Nini maana ya WOZA (shairi)

kaburunye

JF-Expert Member
May 12, 2010
672
74
Nini maana ya WOZA, naomba kuulizia
Neno linanitatiza, kila nikifiria
Wale nilowauliza, jibu hawakunipatia
Nipeni maana yake, wale mnaofahamu.

Nilimwuliza ayubu, jibu hakunipatia
Akajifanya ni bubu, nilipomfuatilia
Nasemwa sina adabu, swali nikiulizia
Nipeni maana yake, wale mnaofahamu

Kwangu hili neno geni, nawaambia ukweli,
Maana yake ni nini, lijibuni langu swali
Msiingie mitini, nipeni jibu la kweli
Nipeni maana yake, kwa wale mnaofahamu

Hapa tamati nafika, mbele ninaona giza
Mwenzenu mi nimechoka, mambo yamenitatiza
kuendelea nataka, moyo unanikataza
Nipeni maana yake, kwa wale mnaofahamu
 
hilo jibu umepata sasa furahia,

kiliocho mwanasayuni kakitibia,

Ayubu rafikiyo wende kumwambia,

jibu ndo hilo aweza kuongea.

Haya sasa na mie nilokwandikia?


kipi taja nipatia?

mie soda tu taninunulia.

naye wa syuni namwombea,

Mpe japo kitabu cha Biblia.

wanakondoo wengi kuongozea.

Tamatini kama weye Woza sikuijua.

Akhsante mwanasayuni sasa Twasherekea.
 
kwanini laandikwa kwa herufi kubwa?
ni kikabila chao sauzi au limetoholewa?
 
Kaburunye na mzioni, Aza, Mswahiliani
pole nawapatieni, jibu lingojeeni
WOZA neno pijini, litilie maanani
World Cup South Africa..na kifupi cha South Africa kwa country codes ni ZA! hence the infamous..WO-world cup-ZA-south Africa!

Nadhani mmenipata, japo beti zimenuna
maana nimeikita, sitaki kugunaguna
iwasilisheni Bakita, kwa Ayubu na Amina
WOZA kweli kifupi, Zioni unasemaje!???
 
Compaq nakushukuru, kwa jibu lako makini
kijana wa kinyaturu, jibu nimeliamini
Usinidai ushuru, nikakimbia porini
Kwa kweli maana ya WOZA, kwa sasa nimeelewa
 
Sijui mie nilisoma lini....
Jamani mnanifurahisha na hii mistari.
 
Back
Top Bottom