika kipindi hiki ambacho mkataba huo unaelekea ukingoni ilikuwa ni wasaa wa pande mbili kwa maana ya Simba na Sportpesa kukaa mezani na kujadiliana na kuona namna ya kuboresha ama laah, na endapo wasipofikia makubaliano basi kupitia Mwenyekiti wa klabu ambao ndiyo wenye hisa 51 ndio wangetoa mwelekeo tena kwa utaratibu maalumu, lakini cha ajabu anaibuka mdhamini ambaye naye ni mshindani wa kibiashara na Sportpesa na kutoa kauli yenye dhihaka kitu ambacho hakitoi taswira nzuri kwa wadhamini wengine na kunaweza kuweka mazingira magumu kwa wadhamini wengine kuja kuwekeza kwenye klabu ya Simba.
Lakini kwa dhihaka ambazo Mo Dewji amezitoa kwa Sportpesa kwa udhamini wao je yeye ambaye ameendelea kutumia nembo ya Simba na kuweka matangazo yake kwenye jezi za Msimbazi kila kona, ameifaidisha klabu kwa kiasi gani?
Udhamini wa MO EXTRA na MO HALISI unatoa tija kiasi gani kwa Simba SC. Je kinachotolewa na SPORTPESA kinafanana na wanachokipata Simba SC kupitia hizo bidhaa mbili ambazo Mo Dewji anazitangaza kupitia na nembo na jezi za Simba SC?
Leo atoke hadharani atuambie kila bidhaa anayoitangaza kupitia Simba SC kwa mwaka klabu inafaidika vipi na wanapata kiasi gani na kipo wapi?
Vilevile Wanasimba na Watanzania wanatakiwa waelewe kuwa Mo Dewji na makampuni yao sio wenye dhamana ya uongozi.
Hii ni kwa sababu wakati wowote na kwa sababu yeyote wanaweza kujitoa Simba kuamua kuingia ubia na kampuni yeyote hivyo kutumia nafasi yake ya udhamini wa asilimia 49 na kujivika nafasi ya Simba SC ni kosa na kuidhalilisha klabu kwani inaonekana haina nguvu na ule umiliki wa asilimia 51 hauna kitu wala tija ilihali wametoka kuchagua mwenyekiti mpya hivi karibuni.
Kwa alichokifanya Mo Dewji leo, Je ni makubaliano baina ya makampuni yake na Simba?
Au ni utashi wake? Kama ni utashi wake maana yake hatambui mipaka yake na yule Mwenyekiti wa Simba aliyepewa dhamana ya kulinda umiliki wa asilimia 51 yupo kama picha tu.
Biashara ni makubaliano inapofikia mmeshindwa kukubaliana ni vema mkaachana kwa amani huku kila mmoja akilinda heshma yake na heshma ya upande wa pili.
Leo kuja kuidhihaki Sportpesa ni sawa na si uungwana yapo mengi wameyafanya kwa klabu ya Simba.
Hili swala si la kiushabiki ni vema wanasimba mkaanza kuona namna ambavyo klabu yenu inavyokwenda kutaifishwa na kuwa timu ya familia na niliandika hili.
Leo hii zile shilingi Bilioni 20 zimebaki hadithi isiyokwisha wala hasemi ataziweka lini?
Amebaki anaruka kama maharagwe ya Mbeya na kuanza kuchokonoa wadhamini wengine ambao wanafanya kazi na Simba huku mkataba ukiwa bado upo na kuonesha dhihaka na dharau.
Najua wenye uwelewa na mapenzi mema na Simba watakuwa wamenielewa ila wale wachumia tumbo vichawa vya Mo Dewji watatafuta majibu rahisi juu ya hili, lakini pia wanachama ni wakati wa kujitafakari huku mkihoji mwenyekiti wenu mmemchagua kwa kazi gani?
Njia niliyotumia kwenda ndio nitakayorudia
Msemakweli wa haki
Nimemaliza