Nini maana ya uwekezaji katika madini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini maana ya uwekezaji katika madini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ringo Edmund, May 19, 2012.

 1. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  nimekuwa nikitafakari hizi sera za serikali ya ccm awamu ya tatu na nne nakosa jawabu naombeni wana jf mnisaidie.
  Kuna kauli zinatolewa kila wakati na uongozi wa juu kuwa mitaji inagombaniwa duniani na hivyo ni kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji ili kuwakaribisha ncini.kuna baadhi ya sekta naona si sahihi kuwaita wawekezaji ,nitafafanua kuhusu sekta ya madini ila ziko nyingi kama mbuga za wanyama nk.
  Ningewaelewa sana kama katika madini wangeitwa madalali kwa sababu mwekezaji ni yule anayekuja kutumia rasilimali ulizo nazo na kuzalisha bidhaa.kwenye madini si hivyo wanakuja kuchimba madini yetu na kuuza.
  Walitakiwa wanunue madini na kuzalisha vito na kuviuza nchini na nchi za nje na kulipa kodi,wanochokifanya sasa ni udalali na walikuwa wanastahili kulipwa 10% kwa sababu ya kazi wanayoifanya.sasa badala yake sisi ndio tunaolipwa kama madalali.
  Haya madini kayaweka mwenyezi mungu na anahitaji sadaka je sisi tuliokabidhiwa hayo madini tutalipaje sadaka?ni katika madini yote au ni katika gawio letu kama madalali?

  Mimi nafikiri ni jukumu letu kama taifa kukaa chini na kuangalia maana ya uwekezaji ili tusiendelee kuliuwa hii taifa kwa sababu ya njaa za viongozi wetu?
  Ukijiuliza kati ya kuchimba na madini yenyewe ni kipi chenye gharama kubwa?unaweza ukajibiwa ni gharama za uwekezaji na kama ni hivyo hiyo biashara ni kichaa,haifai na kama ni madini kwa nini tunalipwa kidogo kwa kitu ambacho hakizai?

  Hayo ni maoni yangu naombeni mwenye uelewa wa zaidi.
   
Loading...