Nini Maana ya Ugonjwa Wa Autism? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini Maana ya Ugonjwa Wa Autism?

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Nov 1, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Autism


  [​IMG]

  Tabia za kawaida, hupanga vitu juu.​  Autism ni tatizo la kiroho na kihisia linalotokea kwa watu tangu utotoni na kuathiri uwezo wao wa kuwasiliana na watu wengine. Watu wenye matatizo ya autism hawaonekani kama watu wa kawaida. Muda mwingine hawapendi kuwaangalia wengine pale wanapozungumza nao, au hawapendi kushirikiana mambo mengine na watu wengine. Pia, hawapo vizuri katika kimawasiliano. Muda mwingine wanakuwa

  hawawezi kuongea, au kuzungumza na watu wengine. Mwishoni, hujijibu wao wenyewe. Wanaweza wakawa na shauku na kitu ambacho mtu mwingine ambaye hana matatizo ya autism asifikirie kama kina umuhimu. Mtu mwenye tatizo hili anaelekea mara nyingi kurudiarudia matendo kadhaa, na anaweza kuhofia vitu katika mazingira yake yasiyoelewka kama tatizo na wengine.

  Dalili
  za autism

  Kukaa peke yake

  Mtoto wa kawaida asiye na autism huwaangalia watu wakizungumza, hutazama wengine usoni, hutabasamu, na huwa na shauku na watu wengine. Watoto wenye autism, wanaweza kupenda vituvitu zaidi kuliko sura au watu wengine. Wanaweza wakatazama usoni kwa

  sekunde tu, halafu mara moja akageuka. Wanaweza wasitabasamu, au wanaweza wakatabasamu kwa kitu kile alichokipenda.

  Watoto wenye matatizo ya autism huwa na kawaida ya kukaa wenyewe tu, bila kuwepo kwa wengine. Wanaweza wasiwe na shauku ya

  kutaka urafiki na mtu yeyote. Pia, wanaweza wasiwe wanafanya kawaida kama kukumbatiana na alama nyingine za upendo kwa wazazi wao. Hii haimanishi kama hawa wapendi wazazi wao, ni kwamba hawajui namna ya kusema hivyo vitu.


  Wanaweza wasione hisia za watu wengine; kwa mfano, wanaweza wasione tofauti kubwa sana kati ya labda mzazi ana furaha ma ana uzuni. Wanaweza wakacheka na kulia kwa mara zisizoeleweka.


  Kutozungumza


  Mtoto mweye autism anaweza asithubutu kuongea, maana, au kujaribu kuelewa maongezi kati ya mwenzie mwenye umri sawa. Kuna baadhi yao huwa hawaongei kabisa. Wengi wao hawawezi kuongea vizuri na watu wengine.

  Kufanya vitu tena na tena zaidi


  Kuna baadhi ya maautistic hutumia muda mwingi kufanya vitu vimoja kwa mara nyingi na nyingi zaidi, au kuwa na shauku na vitu ambavyo si vya kawaida; kuna baadhi yao wanaweza kutumia muda mwingi kwa kujizungushia mkono wake, kutembea na visanamu vyao, au

  kuvipnga vitu kwa mpangilio mmoja. Watu wenye matatizo ya autism wanaweza wakatumia muda mkubwa kwa kupanga visanamu vyake kwa mstari mmoja au vyumbavyumba na wanaweza kusikia jazba pindi mtu akavivuruga pale katika eneo lake.


  Baadhi yao hawataki badiliko lolote lile, na wanaweza wakafanya mambo yaleyale kila siku bila kubadilisha—kama vile kuto kula, wanapokula, wanavaa, wanapiga mswaki, au pale wanapokwenda shule—huwa na uzuni kama kuna badiliko lolote katika vitu hivyo. Pia, wanaweza wakawa na shauku na vitu vya ajabu na kutumia muda wao mwingi kujifunza vitu hivyo.


  Historia


  Autism lilipewa jina kwa mara ya kwanza mnamo 1943. Leo Kanner alifanya utafiti huu kwa watoto wapatao 11 na akagundua vitu ambavyo si vya kawaida kuhusu wao. Aliita early infantile autism. Muda huohuo, daktari mwingine, Hans Asperger, akafanya utafiti mwingine karibuni kitu sawa. Alichogunda sasa kinaitwa Asperger syndrome, wakati alichogundua Leo Kanner kinaitwa autistic disorder, childhood autism, infantile autism, au tu autism.


   
 2. k

  kichwakipana Senior Member

  #2
  Oct 1, 2014
  Joined: Jun 18, 2013
  Messages: 195
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kuna dawa ya kutibu autism
   
 3. gody

  gody JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2014
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 1,227
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Je, akishakuwa mtu mzima anakuwaje?
   
 4. gody

  gody JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2014
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 1,227
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. U

  Undu JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2014
  Joined: May 18, 2013
  Messages: 1,745
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  Hakuna dawa zaidi ni kumpeleka mtoto mwenye autisim kwa occupation therapist afundishe kazi za kufanya ili kumjenga kiakilu
   
 6. Mishughuliko

  Mishughuliko Member

  #6
  Apr 17, 2015
  Joined: Oct 30, 2013
  Messages: 46
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  tufanyeje wenye watoto wa aina him?
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2015
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Asipotibika wakati yupo mtoto anakuwa mtu mzima anakuwa mtu mwenye akili ya tahira Mapepe.
   
 8. Pampula jr

  Pampula jr JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2015
  Joined: May 2, 2013
  Messages: 612
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  nahitaji unielekeze nifanyeje maana nina mtoto ana tatizo hilo na ana umri wa miaka mitano sasa na haongei ni kama bubu
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2015
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kama imeshindikana hospitali kumtibu mwanao nitafute kwa wakati wako ukihitaji mimi bonyeza hapa.Mawasiliano
   
 10. bukoba boy

  bukoba boy JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2015
  Joined: Jan 15, 2015
  Messages: 4,739
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Huu ugonjwa upo ulaya zaidi.
   
 11. S

  SHILOTI New Member

  #11
  Apr 3, 2017
  Joined: Mar 20, 2017
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  sasa ndiyo nimeelewa maana nilikuwa sijaelewa eti!
   
 12. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #12
  Apr 3, 2017
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,057
  Likes Received: 1,193
  Trophy Points: 280
  Kuna jamaa mmoja alichemka kazi sehemu kaamua kuwa balozi wa huu ugonjwa ,nahisi at a yy anaumwa hii kitu
   
 13. k

  kilama JF-Expert Member

  #13
  Apr 3, 2017
  Joined: Jul 14, 2015
  Messages: 1,410
  Likes Received: 669
  Trophy Points: 280
  Kama nimechelewa kukujibu kama mdau alivyokujibu hapo juu. Yakupasa kumpeleka mtoto kwa watu wa occupational and physical therapists watamsaidia sehemu kubwa sana hata kama hataweza kurudi kwenye normal kabisa lakini angalau atakuwa mtu miongoni mwa watu. Tatizo la language pia linatibika japo si kwa dawa ila na mtu anayeitwa language therapist.
   
 14. k

  kilama JF-Expert Member

  #14
  Apr 3, 2017
  Joined: Jul 14, 2015
  Messages: 1,410
  Likes Received: 669
  Trophy Points: 280
  Kuna kitu kinaitwa Early Intervention hapo mtoto atapata angalau kwa kiasi kikubwa sana.
   
 15. k

  kilama JF-Expert Member

  #15
  Apr 3, 2017
  Joined: Jul 14, 2015
  Messages: 1,410
  Likes Received: 669
  Trophy Points: 280
  Kama nitakuwa nimechelewa sana kukujibu nenda /mpeleke mtoto kwenye Kituo cha watoto /watu wenye mtindio wa akili hao wengi wanakuwa na huduma za occupational and physical therapy. Kwa umri wa miaka mitano bado haujachelewa sana atakuwa okay kabisa. Kwa ifakara kuna Kituo kinaitwa Bethlehem ni cha kanisa katoliki kipo vizur sana. Kuna wanafunzi waliolelewa hapo then badaye tukaungana pamoja shule ya msingi tukamaliza walikuwa okay japo wengi wao walikuwa na mental retardation.
   
 16. k

  kilama JF-Expert Member

  #16
  Apr 3, 2017
  Joined: Jul 14, 2015
  Messages: 1,410
  Likes Received: 669
  Trophy Points: 280
  Nina baadhi ya video za occupational and physical therapy.
   
 17. KingKacha

  KingKacha Member

  #17
  Jan 18, 2018 at 9:12 PM
  Joined: Jun 15, 2016
  Messages: 64
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 25
  Wataalam wanasema kwamba, tusiseme ugonjwa. Hii ni hali inayompata mtoto eitha akiwa tumboni au akiwa anakua na huja kuonekana mtt akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu.

  So kiufupi nasema si ugonjwa kwakuwa utaratibu wa kuwasaidia huwa hauinvolve dawa. Ni kumfundisha tu.

  Na wengine huwa vizur kuliko binadamu ambaye hajawah pata hali hiyo..

  Kwahiyo kama una mtt wa aina hiyo Mshukuru Mungu tu. Si jambo baya iq zao pia huwa juu zaidi na wanaweza kuperfom katika viwango vya juu kuliko unavyotegemea katika fani flan atakayoichagua kwakuwa akikipenda kitu hukipenda hasa na asichokipenda hawez kukipa umuhimu hivyo humsaidia kuwa makini na vitu vichache na kuvifuatilia sana
   
 18. w

  wakurochi Member

  #18
  Jan 18, 2018 at 10:12 PM
  Joined: Dec 4, 2017
  Messages: 36
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Asante sana mtaalam nilipata kuona kwenye youtube mngonjwa mmoja wa hiyo autism alikuja kuwa na kipaji cua kuchora hatari tupu, yaani anatisha. Mjengo kama ile Ikulu yetu anaangalia dk 10 halafu anaomba karatasi,baada ya masaa anakuwa amemaliza. Ila wanasema hajapona bado. Mtafute youtube stephen Wiltshire. Kama ana tatizo kama hilo basi Mungu ni wa ajabu sana
   
 19. storyteller

  storyteller JF-Expert Member

  #19
  Jan 18, 2018 at 10:39 PM
  Joined: Nov 5, 2014
  Messages: 564
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 80
  Autism - usonji
   
Loading...