Nini malengo ya mke mchawi?

Nini malengo ya mke mchawi?

Kuoa ama kuolewa na mchawi ni gharama sana. Hawa viumbe roho zao ni za chuma
 
Ndugu zangu na wana jamii forums, nina maswali machache ambayo yanaitaji Msaada... Ni malengo gani mke mchawi anaweza kuwa nayo? Maana kama ananiloga nisifanikiwe kwenye ajira yangu na yeye anaathirika, Kama analoga watoto nayeye anaathirika, sasa swali langu ni kwamba ni malengo gani anaweza kuwa nayo kwa familia?

Mimi ni Mkristo, Mkatoliki, nimesoma, nimeajiriwa kama mkaguzi wa hesabu, sijawahi tegemea ushirikina hata kidogo kwenye maisha yangu!

Naomba majibu!
Asante nimekuja kwa kuchelewa japo natambua tuna mawasiliano tayari.... Sababu zipo nyingi lakini kati ya hizo nyingi kubwa ni hizi.....

1. Kurithishwa mikoba ya uganga... Hapa anaweza kuwa ni mama mzazi bibi ama hata shangazi.... Hawa wanaweza kuwa wafu ama wako hai...

2. Ushawishi wa marafiki... Mara nyingi kwenye harakati za kutafuta maisha ama kulinda mahusiano ama kutafuta mpenzi... Watu hukutana na marafiki wabaya na kuwashauri vibaya...
Inaana kama utani... Lengo likiwa ni kutafuta tiba tuu... Lakini baadae unajikuta unanogewa na kutamani kuwa mchawi kabisa

3. Upweke ndani ya mahusiano/ndoa
Harakati na changamoto za maisha hutufikisha mahali tukayapa mahusiano kisogo ama umuhimu mdogo.... Kwa wengine hutafuta nafuu kwa ulevi ama kuwa na mpenzi mwingine... Lakini wengine hujikuta wametumbukia kwenye ushirikia

4... Mahusiano ya siri na watu wasioleweka wanaofundisha unajimu, kinga, ngekewa nknk
 
Back
Top Bottom