Nini mahusiano kati ya AKILI na MOYO ktk Mapenzi?

Sazira kwetu

Senior Member
Aug 23, 2015
155
104
Kheri ya chrimas wana jukwaa, nilejee ktk mada yangu hapo juu,nimekuwa nikijiuliza mara kadhaa bila majibu juu ya mapenzi kuhusishwa na moyo.

Nielewavyo mim kila jambo alifanyalo binadam hulatibiwa na akiri ambayo ndiyo kiini cha kila tendo alifanyalo mwanadam.

Sasa toka nimekuwa nimesoma na ninaendelea kusoma bado hata sijapata sehemu iliyoandikwa kazi ya moyo nyingine ni kupenda au ni ishara au alama ya upendo au mapenzi.

Je ukweli ni upi moyo hupenda au akiri ndiyo hufanya kazi hiyo na kutunza kumbukumbu za hisia kwa yule umpendae?

Je kwa nini alama ya upendo huonyeshwa kwa mchoro wa moyo?
Je upendo ni zao la akiri au moyo?
Je nini uhusiano wa moyo,nafsi na akiri katika kupenda?

Natambua hapa kukwaani kuna wajuzi na wataalamu wa mambo mbalimbali nitapatiwa majibu na tutatapa kujifunza kwa undani kiini cha upendo.

Natanguliza shukurani zangu za kipekee kwa wanajukwaa wote.
Naomba kuwasilisha,
CC:kiranga,mseza mkulu,the bos na wengine wote mnakaribishwa.
 
kila shughuli mwilin huratibiwa na ubongo uhusiani wa picha ya moyo na mapenz nikumaanisha umpendae anaumuhim kama punz na punz kazi yake moyo ndio mchoro wa moyo iman akitoka waweza kata roho kitu ambacho unakuwa unawaza kutumia ubongo kwamba ukimkosa itakuwa hivyo
 
Me si mjuzi ila nahisi hivi.

Akili na moyo zinahusika ili kuleta balance.
Akili inakupa jeuri inakujuza kuna wanawake wengine kibao, moyo unapenda hautaki kuacha.
Moyo hurepresent nafsi in many cases, ndio maana huitwa soulmate.

Moyo kama kiungo kinasukuma damu, kwanini wanahusisha moyo na soul, nadhani sababu ya damu vile damu ndio wese la kufanya mwili ufunction, kama petrol/ diesel na gari.

Wajuzi watiririke
 
Kama leodigardcyrilo na Hoshea
Walivyokwambia Hapo juu,Moyo Hauna Mahusiano yoyote na Upendo
Emotional Activities zote zinaratibiwa na Ubongo.

kujibu Maswali yako ya Mwisho Ngoja nikupe Historia Fupi ya swali Lako;
Wamisri wa kale,walikuwa Wanaamini kuwa Moyo Ndiyo chanzo cha Roho,Hisia na kumbukumbu yaani soul,Emotion&Memory.
Hata wakati wa Mummificationwalikuwa wanauhifadhi Moyo na kuondoa Ubongo.

wazo Hilo lili-supportiawa na Aristotle.Aristotle Alifikiri kuwa Moyo,Ndiyo chanzo cha Akili/Intelligence,Hisia,na utambuzi au sensation
Kwa kuwa Aristotle Ndiye aliyekuwa Mwanafalsafa Mwenye ushawishi Mkubwa wakati ule.watu Wengi walimuamini.

Hata Baadhi ya Artists wengi na Waandishi wa Mashairi wakati ule,Walitumia Moyo kama Alama ya Upendo
Baadae Alama Hiyo Ikasambaa kwa kasi sana kuanzia karne ya 16 Mpaka Leo

Kwasasa Moyo unatumika Kama Metaphor au Lugha ya picha tu.

Wajuzi wengine wataendelea zaidi.
 
Last edited:
kazi ya moyo ni kusukuma damu na damu itembea vizuri ktk mihimili yake ndio akili hufikiria vizuri na kufanya maamuzi sahihi na ndio maana akili ikipata mshituko moyo unasimamisha kz yake hivyo maumivu ya moyo huja kwa haraka.
nataka kusema moyo na akili vinafanya kazi kwa pamoja havipishani hata kidogo
 
Kama leodigardcyrilona Hoshea
Walivyokwambia Hapo juu,Moyo Hauna Mahusiano yoyote na Upendo
Emotional Activities zote zinaratibiwa na Ubongo.

kujibu Maswali yako ya Mwisho Ngoja nikupe Historia Fupi ya swali Lako;
Wamisri wa kale,walikuwa Wanaamini kuwa Moyo Ndiyo chanzo cha Roho,Hisia na kumbukumbu yaani soul,Emotion&Memory.
Hata wakati wa Mummificationwalikuwa wanauhifadhi Moyo na kuondoa Ubongo.

wazo Hilo lili-supportiawa na Aristotle.Aristotle Alifikiri kuwa Moyo,Ndiyo chanzo cha Akili/Intelligence,Hisia,na utambuzi au sensation
Kwa kuwa Aristotle Ndiye aliyekuwa Mwanafalsafa Mwenye ushawishi Mkubwa wakati ule.watu Wengi walimuamini.

Hata Baadhi ya Artists wengi na Waandishi wa Mashairi wakati ule,Walitumia Moyo kama Alama ya Upendo
Baadae Alama Hiyo Ikasambaa kwa kasi sana kuanzia karne ya 16 Mpaka Leo

Kwasasa Moyo unatumika Kama Metaphor au Lugha ya picha tu.

Wajuzi wengine wataendelea zaidi.

einstein newton, hivi hujawahi kuhisi kitu alafu moyo ukarukaruka juu?
 
Last edited by a moderator:
kazi ya moyo ni kusukuma damu na damu itembea vizuri ktk mihimili yake ndio akili hufikiria vizuri na kufanya maamuzi sahihi na ndio maana akili ikipata mshituko moyo unasimamisha kz yake hivyo maumivu ya moyo huja kwa haraka.
nataka kusema moyo na akili vinafanya kazi kwa pamoja havipishani hata kidogo

hivi mtu akizimia akili inafanya kazi?
 
Ni kwamba, utakapwona mtu umpendaye basi hisia za upendo huo huanzia moyoni. Moyo utamwona umpendaye kwa kutumia madirisha yake ambayo ni macho. Lakini kama ilivyo kawaida ya maumbile ya mwanadamu, kitu chochote kikiingia mwilini lazima akili itambue.

Sasa kazi ya akili hapa ni kutambua na vilevile kuchambua kile kitu kwa ujumla. Unaweza ukapenda kahaba na akili ikajua kama huyu ni kahaba lakini moyo ukakataa kumuacha. Yaani akili kazi yake ni kutambua na kushauri hiki kitu ni sahihi au la.

Yaan kama kwenye familia basi moyo ndio mtoto amayependwa sana na wazazi wake. Kwa sababu moyo unapotaka kitu, kiwe kizuri kiwe kibaya basi unataka upate hapo hapo. Hata kama kipo nje ya uwezo wake hutamani hivyo hivyo. Chukulia mfano wa mdogo wenu wa mwisho anayependwa sana! Anapotamani kitu anakua katika hali gan? Basi ni sawa na moyo unapopenda sehemu.

Halafu akili ni kama Mzazi, kazi yake ni kuuongoza moyo. Ingawa akili inahofiwa kuumiza moyo kwa kumnyima kile moyo unachokitaka. Mtoto(moyo) anapolilia kitu baba(akili) kwa kujua kile kitu ubaya humnyima na kusababisha mtoto (moyo) kuumia. Lakini kama mnavyofahamu katika familia(mwili wa binadamu). Mtoto kipenzi (moyo) anapokosa raha basi familia(mwili) kwa ujumla nayo hufadhaika. Hapo ndo utaona mtu kula hutamani, usingizi hapati, na uwezo wa kufikiri hupungua.

Lakini kwa upande wa pili, moyo(mtoto) unapotaka kitu na baba(akili) ikatambua uzuri wa kile kitu na ikaweza kumtimizia basi moyo(mtoto) huwa katika furaha. Kumbuka moyo ukiwa na furaha basi maungo karibia yote katika mwili hustawi na kunawiri. Hii ni dhana ya kukonda na kunenepa. Nisiende sana huko.

Pia upande wa tatu, moyo(mtoto) unaweza kutaka jambo na akili(baba) ikathibitisha kwamba kitu hicho ni kizuri lakini akili ikashindwa kupata pia hii itapelekea moyo kuwa na huzuni. Lakini hii huzuni itatofautiana na ile ya akili kutokubali jambo husika. Hii mbali na moyo kulia lakini itatambua kama hiki kitu hatuna uwezo wa kukipata. Chukulia mfano wa mtoto anayetamani kitu ambacho anajua baba yake hawezi kumnunulia.

Kwa nini nasema akili ndo ina wajibu wa kumpatia moyo kile inachohitaji? Kwa nini akili nimeipa cheo cha kuwa baba?. Kwa sababu ndo ina control maungo yote(ni kwa matendo ya hiari tu). Kwa hiyo mbali na kupenda utahitaji kumfuata uliyempenda, ambayo ni kazi ya miguu(inaongozwa na akili). Pia utamwambia(mdomo unaongozwa na akili). Au kutuma sms(mkono unaongozwa na akili).

Kwa hiyo kama akili haitaki, haiwezi ikaamrisha viungo kufanya lolote. Na ndipo moyo unapozidi kulia na kupelekea viungo vingine navyo kutofanya kazi vizuri. Kwa sababu moyo(mdogo wao kipenzi) hana raha.

Note; akili ina nguvu ya kucontrol viungo vingine katika mwili wa binadamu lakini sio moyo. Akili ikitaka kuulazimisha moyo always panakuwa na bad effect.
Mada ni ndefu na siwezi kuandika yote hapa. Mtaniwia radhi kwa maelezo marefu. Naruhusu nikosolewe.
 
Ubongo ndo huendesha shughuli zote za mwili kama kusambaza damu mwilini na ikitokea mishipa ya damu ikaziba ubongo hujua ndani ya sekunde moja. Unaweza kuniambia kwanini pete ya ndoa huvaliwa kwenye kidole cha pili kutoka mwishoni?
 
kazi ya moyo ni kupenda na kazi ya akili ni kupambanua

Moyo kazi yake kusukuma damu basi...! Issues za kupenda ni minds/akili ambayo ni kazi ya ubongo tu basi. Hamna cha moyo moyo upo tu km ilivyo kwa bandama basi.
 
akili kazi yake ni kuendesha mambo yote yanayotokea mwilini ila viungo vingine mwilini huonesha effect mfano ukihisi njaa hapo akili iliishatambua zamani kwamba mwili umepungukiwa na ki2 fulani ss itatuma mawasiliano kwenye sehemu husika ndani ya mwili na ndo hapo utaona effect fulani inatokea ss kwenye suala hii la kupenda ni kuwa akili ndo itakuonyesha kwamba umevutiwa na msichana /mvulana fulani ss ili kuonesha effect ndo pale either utakapo muona huyo msichana/mvulana kuna impulse itatokea from ubongo na kufanya aina fulani ya hormone(adrenaline) kuzalishwa mwilini kisha moyo utaipamp hiyo hormone na kuweza kuisambaza mwilini kupitia damu na ndo hapo utaona mapigo yanaongezeka na kuona furaha kila umwonapo kwa kuwa akili imemkubali.
 
ss kwenye suala la kutendwa ni kuwa utakapo tendwa na huyo umpendaye ni kuwa utakuwa na mawazo mengi sana nahasira sasa hayo (mawazo + hasira) itapelekea ubongo ku overload kwa kuwa itapokea more than one impulse(ujumbe) na hivyo kusababisha uzalishwaji wa large amount of adrenaline hormone ambayo itaufanya moyo kuongeza kasi ya usukumaji damu mwilini hivyo pindi utakapozidi kuwaza kuwa umetendwa hii itapelekea moyo wako kuzidiwa na usukumaji damu wa haraka kwa muda mrefu na hivyo kuanza kutaka kurudi katika hali yake ya awali (na kumbuka hapo bado hormone inazalishwa na damu ni inamove rapidly) na hivyo kusababisha uhisi kama uchungu kwenye moyo ss hali hiyo ikizidi utakuta mwishowe moyo huchanika KWA HIYO MPAKA HAPI TUMEJUA KAZI YA MOYO NI MOJA TU KUSUKUMA DAMU NA MAHORMONE AMBAYO HUZALISHWA NA UBONGO KUPITIA CERTAIN EVENT NA SIYO KUPENDA. ANGALIZO UTAKAPOTENDWA JARIBU KURELAX HAPO UTAUPA UBONGO POSITIVE MESSAGE KWAMBA UKO RELAXED NA HIVYO KIPUNGUZA KIWANGO CHA UZALISWAJI WA HIYO HORMONE NA UTAENDELEA VIZURI TU.
 
Nawashukuru sana wadau WOTE mliochangia na kuidadavua mada hapo juu

Shukurani za kipekee ziende kwa Einstan newton aliyetoa historia ya alama ya moyo kuonyesha ishara za mapenzi au upendo,na Smigo4u kwa kutupa uhusiano uliopo kati ya akiri na moyo ktk kupenda au upendo.

Nilichojifunza kutoka kwa wanajukwaa hapo juu ni kuwa alama ya moyo ktk kuonyesha ni ya upendo ni ya kihistoria zaidi kuliko uhalisia

Pia kingine nilichojifunza ni kuwa akiri ni main control wa mambo yote ayatendayo mwanadam,na moyo huhusiswa na upendo kwa kutumia Homone ya Adrenaline pale tu akiri inapomkubari au anaposalitiwa.

Maswali hayo yote nilishajiuliza kwa mda mrefu lkn kupitia Jamii foram nimepata majibu ya maswali yangu

Sasa nimeamini
Jamii foram is the home of great think where we dare to talk open.

Karibuni wadau wote tuendelee kuchangia mada hapo juu maana elimu ni kiini cha maarifa na maarifa ni chakula cha afya ktk kuujenga ubongo.
 
Back
Top Bottom